Masikio yameumbiwa kusikia, moyo kutafakari na kuamua, akili kung'amua na kutambua lipi baya na lipi zuri, nafsi ndiyo wewe na mimi, ila Roho ndiyo uhai sasa, vinne hivi vipo ndani yetu, yaani kwenye miili yetu na ndiyo mimi na wewe sasa.
Wanawake wa leo ujuaji umewaponza sana na mbeleni mwao ni giza totoro,wengi wao hawalijui hili isipokuwa wachache walio rehemewa, huku wakisahau ya kuwa kila jambo lina chanzo na historia imeaandika.
Nikawa najiuliza hivi, hili kweli wanawake wa leo ambao wamewezeshwa hawalioni ? Mbona wanayo yadai ni madogo sana kuliko matokeo ya kile wanachokidai ? Leo mwanamke amefanywa kama bidhaa, lakini wao muda huo huo wakijinadi ya kuwa wamewezeshwa na wametolewa gizani, na huku wakijinadi ya kuwa zama zimebadilika ? Sasa mbona wao ndiyo wako gizani zaidi kuliko zama zote ? Hivi leo hii hakuna upuuzi wowote unaofanyika isipokuwa mwanamke amewekwa kama chambo, mwanamke amekuwa mtu wa kuvutia bisashara,wanawake wa kileo heshima kwao si lolote. Mwanamke gani aliwahi kutoka na kulikemea hili na kuzilinda heshima zao na thamani zao ? Wao wamefundishwa ya kuwa adui yako namba moja duniani ni Mwanaume na lazima ushindane nae, na uhakikishe unamshinda (Huwa nacheka sana).
Nikaja kuhitimisha ya kuwa Wanawake wa leo yule aliyewatoa majumbani aliwaficha lengo la kwanini aliwatoa majumbani na kuwaleta mtaani kwa jina zuri la "HAKI" ila ukweli ni kuwadhalilisha. Lakini alifanikiwa sana kwa kondoo kumvisha sanamu la Ng'ombe na kisha wenyewe wakaambiana yule ni Ng'ombe na siyo kondoo, huoni pua ile, huoni pembe zile ? Yaani akawa anaona mambo mazuri mazuri tu,kuwa na mahela, kumiliki mali na mfano wake.
Nina mengi ya kuandika, ila nakumbuka maneno mazuri yaliyotoka kwenye kinywa Twahara yasemayo "Bora ya maneno ni maneno machache na yenye faida".
Nahitimisha kwa nukuu maridhawa ya Will Durant, mwanafalsafa anayejulikana vyema, na mwandishi wa kitabu kiitwacho ‘History of Civilization’ anasema, “Tukijaalia kuwa tunaishi katika mwaka wa 2000 A.D na tunataka kujua tukio lililokuwa muhimu kabisa katika robo ya kwanza ya karne ya 20, tutaona kuwa haikuwa vita ya kwanza ya Dunia wala Mapinduzi ya Urusi. Lilikuwa ni badiliko la nafasi ya mwanamke. Historia haikuwahi kushuhudia badiliko la kusisimua kiasi hicho ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Nyumbani, ambapo ndio ulikuwa msingi wa kiuendeshaji wetu wa kijamii, mfumo wa unyumba (ndoa), ambao ulizuia ufisadi na zinaa na kuleta utengamano wa maisha ya familia, na sheria madhubuti ya maadili iliyotusaidia kuondoka katika ushenzi kwenda katika utamaduni na tabia inayokubalika ya kijamii, yote haya yalisukumiziwa mbali na badiliko hili la kimapinduzi.”
Angalizo
1. Wanawake wa humu wana rauka sana kama wametoka usingizini, ombi langu mkija katika huu uzi mje na hoja za kielimu na sisi kutuonyesha uanamke wenu na kutia kwenu huruma. Bali mje na hoja za kielimu na mtuambie ilikuwaje mpaka mkatolewa majumbini na kuingia mtaani.
2. Siyo lazima tufikie muafaka sababu muafaka si lengo katika mijadala ya kielimu, bali lengo ni kuuweka wazi ukweli, bila kuangalia nani atachukia wala nani atalaumu.
3. Lazima tuheshimiane na tusivunjiane heshima. Hapa ni hoja kwa hoja.
4. Wanawake mkiulizwa maswali mjibu siyo mnakimbia.
5. Nachukua fursa hii kuwaita wanawake wote humu, huku nikiwaambia ya kuwa "Huu uzi ni wenu, karibuni mjimwaye mwaye" ila mje na hoja kama nyinyi ni wa kweli. Kwa uchache naomba ni waite kadhaa : Rowin cariha Paula Paul SIERA
Ni mimi kijana mtiifu Zurri