Swali kwa wazazi na walezi: The Diaper Dilemma

Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
18,146
34,190
Habari za asubuhi JF, Natumai mu wazima na familia zenu hazijambo.

Niende straight to the point kuhusu mada yangu. Kiukweli motherhood sometimes inakuwaga mtihani kwangu. Lol. Na kwa hili namshukuru Mungu uwepo wa dada zangu kina gfsonwin Kaunga, The secretary na wengine katika kuniongoza na kunishauri.

Leo hii mada yangu inahusu diapers ama pampers kama tulivyozowea kuziita. Nilipojifungua mtoto wangu wa kwanza nia yangu ilikuwa kutumia washable diapers ama cloth diapers. Lakini zilinishinda kuzifungq mpaka I gave up na kuanza kutumia disposable diapers.

Kiukweli sikujua when or how to stop mpaka baby alipozikataa mwenyewe at two years

This little munchkin at seven months hates diapers. Yaani nikimvua ana bonge la smile. Kumvisha atalia huyooo. Niseme tu kuwa I change diapers immediately they are wet or soiled.

Sasa napenda nimuachishe mapema.

Mpendwa mzazi/ mlezi ,How do I do it? When do I do it?

I Thank You In Advance
 
Anza potty training taratibu akizoea unaachana na diapers. Lakini jaribu kuchange diaper brand maybe he/she is just not comfortable with the one you are using now.
 
Naunga mkono maoni ya Wadau hapo Juu jaribu kubadilisha brand labda itasaidia,jaribu Huggies Diapers ni nzuri sana,pia jaribu kuangalia unavyofunga labda unakaza sana kiasi kwamba inakuwa imembana sana na kuleta discomfort kwake.

Miezi saba inafaa unaweza anza potty training hasa kwenye kupata haja kubwa naamini mpaka hapo ushajua wakati gani zaidi anapata haja kubwa. Kama upo nyumbani tu siku moja moja siyo mbaya unampa ahueni kwa kumvisha pantii tu ingawaje ndo utapata dhahama ya kufua kila wakati.
 
Kwanza kabisa mbadilishie aina ya pampers unazotumia sasa hivi. Binafsi sijawahi kutumia Molfix kwahiyo sijui ziko soft kiasi gani ila Sleepy sio soft kivile hivyo inawezekana zinamfanya unconfortable, ni vile tu hawezi kusema. Nunua Pampers hata ile pack ndogo kabisa yenye 8pcs ujaribu kumvalisha kwa siku mbili tatu uone itakuwaje. Kama akiendelea ku-react the same way utajua kwamba hapendi kabisa diapers.

#2 Kwa siku mbili hivi jaribu kusoma ratiba yake ya kupoop, yani hata kama haupo nyumbani mwambie dada wa kazi amwangalie akuambie anajisaidia mida gani. That way utaweza kujua muda gani umuweke kwenye potty.

#3 Mtafutie potty zuuuuuuri, kama yale ya magari magari hivi uanze kumkalisha kama mchezo tu bila kumvua nguo ili asiogope, azoee na mostly afurahie. Akishaanza kukaa bila utata time ile mida yake ya kupoop umkalishe bila nguo for as long as possible. Unaweza kucheza nae na kuongea kumu-encourage akiwa amekaa ili ajisikie huru maana watoto wengine huwa wanaweza kujizuia kwakua wanakuwa na hofu kwakuwa ni kitu kipya na sivyo alivyozoea. Usiogope kusafisha poop off the floor for some time kama unataka kufaulu kwenye hili. Baada ya muda atajifunza/atazoea kwamba kupoop ni kwenye potty na mtafundishana hata namna ya yeye kuonyesha akitaka kupoop. Hapo sasa diaper mtavaa usiku tu, pakukucha anavua na havai tena mpaka muda wa kulala.

GOOD LUCK!!!
 
Potty training is a life saver....Kwa anayeshinda naye nyumbani au kama ni wewe mwenyewe, mvalishe nguo bila diaper, ila safari za kwenda potty ndio ziwe habari ya nyumbani. Sio kumsubiri, nyie ndio mumpeleke mara kwa mara...Diaper atumie zaidi akilala.

Zinakera nazo jamani...though you can also consider the size, tunaambiwa hii ya kilo 3 na mtoto kilo 3, lakini unamuona kabisa mtoto anabanwa..

Kuna diapers nyingine, zile locks zake zinakata, hivyo unakuta mtoto ana mikwaruzo...labda nayo sababu...(kagua sleepy coz molfix hazikati, lock yake ni laini)
 
jaribu diaper za brand nyingine.....pia kuangalia anakaa nayo kwa muda gani wakati mwingine inamkera kwa joto.


kuna potty zinakuwa na kitufe cha music ya watoto hiyo itasaidia kuanza kuzoea kutumia kidogo kidogo
 
Karucee

Hi Karucee! Pole kwa malezi.
Mada yako ya leo imebobea mno kwenye umama, kwa hiyo I
am technically elliminated for contribution.Sorry for that and byebye!
 
Last edited by a moderator:
wasiwasi wangu itachakachuliwa muda si mrefu

ʞʍelı ɯʞnn' ʞnuɐ ʌıɾɐuɐ ɥnɯn ɾɟ ʍɐuɐʇɐqıɐ zɐ ʞnʌnɹngɐ sɐuɐ ɯɐpɐ ʞɐɯɐ ɥızı
 
Naunga mkono maoni ya Wadau hapo Juu jaribu kubadilisha brand labda itasaidia,jaribu Huggies Diapers ni nzuri sana,pia jaribu kuangalia unavyofunga labda unakaza sana kiasi kwamba inakuwa imembana sana na kuleta discomfort kwake. Miezi saba inafaa unaweza anza potty training hasa kwenye kupata haja kubwa naamini mpaka hapo ushajua wakati gani zaidi anapata haja kubwa. Kama upo nyumbani tu siku moja moja siyo mbaya unampa ahueni kwa kumvisha pantii tu ingawaje ndo utapata dhahama ya kufua kila wakati.

Mke mwenza upo deep!
 
Back
Top Bottom