Swali la Dhali: Kwanini unaliamini Bunge zaidi vita dhidi ya Ufisadi kuliko Mihimili mingine?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,992
2,000
Nimegundua baada ya ushabiki mkubwa ulioonekana Bungeni wakati wa sakata la escrow kuwa wapo watu kati yetu ambao wanaamini sana Bunge katika vita dhidi ya ufisadi kuliko mihimili mingine. Ninajaribu kuelewa hasa ni kwanini baadhi ya watu - kama ni wengi au la sina uhakika - wanaamini sana Bunge kiasi kwamba wako tayari kutoangalia rekodi ya Bunge vita ya ufisadi na kuacha lionekane linaoongoza vita hiyo kuliko mihimili au taasisi nyingine. Nina maoni yangu kuhusu hili lakini sijui wengine ambao wanaamini Bunge zaidi wanafanya hivyo kwanini hasa?

Kama wewe unaliamini Bunge zaidi kuliko taasisi nyingine na hata mihimili mingine unafanya hivyo kwanini? Unafikiri Bunge litaweza kupunguza kutokea kwa ufisadi mkubwa huko mbeleni baada ya hili la escrow? hasa ikizingatiwa kuwa tumedokezwa kuna kashfa nyingine 4 kubwa zinakuja?
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
Hao wabunge wenyewe ndo wanaongoza kwa kutoa namkupokea rushwa. Subiri wakati wa kampeni ya uchaguzi ujao ndo utakavyojua kuwa pale bungeni wanapiga mayowe tu ilhali wao wenyewe ni wala na watoa rushwa wakubwa
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,250
Binafsi jicho langu la kupambana na UFISADI NDANI ya TAIFA naliweka zaidi kwenye MUHIMILI HUU BUNGE kwa kuwa BUNGE ndio MUHIMILI ambao kwa Uhalisia ni chombo chenye SAUTI ya UMMA. Rejea yanayoendelea kwenye BUNGE letu TANZANIA na kashifa mbalimbali kama EPA na ESCROW ndani ya TAIFA nafasi hiyo adhimu inawapa matumaini Watanzania kwa kuwa pamoja na kuwa Bunge ilo lina Wabunge toka chama Tawala wapatao 83% lakini ndani yake kuna Wabunge pia wa Kambi ya Upinzani wapatao 27%.

Kupitia Wabunge wa kambi ya Upinzania Taifa linapata SAUTI ya KUHAMSHA HISIA. UFAHAMU, ELIMU, NA MWAMKO wa UMMA juu ya Vita dhidi ya ufisadi ndani ya Serikali. Uwepo wa Kambi ya Upinzani ndani ya Bunge ya Wabunge wapatao 27% huku wakishrikiana na Baadhi pia ya Wabunge wa Chama Tawala wenye misimamo ya kuweka Maslahi ya Taifa mbele wamechukua nafasi za mbele kama Wapiga MBIJA [WHISTLE BLOWER] wa kuibua UFISADI nafasi ambayo kupitia kambi ya Upinzani ilianza kufanyiwa kazi na Mh Dk Slaa akiwa na LIST OF SHAME.

Ufahamu wa Watanzania juu ya kashifa za kifisadi zinapata uhalali wa kujadiliwa na kupata majibu yawe yasiostahi ama yanayostahiki lakini Umma wa Watanzania unapata Dalasa la kupima kati ya wapinga Ufisadi na Watetezi wa Itikadi ya Ufisadi nani yu Mkweli. Kupitia vikao hivyo vya majadiliano ya kibunge ni nafasi mwafaka ambayo inaibua dalasa kwa Watanzania kujua mambo mbalimbali yanayohusiana na Matumizi ya Pesa ya Umma kwenye miradi mikubwa yenye harufu ya za kifisadi.Kwa kuwa TAIFA kama TAIFA kwa jinsi ujenzi wa mifumo yetu ya CHECK AND BALANCE isivo na wigo mpana wa kumpa RAIA wa kawaida nafasi ya JUKWAA la kusemea Mawazo, Maoni, Ufahamu na malalamiko yake pale anapoona mambo hayako sawa.

Basi kupitia Wabunge wa upinzani na wale baadhi wa chama Tawala, Raia wema wenye Taarifa sahihi za kifisadi au kuhusu mambo yoyote yasio sahihi katika mihimili mingine ukiwemo pia wa Bunge, upata nafasi ya kushirikiana na wabunge hao kupata taarifa na hoja na kupeana uwezo wa kuyasema kwenye Bunge ili kuomba majibu halisi ya Tuhuma hizo za Ufisadi. Kutoka na aina hiyo ya kimahusinao ya Wabunge na raia katika sura ya Kiwakilishi ya ndani ya Wabunge wakiwakilisha umma toka ngazi hiyo ya jimbo vita dhidi ya ufisadi kupitia pembe ya Bunge imebeba sura ya kuanzia jimbo mpaka kufika Taifa.

Picha hii ya vita vya kupinga ufisadi yaweza anzishwa na ama na Mbunge wa Jimbo la Kasulu au Kahama au Nkasi kwa Mbunge huyo kuibua hoja ya UFISADI yenye sura ya KITAIFA japo Mbunge husika ni Mwakilishi tu wa Jimbo fulani.Uhalali huu ndio umeleta Mapinduzi ya BUNGE kuonekana kama ni sehemu yenye kuweza kuleta Mapinduzi ya Mapambano dhidi ya ufisadi katika Mstari ambao Ndani ya Taifa na Nje ya TAIFA watu wanapata nafasi ya kuona UHALALI KIKATIBA wa Majadiliano yenye SURA ya Demokrasia na hatua za utekelezaji kisheria zikichukua nafasi na watu na Mataifa mengine kupima matokeo ya Majadiliano hayo yameleta Majibu yenye Mshindo [IMPACT] gani katika Maendeeleo ya TAIFA na KIMATAIFA,
 
Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
6,916
2,000
Nimegundua baada ya ushabiki mkubwa ulioonekana Bungeni wakati wa sakata la escrow kuwa wapo watu kati yetu ambao wanaamini sana Bunge katika vita dhidi ya ufisadi kuliko mihimili mingine. Ninajaribu kuelewa hasa ni kwanini baadhi ya watu - kama ni wengi au la sina uhakika - wanaamini sana Bunge kiasi kwamba wako tayari kutoangalia rekodi ya Bunge vita ya ufisadi na kuacha lionekane linaoongoza vita hiyo kuliko mihimili au taasisi nyingine. Nina maoni yangu kuhusu hili lakini sijui wengine ambao wanaamini Bunge zaidi wanafanya hivyo kwanini hasa?

Kama wewe unaliamini Bunge zaidi kuliko taasisi nyingine na hata mihimili mingine unafanya hivyo kwanini? Unafikiri Bunge litaweza kupunguza kutokea kwa ufisadi mkubwa huko mbeleni baada ya hili la escrow? hasa ikizingatiwa kuwa tumedokezwa kuna kashfa nyingine 4 kubwa zinakuja?
Kwa kutunga sharia.
Muswaada wa Mnyika ulikuwa ni mswaada mzuri kuliko hata katiba ya tume ya warioba.
Kwa upande wa executieve branch, sharia ya kuhujumu uchumi ya 1982 ilikuwa bora kuliko uanzishwaji wa CAG.

Ila kwa sharia za sasa, bunge ni sawa na mbwa anayeubwakia mti.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Hao wabunge wenyewe ndo wanaongoza kwa kutoa namkupokea rushwa. Subiri wakati wa kampeni ya uchaguzi ujao ndo utakavyojua kuwa pale bungeni wanapiga mayowe tu ilhali wao wenyewe ni wala na watoa rushwa wakubwa
Unakigeuka mpaka chama chako sababu ya hili sakata, kamati za maadili si mnazo???!!
Nani kashawajibishwa kwa haya uyasemayo??!!

Watu wana imani na bunge kwa kiasi fulani sababu ya "tutakutana jimboni wakati wa uchaguzi" japo hili mbunge akiambiwa hata na mtoto hii lugha inafungua milango yao ya fahamu!!!!
Hao wengine wanawajibika kwa mamlaka ya uteuzi ndio maana labda watu wamejionea washike kilicho mkononi kuliko kutegemea ahadi na fadhila!!!
 
Okinawa

Senior Member
Nov 16, 2009
174
225
Bunge likipata uwakilishi wa Wapinzani 50+% bila shaka litasaidia sana.
Kwa upande wa mahakama ndo hao na majaji wamehongwa unategemea watatoa haki?
Kwa upande wa Executive Rais wetu hana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi.
 
Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,159
2,000
Kwa mkanganyiko ulioko kwenye mihimili ya Dola ya Tanzania ni vigumu kujua hasa ni nani alistahili kusimamia nini na kwa wigo gani, najaribu kuwaza mawaziri kuwa walinda maslahi wa chama cha siasa of which ndicho kilichowapa ulaji kisha wajinasibu kwamba ni wasimamizi wa shughuli za serikali...kwanini tusione mkanganyiko uliopo! Hiyo ni mosi pia nalitazama Bunge lisilo na meno ambalo wawakilishi wa wananchi wanatumia muda mrefu kusimamia ilani na kueleza sera za vyama kuliko mambo ya msingi walistahili kuyapeleka Bungeni kama mawakala wa Wananchi wa Majimbo walimotoka! Yatosha kusema ikiwa watendaji wa Mahakama ni wateule wa Serikali, Mawaziri ambao ni wabunge wanapewa tena ajira na serikali bila kuachia nafasi zao za ubunge basi tutegemee uwepo wa Jengo zuri Dodoma ambalo litabakia ukumbi wa kukaribishia wageni wa ''waheshimiwa wabunge''
 
Convincing!!!
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,871
2,000
Kufuatia mfumo wetu, Bunge ndio taasisi pekee yenye uwakilishi wa wananchi, hivyo Bunge ndio taasisi ya wawakilishi wa wananchi!, ukiyasoma majukumu ya Bunge, zaidi ya jukumu kuu la kutunga sheria, jukumu jingine ni kuisimamia serikali!, ni katik jukumu hili la usimamizi, ndiko imani ya wananchi ilikolalia!.

Tatizo ninaloliona tangu kwa sisi wananchi, serikali yetu, na bunge letu ni ignorance, taasisi iliyobaki yenye angalau angalau ni mahakama tuu kwa sababu it is supposed to go by the books!. Serikali ndiye mtuhumiwa mkuu, Bunge lililokuwa supposed kuisimamia serikali, ndilo bunge hili full of ignorants, badala ya kuiamuru serikali, linaishia kuitazama na kuishauri tuu, na kuipa serikali uhiyari ya kuupokea ushauri huo na kuutekeleza, au kuupokea na kuupuuzia just like tissue paper, unaitegemea sana kufutia tuu... na ukimaliza ni kuiflush pamoja na ule ...!.

Kama Bunge lingekuwa serious kumwajibisha Mkuu wa serikali bungeni!, kabla yeye hajawajibishwa, hao wahusika huko chini wangeisha achia ngazi zamani kusubiria hatua za kimahakama!.

Mkiwa na serikali lege lege, na Bunge butu, we are really doomed!.

Pasco
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,445
2,000
bunge ni sehemu ambayo kila chama kinapigania maslahi yake ya kupata umaarufu na maslahi ya wananchi yanakuja by the way lakini sio priority ya wanasiasa.Wanasiasa wanaposigana bungeni wanatafuta political scores itakayowawezesha kukamata dola. Hivi tumeshasikia wabunge wangapi wana kasha za ufisadi ikiwamo mmoja kukatisha ziara ya mbunge wa viti maalum mukya,Zambi si alituhumiwa kuomba kitu kidogo akitekeleza shughuli za bunge?sitta si amekatalia kwenye nyumba ya uspika tena aliyojenga nyumbani kwake?si ni wabunge hawa hawa wanaokaa kwenye bodi za mashirika yanayotuhumiwa kwa ufisadi? si ni wabunge hawa hawa WANAOLAZIMISHA POSHO KUBWA za vikao? kwani hawajui kwamba nchi hii ni masikini? si ni wabunge hawa hawa ambao MISHAHARA YAO HAIKATWI KODI japo wanajuia kuwa taifa linahitaji kodi kwa maendeleo ya Taifa? au ufisado ni mpaka mtu aibe ? si unaweza kuiba kwa kujiwekea sheria inayoruhusu uibe?si wabunge hawa hawa huchukua hela za safari halafu hawaendi? binafsi sina imani na mhimili huu kwa kuwa uko BIASED na uko attached na political interest kuliko mahakama ambako ni mahali pekee haki inatendeka na mdai na mdaiwa wanakutana na kuhojiana uso kwa uso kuliko bunge ambalo sasa limekuwa na tabia ya kutoa taarifa za kamati bila kuwahoji linalowatuhumu anzia kwa lowasa mpaka tibaijuka,
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Kufuatia mfumo wetu, Bunge ndio taasisi pekee yenye uwakilishi wa wananchi, hivyo Bunge ndio taasisi ya wawakilishi wa wananchi!, ukiyasoma majukumu ya Bunge, zaidi ya jukumu kuu la kutunga sheria, jukumu jingine ni kuisimamia serikali!, ni katik jukumu hili la usimamizi, ndiko imani ya wananchi ilikolalia!.

Tatizo ninaloliona tangu kwa sisi wananchi, serikali yetu, na bunge letu ni ignorance, taasisi iliyobaki yenye angalau angalau ni mahakama tuu kwa sababu it is supposed to go by the books!. Serikali ndiye mtuhumiwa mkuu, Bunge lililokuwa supposed kuisimamia serikali, ndilo bunge hili full of ignorants, badala ya kuiamuru serikali, linaishia kuitazama na kuishauri tuu, na kuipa serikali uhiyari ya kuupokea ushauri huo na kuutekeleza, au kuupokea na kuupuuzia just like tissue paper, unaitegemea sana kufutia tuu... na ukimaliza ni kuiflush pamoja na ule ...!.

Kama Bunge lingekuwa serious kumwajibisha Mkuu wa serikali bungeni!, kabla yeye hajawajibishwa, hao wahusika huko chini wangeisha achia ngazi zamani kusubiria hatua za kimahakama!.

Mkiwa na serikali lege lege, na Bunge butu, we are really doomed!.

Pasco
Pasco umekosea mahalipamoja tu,hata MAHAKAMA hatuna.Ukiona HAKIMU anaweza kupokea pesa bila hata kuogopa,halafu anakaachini ana hukumu KESI ya mtu aliyempa MSHIKO sidhani kamautapata HUKUMU stahiki,ni lazima itaangalia maslahi ya aliyempa MSHIKO.

Bunge letu hili wengi wa wabunge wetu ni MSALAHI yao kwanza,anachowaza ni lini WAZIRI ataondolewa ili yeye awe WAZIRI,unategemea huyu aisimamie SERIKALI?Kama Spika anachaguliwa na WASHIKA dau,MAFISADI unadhani kutakuwa na UHURU wa BUNGE?

In short HATUNA SERIKALI,MAHAKAMA WALA BUNGE,tupo tupo tu.

Na sina Uhakika kama jeshi lipo kwa ajili ya TAIFA au WATAWALA,maana Polisi kutwa kucha kupelekeshana na WAPINZANI kisa Chama Tawala kimeagiza.

Kwa kweli sina uhakika na Jeshi siwezi kulisemea.Hawa tunaowaita TISS hawa wako kwa maslahi ya watawala na chama,maana taasisi hiiingekuwa ya kwanza kumuweka kiti moto Singasinga wetu aka Mtoto Mpendwa wa WATAWALA.
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,843
2,000
Hapana mimi siamini mhimili wowote katika suala la kupambana na Rushwa na Ufisadi.

Kwa bahati mbaya sana Mhimili wa Executive umeoza mno kiasi cha kusababisha uozo mwingine kuonekana ni marashi. Bunge na Mahakama pia vimeoza, ila wa mwanzo ndio balaa. Na kwa hali ilivyo sasa hapana budi kwamba KATIBA MPYA (ya wananchi) ni lazima.

Tumefika mahali nchi hii lazima izaliwe upya, tuunde upya nchi yetu na tufike malengo ya kuwa na nchi/jamii yenye utawala wa sheria, haki, amani na maendeleo sawa kwa wote.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,992
2,000
Lakini wabunge huwa wanazungumza kwa ukali sana kwenge masuala ya ufisadi. Hili alo linawapa wananchi imani zaidi?
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
3,514
2,000
yeyote atakayeonekana zaidi kuwabana / kuwaongelea mafisadi basi ataaminika kutokana na historia ya mahakama either kwa kubanwa na sheria au kwa makusudi kuonekana kutokufuatilia kesi imepelekea kutokuaminika wakati bunge kutoa kwake ushauri au kupiga kelele inakuwa imeshafanya kazi yake..... In short kazi ya mahakama ni ngumu zaidi na kama unavyojua justice needs not only to be done but seen that it is done..... Linapokuja suala la ufisadi kama fisadi kwa macho ya wananchi akiwa hana hatia ki uhalisia ni vigumu kuonekana haki imetendeka mbele ya wananchi
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,250
Lakini wabunge huwa wanazungumza kwa ukali sana kwenge masuala ya ufisadi. Hili alo linawapa wananchi imani zaidi?
Nimeipenda hii kuwa Wabunge wanazungumza kwa ukali zaidi maswala ya ufisadi, hivyo linawapa imani Wananchi, ahahhhaa Mwanakijiji unamaanisha ACTIONS SPEAKS LOUDER THAN WORDS.Ndio kusema wapige kelele weheee waongee mpaka microphone zichanike hakuna lolote la maana.

Ni kweli kabisa hakutakuwa na majibu ya dhidi ya kile kinachosemwa Bungeni Kwa Ukali ila kutakuwa na mlundikano wa HASIRA ya Mkusanyiko Wa Maswali Mengi dhidi ya Kashifa nyingi za Ufisadi na Mkusanyiko huu siku ukija kupata mtumbuaji .....picha yake ushawai kuona JIPU lililoiva kwa Kupakwa unga wa Choroko Likitumbuliwa Uwa lina rusha Uchafu wake Kwa Kasi Kubwa sana.Sasa Mkusanyiko uwo wa kusema Kwa ukali huku Wananchi wanameza wakitafuta majibu ya kina polepole HATIMA yake ni MBAYA sana kwa mtu yoyote mwenye VISION si jambo la kufikilia kuishi nalo eti kuwa YOUR RUNNING THE SHOW....No its the bad idea and bad advice.
 
Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
nawaamini 50/50 kote.
mfano kwenye;
1.bunge wapo waliohusika moja kwa moja kwenye wizi huu kama akina chenge, ngelega na wengineo lakini pia wapo waliosimama kidete kupinga kama akina sendeka, Zitto, Kafulila nk.
2. kwenye serikali nako pia wakati akina muhongo, werema, maswi, anna tiba n ataasisi zingine za umma zikituibia bado kuna wengine japo wameonesha kuwa hawakufurahishwa na wizi ule kama akina wasira, mwingulu et al.
3. kwenye mahakama wakati akina mujilisi na wa watamwa wakishiriki kikamilifu tena bila aibu kutuibia lakini majuzi Jaji Mkuu Othman chande amekuja kivingine kuwa kama wamehusika basi sheria ishike mkondo wake.

kwa lugha ingine ningesema hili ni suala la kiutashi zaidi kuliko mhimili husika ndo maana nawapa 50/50. This is my view.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,992
2,000
Hivi ikitokea tena kashfa nyingine halafu wakazungumza tena kwa ukali; wakaunda kamati, wakafanya uchunguzi, wakaja na ripoti kali na mwisho maazimio ya kutekelezwa na serikali utajisikiaje?
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,403
2,000
Kufuatia mfumo wetu, Bunge ndio taasisi pekee yenye uwakilishi wa wananchi, hivyo Bunge ndio taasisi ya wawakilishi wa wananchi!, ukiyasoma majukumu ya Bunge, zaidi ya jukumu kuu la kutunga sheria, jukumu jingine ni kuisimamia serikali!, ni katik jukumu hili la usimamizi, ndiko imani ya wananchi ilikolalia!.

Tatizo ninaloliona tangu kwa sisi wananchi, serikali yetu, na bunge letu ni ignorance, taasisi iliyobaki yenye angalau angalau ni mahakama tuu kwa sababu it is supposed to go by the books!. Serikali ndiye mtuhumiwa mkuu, Bunge lililokuwa supposed kuisimamia serikali, ndilo bunge hili full of ignorants, badala ya kuiamuru serikali, linaishia kuitazama na kuishauri tuu, na kuipa serikali uhiyari ya kuupokea ushauri huo na kuutekeleza, au kuupokea na kuupuuzia just like tissue paper, unaitegemea sana kufutia tuu... na ukimaliza ni kuiflush pamoja na ule ...!.

Kama Bunge lingekuwa serious kumwajibisha Mkuu wa serikali bungeni!, kabla yeye hajawajibishwa, hao wahusika huko chini wangeisha achia ngazi zamani kusubiria hatua za kimahakama!.

Mkiwa na serikali lege lege, na Bunge butu, we are really doomed!.

Pasco
I surely agree with you Pasco, we are reall doomed.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom