Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,447
Nitaanza kwa utani tu. Katika nchi mmoja ya Ulaya watu wameruhusiwa kutembea na bangi lakini kwa matumizi ya binafsi (personal use). Hivyo kuna jamaa akahamua ku-import container nzima la bangi. Alipokamatwa na polisi, jamaa akajitetea kuwa ni kwa personal use, ingawaje ilikuwa ni ya biashara. Akaachiwa huru na sheria ikabidi ibadilishe hili kuonyesha kiwango gani mtu anaruhusiwa kubeba kwa personal use. Kwa mtaji huu kitu kisichoandikwa kisheria sio kosa.
Nikirudi kwenye mada: Najaribu kuisoma katiba ya serikali ya Tanzania na sioni sehemu inayosema kuwa ni lazima mgombeaji wa cheo cha kisiasa awe mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa. Hivyo basi kwa mtaji huu, mtanzania anaweza kuwa mwanachama wa vyama vingi vya kisiasa na kugombea nafasi moja au nyingi kwa kutumia tiketi ya vyama vingi.
Kwa maoni yangu uanachama wa chama cha siasa is not mutually exclusive. 2015 ninaweza kugombea udiwani kwa kutumia uachama wa CUF na wakati huo huo kugombea ubunge kwa kupitia TLP na CHADEMA au CCM. Sheria ya nchi haikatazi mtu kushikilia udiwani na ubunge kwa wakati mmoja.
Naomba ufafanuzi wenu