Swali kwa wataalamu wa upimaji ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa wataalamu wa upimaji ardhi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jatropha, Jul 22, 2009.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Eneo letu lina mchoro wa kina uitwao TP Drawing No 1195 iliyopitishwa tarhe 19 Oktoba 1996, na ambao umekuwa ikitumika kupima viwanja eneo hili. Hivi karibuni wamejitokeza watu kutoka Wizara ya ardhi wanandai hawaitambui TP Drawing hiyo na wanapima viwanja juu ya viwanja vingine vyenye offer na hata hati miliki kwa madai eti huu ni mradi.

  Nauliza kutoka kwa watu wenye taaluma ya mambo haya, Je hii ni sawa? Nini maana ya mchoro kupitishwa ikiwa baadhi ya watu au taasisi zitadai haziutambui? Je ni hatua zipi wananchi tunaweza kuchukua/
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Jatropha;528879
  Hao watu wa kwanza waliopima kabla ya hawa wapya, ni watu wa Idara gani na walitoka wapi?
   
 3. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu huo mchoro wa awali ulisainiwa na nani? Kisheria hamna upimaji unaoweza kufanyika juu ya upimaji mwingine, hii inawezekana tu iwapo upimaji na TP ya kwanza ilikuwa nullified, ilitenguliwa, na hii ni lazima ifanyike kisheria na kimaandishi. Hebu muwabane hao wapimaji wanaokuja sasa hivi wawaeleze kwa kina. Hati ya ardhi inaweza kutenguliwa Tanzania ila ni Rais ndio mwenye mamlaka hayo kama katengua wawaambie pia. Ila ndugu yangu mambo ya mjini nayo ni makubwa, usishangae kusikia hiyo TP ya kwanza ilikuwa ya 'vishoka' tu pale wizarani!
   
 4. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  hilo eneo liko wapi? au ni kwembe?

  kuna kesi kama hizo zimetokea ila wananchi walienda pale wizarani kuwaona wakubwa (mpaka katibu mkuu) wakiwa na hizo documents. haiwezekani kulipima upya eneo lenye mipaka (beacons) na watu wana hati miliki.
  miaka hii kuna ufisadi kila kona msilale!
   
 5. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,042
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Mkuu wa Wilaya kafikia wapi mkuu ama naye kaungana nao?
   
 6. Surveyor JA

  Surveyor JA Member

  #6
  Jun 10, 2016
  Joined: Jun 4, 2016
  Messages: 62
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  1465571884250.jpg
   
Loading...