Nadhani watu wengi akiwemo mwanakijiji bado awajatambua ukweli na chimbuko la matatizo na kuwa lawama zinaenda kwa wasiostahili.
Tatizo linalotokea sasa ni kosa lililopitishwa na bunge letu mwaka 1992 baada ya kupitisha mswada wa TISS act 1992 ambayo iligeuza usalama wa taifa toka chombo cha utendaji na kuwa chombo cha ushauri. kabla ya hapo usalama wa taifa walihusika moja kwa moja katika kugundua na kuzuia jambo lolote lenye madhara kwa taifa lakini kwa sasa wao kazi yao ni kuchunguza na kutoa mapendekezo kwa serikali na si kazi yao kuona kwamba yamefanyiwa kazi au lah kwani wao si watendaji.
kwa sheria hii ya TISS act ya 1992 inamaanisha ata usalama wa taifa wakigundua kuna meli imebeba mabomu inakuja katika nchi yetu wao kazi yao si kuizuia bali ni kutoa taarifa ya ujio wa meli hiyo na kama vyombo husika vikishindwa kuizuia wao wataacha iingie na ata ilipue taifa letu kwani ni nje ya kazi yao.
Godwine, Mwanakijiji ametumia neno 'overhaul' meaning unajenga upya - kama ni sheria, mabati, ukuta, zege whatever.... overhaul. Kwa hiyo kama tatizo ni sheria basi exercise ya overhaul ndiyo itamaliza.
Last edited by a moderator: