Swali kwa wanaume hasa walio kwenye ndoa...

cheupe sr

Senior Member
Aug 18, 2012
102
34
Habari zenu wana JF,
Nimekua mara nyingi najiuliza bila kupata majibu , na leo nimeona nirudi jamvini pengine nipate mawazo tofauti kutoka kwa wadau. Hivi ni kwanini wanaume kwa asilimia kubwa walio kwenye ndoa huongea kwa ukali/hawana lugha za kimahaba wanavyoongea na wake zao kwenye simu?

Hili jambo huwa linanisikitisha sana, yaani mwanamke hata ujitaidi vipi lakini mwenzio mkavuu kama kauzu..

Labda niwakumbushe tu ndugu zangu wanaume, mapenzi ni kwa pande zote mbili huwa mara nyingi mnajisahau mnafikiri ni nyie peke yenu ndo mnastaili kupendwa na kupewa mahaba 24-7, but unasahau nawe unajukumu la kumpenda mkeo na si tu kumpenda bila matendo hayo yanakua si mapenzi bali ni maigizo..

Nashangaa sana, unataka mkeo akapate wapi mapenzi zaidi ya kwako?? Na ndio hapo mimi ninasema mara zote,wanaume ndio hasa chanzo cha wanawake kutoka nje ya ndoa na hasa ukikuta mwanamke si mvumilivu..

Sawa maisha yanaenda yanabadilika kuanzia mlivyokua girlfriend na boyfriend mpaka sasa labda mnafamilia ya watoto kadhaa, ila mapenzi lazima yaendelee.

Ninafahamu familia kama mbili hivi ambazo tangu nakua mpaka sasa wale wazee wana wajukuu, lakini ukimsikia yule baba anavyo msemesha yule mama ambaye anaweza akafika miaka kama 65 hivi, kwa kweli utawa admire sana, ni wanaume wachache sana wenye karama hizo.
Nadhani pia mmesahau kuwa mapenzi yanajengwa na vikitu vidogo vidogo, sio mpaka umnunulie mkeo mercedece benz ndo atajua unampenda NO NO NO, kauli tu na matendo hicho ndicho haswa tunachokihitaji wanawake ili nasi tujisikie burudani..

Karibuni wadau nanyi mtoe michango yenu..
 
Allaaaah..we kakwambia nani???oooh..sorry nilijua namuandikia Mamaa Yoyoo...
 
Hapa naomba kwanza ujiulize maswali yafuatayo:-
1. Je? Baada ya kupata mtoto mapenzi bado yako kwa baba au kwa mtoto.
2. Hali ya Uchumi bado ipo vilevile?
 
Hapa naomba kwanza ujiulize maswali yafuatayo:-
1. Je? Baada ya kupata mtoto mapenzi bado yako kwa baba au kwa mtoto.
2. Hali ya Uchumi bado ipo vilevile?

Sasa kwa taarifa tu wanasema wakina mama mapenzi yanahamia kwa watoto kutoka kwa baba, ila mimi kwangu ni vise versa, yaani baba amehamishia mapenzi kwa watoto kutoka kwangu.
Hali ya uchumi ianzidi kuboreka siku hadi siku.. kwa hiyo nadhani hiyo siyo sababu.
Kikubwa mi ninacho kiona ni kujisahau au kujiamini sana kuwa unapendwa sasa ukadhani mwenzi wako labda yeye hastaili hayo mapenzi ambayo wewe unapewa..
 
Mimi nakabliana na wewe! Mimi baba yangu Nunda sanaaa! Sio Maza tu ndo anapewa kubwa, hadi watoto nao tumo, hadi mtu mzima bibi (R.I.P) nae alikuwa anaipatapata fresh!!!!!!

Siku akija akawaongelesha kiukarimu hapo ujue yupo kwenye Shutuma nzitooo, tena zenye grounds kali za conviction kwa mkewe! Mnajua tu hapo mtu yupo in BLACKFEMALE/ Blackmail!!!!!!!

The good part akimuongelesha maza anampa kubwa KILUGHA so hatuelewi ila tone tu unajua ya kifaza house!!!!!!!!!!
 
Aisee...this is very true. Mara nyingi ukisikia tone ya sauti ya mbaba inageuka kuwa ngumu, unajua wife huyo! Hata majibu yenyewe ya mkato mkato tu.....

Kina baba msibishe, haya yanawahusu sana tu, anza leo kuwasikiliza wenzako majibu yao (halahala usibambwe)
 
Yaa nakwambia hata hapa ofisini tuko na wakaka kadhaa wenye ndoa zao nakwambia akipokea simu ya mkewe utajua, na akiwa anazungumza either na kimada au nyumba ndogo utajua, yaani mimi huwa ninasikitishwa sana na hicho kitendo...
 
Aisee...this is very true. Mara nyingi ukisikia tone ya sauti ya mbaba inageuka kuwa ngumu, unajua wife huyo! Hata majibu yenyewe ya mkato mkato tu.....

Kina baba msibishe, haya yanawahusu sana tu, anza leo kuwasikiliza wenzako majibu yao (halahala usibambwe)
Dina umenikumbusha ile kabla hajakipata na kukitia ndani mwanaume hujihisi kuwa bado hajapata power ya kukumiliki na kukutreat apendavyo so anajiforce kuwa sie; but once akikupata na kukuweka ndani ndio mambo ya mazoea na kukuona kero. But the same mbaba anaemgombeza mkewe simuni msikilize akiwa anaongea na binti mwingine ambaye hayuko himayani mwake au nyumba ndogo.................mpooooole kama maji mtungini.

Ila wapo wale ambao wanawaheshimu wake zao aisee (Unakumbuka lile tangazo sijui lilikuwa ni la kitu gani jamaa anapigiwa na wife anawaamuru marafiki zake wamute mpira kwenye TV) afu anamdanganya wifey kuwa yuko ofcn hahah)
 
Hiyo huwa ni tabia ya wanaume wengi, yani hawako romantic kabisaaa! Basi ukutane na mwanaume wa aina hiyo, mkali 24 hrs, alafu akirudi nyumbani anaanza kelele kwenye masuala ya chakula mara oooh, hii ,mboga mbona haijakolea nazi, mara chumvi kidogo sana, mara ,mbona jikoni hamjafagia, khaaaa aisee wanaume wa aina hii mnabore sana.
 
Dina umenikumbusha ile kabla hajakipata na kukitia ndani mwanaume hujihisi kuwa bado hajapata power ya kukumiliki na kukutreat apendavyo so anajiforce kuwa sie; but once akikupata na kukuweka ndani ndio mambo ya mazoea na kukuona kero. But the same mbaba anaemgombeza mkewe simuni msikilize akiwa anaongea na binti mwingine ambaye hayuko himayani mwake au nyumba ndogo.................mpooooole kama maji mtungini.

Ila wapo wale ambao wanawaheshimu wake zao aisee (Unakumbuka lile tangazo sijui lilikuwa ni la kitu gani jamaa anapigiwa na wife anawaamuru marafiki zake wamute mpira kwenye TV) afu anamdanganya wifey kuwa yuko ofcn hahah)
Exactly, hata ukiona anavyoongea na wafanyakazi wenzake, so polite......Lakini huyo aliyeko himayani kwake, khaaa!
 
serious,wa baba mbadirike...yaan baba akirudi watoto wote km walikua sebuleni wanakimbilia vyumbani mwao!
Wakati ndo muda wa kukaa na wanao!
Na kinachoniboa wengine utaona wanamgombeza hadi mama mbele ya watoto!lol

Mi ndo ctaki kabisa mwanaume wa kunigombeza
 
Ni wanaume wachache sana wana appreciate kwa jambo lolote unalowatendea mimi nikimtendea mume wangu jambo lolote hushukuru .
 
Men are selfish my dear. Ukimuona anavyocheka na wanawake wote ofisini na hata wakimuagiza maji ya kunywa anawaletea, akirudi home anavuta mdomo kama kalambishwa sumu. Usijikoseshe raha, cheka with all men for the day's share, ukirudi home na wewe unapumzika mdomo na mapafu ya kuchekea. Manake unahangaika nimemuudhi nini kipenzi kumbe mwenzio anachat na wa ofisini na kesho wanaenda kumalizia stori. Sio kama anatembea nao, ila basi tu! Raha jipe mwenyewe bibie.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom