Swali kwa wanasiasa wa Tanzania: mnalifahamu jibu la 'no comment' kwa maswali ya wanahabari?

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
Salaam,

Katika siasa za Tanzania za kipindi hiki cha 'revolutionised media' ni nadra sana kusikia mwanasiasa wa kitanzania akitoa jibu la 'no comment' pale anapoulizwa maswali na waandishi wa habari.

Katika duru za siasa, si sahihi kwa mwanasiasa kuwa na majibu kwa kila swali aulizwalo. Kuna maswali mengine yasiyohitaji haraka wala papara katika kuyajibu. Kutoa majibu katika maswali ya aina hiyo, ni rahisi sana kwa mwanasiasa kujikanganya na kutoa majibu yatakayomweka pabaya yeye na chama chake. Pia majibu hayo yanaweza kuwa siyo sahihi katika kipindi husika cha duru za kisiasa.

Wanasiasa wa mataifa yaliyoendelea, upenda sana kutoa jibu la 'no comment' pale wanapoona hawana maelezo ya kina na uhakika kwa maswali waulizwayo. Pia uzingatia duru za kisiasa za kipindi wanapoulizwa maswali hayo; kwa kuwa uogopa kuharibu sifa yake na ya chama chake ama itikadi/aidiolojia yake.

Ni wakati muafaka kwa wanasiasa wa kitanzania kujifunza na kuwa na mipaka katika majibu mnayotoa kwa waandishi wa habari. Jibu la 'no comment' laweza kukutunzia staha na heshima mbele ya jamii.

Wasalaam
 
Salaam,

Katika siasa za Tanzania za kipindi hiki cha 'revolutionised media' ni nadra sana kusikia mwanasiasa wa kitanzania akitoa jibu la 'no comment' pale anapoulizwa maswali na waandishi wa habari.

Katika duru za siasa, si sahihi kwa mwanasiasa kuwa na majibu kwa kila swali aulizwalo. Kuna maswali mengine yasiyohitaji haraka wala papala katika kuyajibu. Kutoa majibu katika maswali ya aina hiyo, ni rahisi sana kwa mwanasiasa kujikanganya na kutoa majibu yatakayomweka pabaya yeye na chama chake. Pia majibu hayo yanaweza kuwa siyo sahihi katika kipindi husika cha duru za kisiasa.

Wanasiasa wa mataifa yaliyoendelea, upenda sana kutoa jibu la 'no comment' pale wanapoona hawana maelezo ya kina na uhakika kwa maswali waulizwayo. Pia uzingatia duru za kisiasa za kipindi wanapoulizwa maswali hayo; kwa kuwa uogopa kuharibu sifa yake na ya chama chake ama itikadi/aidiolojia yake.

Ni wakati muafaka kwa wanasiasa wa kitanzania kujifunza na kuwa na mipaka katika majibu mnayotoa kwa waandishi wa habari. Jibu la 'no comment' laweza kukutunzia staha na heshima mbele ya jamii.

Wasalaam
Makonda aje kusoma hapa, ulishatowa ushauri mzuri kadhaa nyuma, lakini mijitu mpaka leo hii haielewi kabisa.
 
Nakumbuka ni mzee Lowassa tu ambaye ameshawahi kulitumia hili neno alipokuwa akihojiwa na BBC kabla ya uchaguzi mkuu 2015
 
Back
Top Bottom