Swali kwa wanajamii

Anord92

New Member
Sep 11, 2014
3
0
Je? Adhabu ya kifo inayotumika na mahakama iendelee au ifutwe?
Kwa nini iendelee...na kwa nini unafikiri isiendelee kuwepo....

Ahsanteni.
0cd53500454676afd7fb64684c9c23a4.jpg
 
Adhabu.. ya kifo...!!
ng'ooooo... yani niache ugali na samaki...
haiwezekani
 
adhabu ya kifo haifai.
1. ni kinyume na utu na hadhi ya mwanadamu
2. ukimuua mtu umemfundisha nini? au unamkomoa?
3. kuua ni dhambi
 
Adhabu ya kifo iendelee tu mkuu! Nasema iendelee maana kuna binadamu wengine kwenye kufanya ualifu ni zaidi ya shetani ambao kiukweli ukisema aende jela maisha bado haisaidii. Mfano majambazi wavamia kwako nakukuta wewe na familia yako na mama mkwe,let say una binti zako wawili wa darasa la saba na mwingine kidato cha kwanza.... Katika kuvamiwa unaamrishwa utoe pesa kwakuhofia usalama wa familia yako... haijakaa sawa wanawabaka watoto,mke,pamoja na mama mkwe na wewe pia usjitoe na ufedhuli huo unafanywa mbele ya familia yako. Kama haitoshi wanafanya mauaji mbele yako.... then hao watu wanakamatwa na vyombo vya dola! Em niambie watu hao magereza tu ndo itakuwa suluhisho???
 
Mkuu inapotokea umehukumiwa na mahakama sio dhambi! Maana mahakama inafahamika hata huko mbinguni....
 
Kwa ufahamu wangu Mdogo,punishment inayotolewa Kwa kuenenda kinyume na Sheria Mbali na kuonya (deter),kumrejeshea mtu Hali yake ya awali (Reform/compensate/redress),pia ni kwa lengo la ku-equalize what has been lost (Retribute).
Ndo maana Atakayeua nae pia ahukumiwe na mamlaka husika adhabu ya kifo.
 
adhabu ya kifo haifai.
1. ni kinyume na utu na hadhi ya mwanadamu
2. ukimuua mtu umemfundisha nini? au unamkomoa?
3. kuua ni dhambi
Kama anayehukumiwa adhabu hiyo na yeye aliuwa unaiwekaje..?? Yajibu hayo maswali yako kwa kumfikiria aliyeuwawa na mhukumiwa...
 
Kama anayehukumiwa adhabu hiyo na yeye aliuwa unaiwekaje..?? Yajibu hayo maswali yako kwa kumfikiria aliyeuwawa na mhukumiwa...
afungwe maisha kwani akiwa gerezani si tishio tena. kumbuka wengine wanaua kwa sababu ya wivu wa mapenzi n.k.kumbe yawezekana ni hasira au kuchanganyikiwa. lakini hata mtu auwe vipi yeye asiuwawe. hatuwezi kupambana na uovu kwa kutumia uovu. point kubwa ni kwa Mungu hapendi.
 
Hapo umeitazama haki ya aliueuwa tu.. aliyeuwawa humfikirii kwa chochote... unamtazama kama amefanyiwa alichostahili...

Kumtunza huyo huyo aliyeuwa nibishu nyingine...
 
Back
Top Bottom