VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
CCM ni chama tawala,kwa maana ya kuunda Serikali iliyopo madarakani kwa sasa. Bungeni napo,CCM ina wingi usio na shaka wala mawaa wa Wabunge. Hadi hapo,CCM inatawala mihimili miwili ya dola kati ya mitatu: Serikali na Bunge.
Kwa ukongwe wa CCM kama chama cha siasa,inategemewa kuwa imesheheni wasomi,wabobezi na wajuzi wa mambo mbalimbali ya kinchi na kisiasa. Haitegemewi chama kikongwe kama hiki kiogope hoja kuzisikia na hata kuzijibu. Wataalamu wa kujibu hoja za wapinzani wako tele. Woga unatoka wapi?
Kwa hoja za Lugumi,mauaji ya wanasiasa wa upinzani,tabia za Rais,kulindwa kwa Chenge na uuzwaji wa nyumba za Serikali,CCM na Serikali yake ilipaswa kutoa majibu ya kina. Majibu yapo. Haikupaswa kuogopa na hata kuitisha caucus ya kasi. Hakukuwa na haja ya kufuta mambo hayo kwenye hotuba ya wapinzani. Wangejibiwa na kutulizwa kw majibu mujarabu yasiyo na tabu!
Woga hauna nafasi kwa CCM. Hoja zijibiwe kwa hoja bila kungoja wala kujikongoja!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam