Swali kwa Wenyeji wa Dodoma: Je, nikiwa na mil3 naweza kufanya biashara gani hapo na maisha yakasonga?

Davortesha

Member
Jun 19, 2021
83
119
Habari ndugu wote haswa wajasiriamali wa Dodoma mimi nimtafutaji kama walivyo watu wengine kwa sasa niko Arusha ila mambo huku hayaniendei vizuri kabisha, ila ktk kuongea na watu vijiweni wengi wamenishauri nitoke hapa nije Dodoma ila wengi wao hajaniambia nini cha kuanzanacho nikifika hapo, na mimi sitaki nije kubaharisha maisha maana na familia tayari.

Nisiwachoshe sana ila naombeni msaada wenu wa mawazo.
 
Fika kwanza mkuu, Dodoma siyo mbali,nenda kafanye tafiti kwa macho yako mwenyewe maana hapo umeshauriwa tu na marafiki.Fika eneo husika angalia fursa,uliza wenyeji waliopo hapo kisha rudi nyumbani halafu ujipange kwa uhalisia uliouona.

Huo ndo ushauri wangu kwa kuwa umesema una familia ingekuwa tofauti ningekwambia we nenda tuu itajulikana mbele kwa mbele.Fika fanya tafiti na tathmini ukiwa Dodoma.
 
Kwa mtaji wa milioni 3 dodoma kuna biashara nyingi tu emu buni unacho weza na unachopenda kufanya.
Mfano milioni tatu (3) yako hiyo: 1. Unafungua saloon nzuri ya kiume. Kwa frem ya 150,000 mitaa ya chuo mf. Mipango au UDOM.

Milioni 3 uza nguo kama boxer kiume na kike au mabegi ya spesho.

M3 uza nafaka.
Muhimu zingatia location na biashara.
 
Kwa mtaji wa milioni 3 dodoma kuna biashara nyingi tu emu buni unacho weza na unachopenda kufanya.
Mfano milioni tatu (3) yako hiyo: 1. Unafungua saloon nzuri ya kiume. Kwa frem ya 150,000 mitaa ya chuo mf. Mipango au UDOM.

Milioni 3 uza nguo kama boxer kiume na kike au mabegi ya spesho.

M3 uza nafaka.
Muhimu zingatia location na biashara.
Asante sana mkuu pia nimewaza labda mafuta ya alizeti nitoe singida nilete dodoma maana naona kama kwa sasa hayatakua na mpango wa kushuka bei
 
Fungua kujiwe Cha supu, ndizi choma na kuku wa kukaanga kwa usiku, utauza sana au biashara ya matunda, andaa tolori lifunike kwa juu nenda sehem ya njia kuu hasa iringa road, hutojuta inalipa Sana
Au waweza jichanga zaidi ukanunua bajaji asee hapa unajenga kabisa!
Au tafuta kijiwe Cha supu na kongoro hasa kwa muda wa jioni Hadi usiku inalipa Sana.
Au waweza ingia shambani maeneo ya bahi ukalima mpunga.
 
Tafuta sehemu yenye watu wengi, halafu fungua duka-genge. Utauza sana.
 
Back
Top Bottom