Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,436
- 4,151
Katiba inayotakiwa kubadilishwa ni katiba ya Jamhuri ya muunga wa Tanzania na si ya Zanzibar. Na hata ikibadilishwa hiyo ya Muungano na kuweka serikali tatu , ya znz ya muungano/shirikisho na ya tanganyika bado katiba ya znz itaendelea kusomeka kama inavyosomeka sasa.
Na hata hii katiba inayopigiwa ukunga haiandikiki ikaisha leo ni jambo ya muda 2,3,4,5 years pengine so meanwhile tunayo hii ya sasa "titi la mama tamu hataka kama la mbwa" tuiheshimu na kuheshimu maoni ya wananchi wa Zanzibar tusiwabeze na kuwajeli. Nadhani CDM inahitaji wanachama kule ili kiwe na sura ya kimuungano zaidi basi ushauri wangu ni kuwa wasiwadhihaki wazanzibar kwa maneno ya kejeli wao ndio waliopiga kura za maoni na si kama inavyozungumzwa na viongozi wa CDM kuwa CCM na CUF wao ndio wamepanga.
Mkuu hapa ujumbe wako uko wazi zaidi: hujafurahia bezo za CDM kwa muungano wa CUF na CCM huko Z'bar. Hilo ni jingine. Lakini ukirejea kuhusu CDM watafanya nini wakifanikiwa kufikia ushindi wa kwanza au wa pili huko Zanzibar basi hauna budi kujiuliza kwanza CDM wana visheni gani kuhusu ushiriki wao kwenye serikali ya Z'bar? Ndipo ninapojibu kuwa sioni kama CDM wana mpango wa dhati wa kushika uongozi wa serikali huko Zanzibar.
Nionavyo, kama mambo yakienda kama wanavyotaka (katiba mpya) basi Zanzibar inaweza kuongozwa na chama kingine na wao wakabakia bara (sitaki kusema Tanganyika) na kushirikiana kwenye serikali ya muungano kulingana na katiba mpya itakavyoainisha.