Swali la kizushi, HIVI MTU MZIMA NI KUANZIA UMRI GANI? Tanzania 50 yrs lakini bado haijitegemei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la kizushi, HIVI MTU MZIMA NI KUANZIA UMRI GANI? Tanzania 50 yrs lakini bado haijitegemei

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Chilisosi, Aug 30, 2012.

 1. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Naomba tu ufafanuzi kwenu wadau,
  Nchi yetu leo ina miaka 50 ya uhuru lakini bajeti yake inategemea misaada na haiwezi kujiendesha bila misaada toka nje.
  Angola wamepigana vita miaka ishiri leo wanatuzidi kwa utajiri
  sie tunachojivunie ni eti tuna amani kuliko nchi nyingine.
  Tuna kila kitu lakini bado tunaongoza kwa kutembeza bakuli.
  Mie nadhani tanzania chini ya CCM ni sawa na mtoto ambaye hakui kwa mama yake unakuta jibaba zima lina miaka hamsini bado linakaa kwa mama yake na linadeka hadi hela za sigara linamtegemea mama
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wa Tanzania wengi ni waoga wanaona bara amani afe na dhiki! tuombe tu Mungu awabadilishe mioyo yao bila hivyo... Heri kwenda msituni dhidi ya hawa wakoloni weusi!
   
 3. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  Pamoja na mada yako kutokuipangilia vizuri lakini ujumbe umeeleweka.

  Kwangu mimi swala la umasikini wetu ukiliangalia kwa upana zaidi limesababishwa na mambo mengi. Kubwa zaidi ni siasa ambazo waasisi wa nchi yetu waliamua kuzifuata(Ujamaa na kujitegemea) ambazo mara nyingi nchi ilikuwa inaendeshwa kwa utashi na fikra za mtu mmoja( zidumu fikra za mwenyekiti). Siri ya maendeleo ni pale ushindani unapokuwepo kwenye jamii. Nina maana hata fikra lazima zipate ushindani. Tanzania tulidumaa kwa zaidi ya miaka ishirini kwa kukosekana ushindani. Mfano kidogo tu. Baada ya CHADEMA UK kutangaza swala la mfuko wa kufa na kuzikana. Kwa sasa NSSF wameamuka na tumeanza kuwaona wakinunua matangazo ili kupitisha ujumbe wao kwa diaspora. Hii inaonyesha kuwa walikuwa wamedumaa kwa vile hawakuwa na challenge.

  Swala la kulinganisha uchumi na maendeleo kati ya nchi mbili haliwezekani kwa vile nchi zina resources tofauti. Kwa sasa Angola wanauza zaidi ya barrels millioni mbili za mafuta kwa siku achilia mbali almasi. Halafu nchi ni ndogo yenye watu millioni 19 hivi wakati Tanzania hatuna mafuta na nchi ni kubwa yenye watu zaidi ya millioni 43.

  Unakuwa huitendei haki Tanzania pale unapolinganisha na Angola. Mtu mwingine anaweza kusema Kwa nini basi usilinganishe na Malawi? Ambayo pia imekuwa na amani kwa kipindi kilefu lakini uchumi wake siyo mzuri wakati hata ina watu wachache
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Utu uzima unaanza nchi inapofikia miaka 50.
  Bado miaka miwili Tanzania kufikia miaka 50. Na hapo ndio mwanzo!!!!
  Nchi yenye miaka 50/51 ni nchi ambayo jina lake tumepigwa marufuku kulitaja ila jina lake la utani ni (Bara/Tz bara)
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hii ndiyo ilikua sababu kubwa ya wakoloni kututawala, kwamba hatukua tayari kujitawala.
  Wakoloni weusi nao wameiga somo.
   
 6. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  NONDA.
  Nasikia tanzania bado inakua na ccm wanadai nchi yetu bado changa
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Congo(Zaire) nayo pia inakua?
  Kuna mikakati wa kuifanya Tz kama Congo.

  Wajanja wanahamisha mali, wananchi wanabaki kufungasha viroba na kuhama hama kama hawana nchi na kuambiwa wafunge mikanda. Hiyo iko njiani.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
Loading...