SWALI LA KIZUSHI: Kwa nini aliyepata Divisheni Ziro azuiwe kujiunga Chuo?

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Nimepata divisheni ziro. Nimependa kujiunga kozi chuo. Ada nitajilipia mwenyewe. Mkopo sitaki. Kozi ina nafasi. Kwa nini nizuiliwe kujiunga na kozi ya digirii chuo?

Nikienda chuo na ziro yangu, si nitafeli tu mwaka wa kwanza kama kweli ziro ina maana sina uwezo? Nitakayepata hasara si ni ni mimi? Nyie kinawauma nini?

Kama nisipofeli masomo ya chuo, digirii itakuwa na mapungufu gani mimi kuipata, hata kama nina divisheni ziro huko nilikotoka?

Enzi za ujamaa wakati kila kitu serekali ilikuwa inalipia, ilikuwa sawa kuweka masharti nani ajiunge chuo. Hivi sasa si kila mtu analipiwa na serikali. Kwa nini kuwe na vizingiti kujiunga na elimu ya juu?

Nawasilisha.
 
Unaweza kwenda kupiga picha au kuomba kazi ya uhudumu kanteen
 
Una pointi za msingi Seema nyie mnaofeli au kupata ufaulu hafifu huwa ni wajanja sana ukishapa hicho cheti Cha kumaliza degree ajira fasta mara madaraka baada ya muda mfupi mnawaacha wenye ufaulu mzuri wakisota.
 
Unaweza kwenda kupiga picha au kuomba kazi ya uhudumu kanteen

Asante. Hilo nalo wazo. Nitapiga picha na kuhudumu kantini huku nikisoma chuo. Nasikia mamtoni hayo ni kawaida. Unatisha mkuu.
 
Una pointi za msingi Seema nyie mnaofeli au kupata ufaulu hafifu huwa ni wajanja sana ukishapa hicho cheti Cha kumaliza degree ajira fasta mara madaraka baada ya muda mfupi mnawaacha wenye ufaulu mzuri wakisota.

Hapo tatizo liko wapi? Fursa sawa iwe kwa wote. Kupata ziro siyo mwisho wa dunia. Ni siyo?
 
Sioni tatizo wewe ukijiunga chuo swali linarudi kwako, huko chuo utaenda kusomea masomo gani wakati yote ulishafeli sekondari?
 
Sasa wewe umepata div zero unataka uende chuo ukasomee nini ndugu yangu!!?
Au ndo unataka uende ukasomee jinsi ya kupata zero cha msingi sasa hiv tafuta tu bustani ulime mboga mboga

Nitasoma chochote ada yangu itakachomudu. Kwa nini mugeuke Mugo wa Kibiro kutabiri yajayo kwamba nitafeli chuo kwa vile tu nilipata ziro sekondari? Hata kama nitafeli, nyie inawahusu nini? Si ni ada zangu mwenyewe?

Kama tunataka ufaulu basi chuo waende waliopata Divisheni Wani ya Pointi Saba O-Levo na pia Divisheni Wani ya Pointi Tatu A-Levo. Na akifika chuo asipewe digirii labda awe amepata Jipiei ya 5.0. Pungufu ya hapo wote tumefeli, tunapishana tu viwango. Sasa kwa nini tuchekane na kubaguana?
 
Una pointi za msingi Seema nyie mnaofeli au kupata ufaulu hafifu huwa ni wajanja sana ukishapa hicho cheti Cha kumaliza degree ajira fasta mara madaraka baada ya muda mfupi mnawaacha wenye ufaulu mzuri wakisota.
Wana uwezo mkubwa wa kujiongeza,halaf pia Wana maneno ya shombo.
 
Ndiyo maana AFCON tulitolewa wa kwanza kwa mambo ya kulazimisha

Zile zinaitwa fainali -- tulivyotolewa ni sawa na kupata digirii isiyo na JiPiEi ya 5.0. Haidhuru. Nasi tumeshiriki.

Tungejisikiaje CAF ingesema, hata nyie kichwa cha mwendawazimu 😳 mnataka kushiriki fainali? Tunajua tu mtatolewa hatua za makundi. Msije Misri! Huoni huo ungekuwa uonezi?
 
Unapofeli kwenye eneo moja, ni fursa nyingine ya kuongeza juhudi kwenye eneo hilohilo au kujaribu eneo jingine. Kama umefeli shule basi jaribu kazi za nguvu kama kilimo, uvuvi, biashara, kucheza dance n.k
Lengo la kukupatia elimu wewe si tu ikufae wewe, bali hata jamii inayokuzunguka inufaike. Sasa kila taaluma ina sifa zake kulingana na uzito wa taaluma yenyewe, sasa sifa za kuingilia kusoma hizo kozi huna, maana yake hufai. Kulazimisha kukuchukua ni kutaka kujaza nafasi ambazo zinawastahili wenye sifa zao ambazo huna.
 
Sioni tatizo wewe ukijiunga chuo swali linarudi kwako, huko chuo utaenda kusomea masomo gani wakati yote ulishafeli sekondari?

Chuo nasikia mkifika mnaanza sufuri. Mwalimu anawafundisha mwenyewe, anatunga mtihani mwenyewe, anasahihisha mwenyewe, maksi anatoa yeye. Unafelije kwa mfano? Ukifeli unapewa supu, unarudia mtihani. Ukiifeli mtihani wa supu unarudia tena somo mwaka mwingine. Nani atashindwa shule ya hivyo?
 
Back
Top Bottom