Swali kwa wenye uraia wa nchi tofauti na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa wenye uraia wa nchi tofauti na Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, May 28, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,094
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni niliulizwa na mtu (Mtanzania) hivi Watanzania waliohamia nchi za nje na kuchukua uraia wa nchi hizo wanazipenda kweli nchi wanazoishi kama wanavyoipenda Tanzania? Je, wanaposikia nyimbo za Taifa za nchi hizo huwa wanapata msisimko kama kama walivyokuwa wanapata walipokuwa wakisikia wimbo wa Taifa wa Tanzania? Nilimjibu swali lake kivyangu vyangu (hahahahah) lakini baada ya kulitafakari sana swali hili baadaye, nimeamua kuliweka hapa jamvini ili nisikie mawazo ya wengine walio nje ya Tanzania na pia walio ndani ya Tanzania. Karibuni sana mtoe mawazo yenu. Mimi nitarudi baadaye kuja kutoa mawazo yangu juu ya swali hili.
   
 2. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chako chako tu mzee.,diaspora ipo kwa ajili ya maslahi zaidi,lakini otherwise du,..yale yale ya kipemba changu changu lakini chako chetu tutafanyaje.
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hawaipendi nchi yao. mimi sitakuja kubadili uraia wangu hata siku moja. na uzuri wake, hakuna uwezekano wa dual citizenship ivi karibuni, hivyo watatusamehe tu, waendelee tu kuwa wageni wa Tanzania yetu, wao wabaki na izo nchi zao walizoona nzuri. asiyependa kwao ni mtumwa, mtumwa kabisa.
   
 4. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Present Africans and particlarly Tanzanians need too know more about "Pan Africanism" kutokulijua hili limepelekea Watanzania wengi wanapokwenda Marekani na Ulaya kutokuwa na uchungu na nchi zao na kujikuta wanabadilisha uraia

  Nikirudi kwenye swali lako BAK nina uhakika wakisikia nyiimbo za taifa waliloliacha mfano Tanzania lazima wanatokwa na machozi kwasababu ile hali ya usaliti inawajia na ni kweli kuwa huwa hawana morali yeyote wanaposikia nyimbo za taifa walilojilipulia mfano mtanzania aliyebadilisha uraia na kuwa mmarekani wimbo wa marekani unampa feelings gani? Kimsingi hakuna
   
 5. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,818
  Likes Received: 20,793
  Trophy Points: 280
  hivi kubadili uraia ndio kutokuwa na uchungu na nchi yako au ni kuangalia maslahi??wewe uliebaki na uraia wa tanzania una uchungu na tanzania kwa maneno tu au kwa vitendo.sina data kamili lakini naamini % ya ''WASIO NA UCHUNGU''(waliochukua uraia wa nje) ni negligible hivyo ''WENYE UCHUNGU'' na TZ ni wengi sana,je wameifanyia nini nchi??
  najibu swali lako BAK,naipenda nchi niliyopo kama ninavyoipenda tanzania coz sina sababu ya kuichukia.kuhusu wimbo wa taifa i dont care kama ambavyo nilikuwa siujali wimbo wa taifa wa tanzania(no disrepect but i just dont care)......mara ya mwisho niliimba nikiwa shule ya msingi na kuusikia alipofariki Baba wa Taifa.
   
 6. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  HIVI NI KWELI UNAIPENDA TANZANIA KIASI HICHO? SIDHANI TENA ACHA UONGO KABISA.NCHI NI KITU CHA KUFIKIRIKA WEWE.MUNGU ALIUMBA DUNIA NA KUSEMA NENDENI MKAZAANE NA KUIJAZA DUNIA.HAKUSEMA NCHI.BINADAMU TUMEKUJA NA THEORY ZETU ZA MIPAKA YA NCHI,MIKOA,HALMASHAURI, MPAKA KATA ILI KUIFANYA THEORY YA NCHI IENDE.

  • NYUMBANI MISHAHARA HAITOSHI,LAKINI WATU WANAMILIKI MAPRADO UNATAKA KUSEMA NI MSHAHARA AU BIASHARA KAZINI ? KAMA SIO WIZI ?NA RUSHWA
  • NINA FAMILIA KUBWA INAYONITEGEMEA,MIMI NDIYE NILIYEBAHATIKA KUPATA ELIMU,MSHAHARA WENYEWE WA BONGO UNAUJUA,LAKINI NJE KUNALIPA ZAIDI, nikitumia mshahara huo WATOTO WA NDUGU ZANGU WATAENDELEA KUSOMA NA KUWEZA KUJIKOMBOA KIMAISHA ,SASA UNATEGEMEA NIBAKI BONGO TU?
  • JE UNAJUA KUWA SERIKALI YA INDIA HUPATA % NGAPI YA PATO LAKE KUPITIA WATU WALIO NJE?
  • HIVI UNAJUA UMUHIMU WA WATU WALIO NJE NA MAENDELEO YA NCHI ? KAMA NI WASALITI,SERIKALI ILIKUWA NA HAJA GANI YA KUITISHA MKUTANO WA DIASPORA?
  • SERIKALI ILIKUWA NA HAJA GANI YA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WALIO KWENYE DIASPORA?JE NI KWELI UNAWAONA WASALITI AU ..mhhh
  • UNAJUA KUWA KILA HELA TUNAZOLETWA NYUMBANI ZINALIPIWA KODI,NAKUZUNGUKA,.UJENZI,MASHULENI,MAHOSPITALI,WAKULIMA N.K
  • concl.BASI WALIO NJE NDIO WAKWELI NA NDIO WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO.,NA MAMBO YAO NI HALALI NDIO MAANA SERIKALI IMEWATHAMINI.,WEWE KALAGHA BAHO,..NAIPENDA NCHI YANGU SIO WOTE NI WEZI BABU,NA WENGINE HATUPENDI MAISHA YA WASIWASI NA YA KUBAHATISHA.
  • mwl J.K alisema kila mtu ana haki ya kwenda atakapo, na kuishi atakapo provided havunji sheria za nchi..sasa maoni ya usaliti umeyatoa wapi?kama sio wivu?
  • dual citizenship ni maamuzi ya serikali na bunge, kama imeweza kuona umuhimu wa watu wanao ishi nje na kuangalia jinsi gani itaweza kunufaika nao ,sidhani kama swala lako litakuwa gumu kupatiwa ufumbuzi.,MAISHA NI MASLAHI NA SIO SIFA
   
Loading...