MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,006
- 2,166
Vyama vyote vya siasa ukianza na CCM, sehemu kubwa ya mazungumzo yao siyo ya kweli, not really. Vyama vya upinzani ni rahisi kulinda maneno yao kwa kusema ni wakweli, lakini kwa CCM hawawezi maana wameshaonyesha kwa vitendo wakiwa madarakani kwamba ni waongo. CCM ni waongo.
UKAWA haiwezi kusambaratika kwa kuwa lengo siyo kuwa m/kiti wa chama chochote kile! Habari hizi kama ni za kweli zitakuwa na lengo la kuwakomoa CCM ambacho ndicho UKAWA wanachokitafuta. Anaweza kupewa nafasi ya kugombea Urais na ikapita kwa sababu sioni kama urais ni dili yoyote kwa UKAWA. Sheria iliyopo inampa ushindi aliyetangazwa, siyo aliyeshinda. CCM kwa tabia zao za siku zote, watalazimisha yoyote atangazwe.
Kwa Lowasa sioni faida kwake zaidi ya kuwakomoa CCM kwa maamuzi yaliyofanywa. Inagwa lengo lake kwa nguvu ilikuwa ni urais, siamini kwamba ana imani kwamba akiwa UKAWA anaweza kuwa rais.
Nchi ni ngumu, haifuati sheria. Sasa hivi mawaziri wote wanatumia magari ya serikali na madereva wa serikali kutafuta kura majimboni, kinyume na sheria. wanachokifanya ni kuweka namba za bandia.