Swali kwa Waziri Mkuu: Je Tanzania imejiandaje na cyber security? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa Waziri Mkuu: Je Tanzania imejiandaje na cyber security?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Aug 5, 2011.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tanzania imekuwa ikitangaza kuwa inajiandaa kujiunga na mkongo wa kimataifa wa fiber optic. Mkongo unategemewa kusaidia kukua kwa mtandao wa mawasiliano na internet. Pia tumekuwa tunataarifiwa ujaji wa e-government mtandao utakaorahisisha huduma mbali mbali za serikali. Pamoja na maendeleo hayo pia tumekuwa tukishuhudia cyber attack zinazotokea katika benki mbali mbali nchini. Matukio ya CRDB, Barclays na NBC ambapo cyber attack imekuwa ikichangia kupotea kwa mabilioni ya shillingi kutoka kwenye benki husika.

  US national security cyber office wanasema kila nchi iliyoendelea inashambuliwa na cyber attacks zisizopungua 1000 kwa siku. Isitoshe, baada ya mtikisiko wa benki na uchumi wa dunia makampuni mengi duniani yanapunguza gharama za uendeshaji kwa kutumia mtandao kuendesha shughuli zao uzalishaji. Benki kama HSBC, Barclays, Chase, Bank of New York Mellon, au Apple, Microsoft, na kadhalika wanahamia zaidi kwenye mtandao wa internet kupunguza gharama za uendeshaji.

  Hali kadhalika, makampuni ya uzalishaji umeme, nguvu ya nyuklia, telecommunication na airport zimekuwa zinahamia zaidi katika mtaala wa mtandao kurahisisha mawasiliano na uharaka wa mawasiliano. Vile vile machine mpya zinazojengwa na zimekuwa more of internet based zaidi kuliko hardware based. Kutokana na hizo sababu maendeleo yanapokuja huja vile vile na hatari mbali mbali zinatokana na watu mbali mbali wenye nia isiyo nzuri na nchi yetu.

  Mfano project ya e-government au vitambulisho vya uraia zitarahisisha usambazaji wa taarifa, upelekaji wa taarifa mbali mbali mikoani, uwazi na maendeleo. Hata hivyo wasiokuwa na nia nzuri na nchi yetu project hizi pia ni sehemu nzuri ya kupata taarifa ambazo ni siri ya taifa (national security). Taarifa za tarehe za kuzaliwa watu, kiasi gani wanachopata kwa mwaka, kodi wanayolipa, maradhi ya mtu, ukoo, ulinzi wa nchi na usalama wa nchi, hazina ina kiwango gani cha fedha nakadhalika. Taarifa hizi zikipokewa na maadui wa nchi yetu zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi.

  Vile vile mitandao ya airport, bandari, reli , umeme ni nyaraka za serikali na kutokana mashine nyingi kuunganishwa na internet inaweza kuhatarisha usalama wa nchi. Mwaka 2010, Iran a virus kwa jina la stuxnet ilishambulia kinu cha kuzalisha nyuklia nchini Iran na kusababisha nuclear rods kuoverheat na hasara iliyowarudisha nyuma Iran for six months(CNBC, Code Wars 2011). Mwaka 2007 serikali ya Estonia ilifungwa kabisa na kusababisha hasara ya mabilioni, walifunga ofisi ya rais, serikali kuu, jeshi na sekta ya benki kusababisha wananchi wakwame kwa muda ya siku zaidi ya moja. Hilo lilisababisha wasiwasi kwa wananchi na matokeo wananchi wakaanza kukosa imani na serikali yao.

  Pamoja maendeleo tunayoyatamani pia tunaomba kuuliza je serikali imejiandaaje na usalama wa mtandao? Vile vile serikali je inachokitengo cha usalama wa mtandao kwa ajili ya mabenki, wizara, umeme, reli na kadhalika? Pia wamejiandaje na usalama wa mtandao wa mawasiliano nchini kwani ukuaji wa sekta ya mawasiliano uendane na ukuaji wa usalama wa watu na mali zao?
   
 2. HT

  HT JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  we waache tu, Tz naona watu waja mbiombio. Mpaka waweke mkong e-govt lazima tutakuwa na script kiddies wa kutosha. Halafu IT wenyewe wa kuungaunga kama hizi web zetu za taifa...bah!
   
 3. c

  calmdowndear JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  website ya taifa is a joke

  ikulu wanatumia yahoo kutuma e-mails zao na website yao ni blogspot

  in fact we have nothing to fear on this end
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  PM atakuuliza "cyber maana yake nini?"

  utacheka hadi ufe.
   
 5. F

  FredKavishe Verified User

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kaka nice idea tusubiri kama kina nape watamfikishia maana nchì hii ni sarakasi tu
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Unajua tatizo la umeme nchini linatokana na mipangilio isiyokuwa na umakini na kusababisha kukua kwa mahitaji ya umeme wakati vyanzo vya umeme na uzalishaji umeme ukiendelea kubakia pale pale. Matokeo yake ni kuwa mahitaji ya umeme yamekuwa makubwa kuliko umeme uliopo. Tatizo hilo hilo linaanza kujitokeza sasa katika ulimwengu wa mtandao nchini, tunajitahidi kuenda na wakati ila kama hakuna mtaala wa cyber security then we vulnerable to cyber threats. Taarifa kama za benki, wizara zinaweza kunyonywa na mtu akiwa Iceland na kuuzwa online. Taarifa za usalama wa nchi pia zinaweza kunyonywa na mtu yeyote duniani. Estonia ni funzo zuri sana kwetu sote.

  Nasio online hata offline mfano mtu anaweza kuingiza kirusi katika sekta ya benki chini na kusababisha kasheshe nchi nzima. Isitoshe, vitu kama radar ya nchi au mawasiliano ya simu yanaweza kuwa vulnerable to hooligans na kusababisha maafa ya ajali za ndege mmungu atuepushie mbali ila ndio ukweli halisi.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh, mkuu wangu unachekesha sana. Nchi yetu yenyewe inaendeshwa Kimafia na tunapona kwa rehema za Mungu...leo unauliza jinsi serikali ilivyo jiandaa na Cyber attacks hali malaria tu imetushinda!...Ukoma umerudi na TB ndio gonjwa namba tatu kwa kuua watu...Mkuu usifanye utani hata kidogo ikiwa unajua kwa uhakika hakuna serikali yetu haina servers isipokuwa tunategemea mashirika nchi za nje.. Hivyo hatuna sababu ya kujiandaa kwani kinga zote za cyber attack zinawekwa na host wetu, sisi kama waaarabu tunakunja miguu na kubofya..
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Duh!
  Mkuu that is even worse!! ikiwa kama data zetu tunategemea servers kutoka mashirika nje ya nchi, je tuna uhakika gani na usalama wa taarifa za nchi kumilikiwa nchi nyengine. Imagine taarifa za kiwango cha madini yaliyopo nchini, afya za watu, kodi , benki zetu zikimilikiwa nje ya nchi si hatari hiyo!!!! Dah!
   
 9. HT

  HT JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  government ICT-wise is a joke. Angalia TBC, National Web et al. A big joke
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Uwezo wa taifa kujilinda kwenye nyanja zote kwa sasa uko chini sana. Cyber attack its much complicated kwa awamu ya Jk kutambua na kutilia maanani kwani ni kwenye kipindi hiki usalama wa taifa umepwaya hadi kutia aibu. Vikosi vyote vya ulinzi polisi, jwtz, magereza etc ndio wamelala fofo nchi inachezewa kama shamba la Bibi... Leo uwahoji kuhusu mashambulizi ya kimtandao? Iam telling they hav no Idea of what you r talking about!
   
 11. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu umekwenda mbali sana. Sisi huko wala hatujakaribia. Cyber security ni nini? Kama fedha zilichotwa BOT kama vile mtu anasafirisha mazao kutoka shambani na hakuna aliyeweza kuzuia hilo, tutaweza kuzuia cyber attacks?
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Gurtu,

  Walioiba BOT wameiba Billioni 133 kwa kipindi cha miaka 5 kirusi kama Zeus kinaweza kuiba pesa kutoka account ya nchi au mtu binafsi kwa muda in less than a second pesa zote zikawa zimeisha irrespective of the amount. Kirusi hichi kikishachota hela kutoka automated transactions kinaweza kutengeneza account millioni (ghost accounts) vile vile wakati kinaiba hela mnaweza msigundue kitu gani kinaendelea labda kama tunacho kitengo cha usalama wa taifa kinachoangalia mitandao hii. Isitoshe inaweza kujizalisha in a matter of a second na hivyo kuwa ngumu kukizuia. Pata picha BOT wawe attack na Zeus kama hatuna security system iliyo na maana tunaweza kujikuta tumeamka asubuhi nchi haina hela. Isitoshe hela zilizoibiwa zinaweza kwenda mahali tusijue kabisa.

  Kuna kirusi kinaitwa stuxnet chenye uwezo wa kujilinda chenyewe na artificial intelligence (yaani akili yake yenyewe usually a programmed intelligence kuattack a certain facility). Mfano adui akiwa na nia mbaya kuleta maafa kinaweza kupandikizwa kirusi hiki na kwenda katika sekta ya nishati na kuvuruga mitambo yote ya umeme as long kuna local network. Tunaweza kujikuta tunaanza tena upya.
   
 13. i

  iMind JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Tumejiandaa kikamilifu, tayari ikulu wameshafungua barua pepe mawasiliano@yahoo.com. hili ndo jibu lake
   
 14. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  <br />
  <br />
  FYI Tanzania hatuna chochote ambacho kinaweza kuharibiwa na cyber attack, serikalini penyewe wanatumia internet mainly kwa ajili ya mail na mabank wanasumbuliwa na fraud na sio hacking
   
 15. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Zeus mfano huattack any computer that uses Microsoft Windows software, Windows Vista na Software zinazotumia windows. Je Tanzania serikalini mnatumia software gani? Pia ufahamu kirusi kinaweza kubebwa hata na usb pen na kikaja kuchomekwa katika machine moja wapo katika ofisi za serikali as long kuna local area network sio lazima kiwe online. Fraud na hacking ni ndugu moja majina tofauti. Mwaka 2010 mfano hackers waliweza kuiba almost $70 million kwa kutumia Zeus pekee. Hizi sio hela ndogo na hawa watu ni majizi tu kama wale wanaotumia fraud nyenginezo.
   
 16. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  watakuambia wanatoa Cyber tort(computer Law )
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  La msingi waanzishe kitengo cha usalama wa taifa kitakachokuwa kinashughulikia cyber threats na ni vema kisijulikane kinafanya kazi wapi ili hackers wasianze kukishambulia huko kilipo. Kazi yake kinakuwa kama back up in case of cyber threat. Benki kama CRDB, NBC na Barclays have experienced a first hand cyber attacks na zimekuwa zikisababisha mabilioni ya shillingi kupotea. Pesa hizi zisingelipotea kama kungelikuwa na idara ya usalama wa taifa inayoshughulika na cyber threats as a firewall behind our digital systems in the country. Tukiwa kazi yetu ni siasa na kupiga kelele hatufiki mbali na watu binafsi kama mie na wewe tutakuwa katika hatari kwasababu vijisenti vyetu katika account zinahatari ya kuibiwa na benki zije kukataa kutulipa, vile vile taarifa kama majina, tarehe za kuzaliwa, afya na rasilimali unazomiliki zinaweza kuwa zinapatikana na bwelele na kuuzwa kwa watu wenye kufanyia kazi. Isitoshe, cyber attacks are dangerous kwa wenye kuiba identity za watu unaweza kukuta akina mdondoaji wako 10 na wanataarifa zinazofanana.

  Sawa serikali ilale ila usalama wetu pia upo hatarini kama hakuna hatua madhubuti za kujitayarisha na cyber threats.
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Sina la kuongeza. Kama mechanical attacks zinakushinda hakuna uwezekano wa kukabiliana na cyber attacks. Nakumbuka Maxene Melo aliwahi kukamatwa kwa cyber terrorism, kumbe jamaa ni blogger tu. NI sawa na kumkamata mhasibu wa kijiji kwa kuiba shilingi lakini mbili na kushindwa kumkamata aliyeiba trilioni benki kuu.
   
 19. c

  calmdowndear JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2016
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Usanii tuuu
   
Loading...