Swali kwa WAMAMA wenye watoto: Hivi kwa nini huwa mnafanya hivi???

Tuwie Radhi
Tukubaliane kuwa wengi wa mama hao huaga victim wa matokeo mbalimbali yaliyo fanyika awali na matendo yasiyo na Uadilifu juu ya jamii haswa ya uswahilini. ukweli unategemea mama alee watoto asimamie nyumba nk. Wakati aliyekusanya zogo la watoto hajulikani na hayupo kusimamia majukumu yake. MNATEGEMEA nini ? MSONGO wa mama huishia kwa watoto, majirani na hadi kituoni polisi , mahakani mwishoe gerezani. iwe yeye au watoto wataishia pabaya na hayo ndiyo mnaona hivi sasa VIBAKA wamezidi, Makahaba kibao, majambazi usitaje, wazururaji tele nk. yaani maadili ya kijamii yamezikwa na jamii. Tumerudi porini kuishi kama wanyama wa mbugani kila anayeweza kumrarua mwenzie anarauwa tu. God bless Afrika.
 
Jamaani:
Mujue huyo mama nae alikuwa mtoto hapo zamani, sasa alivyotukana nae alitukanwa kabla huko kwao..... Usisahau wengi ni
mlolongo wa watu waliyo kimbia familiya zao na kutowatendea haki stahiki vizazi vyao. Hapo unategemwe nini. yaani kumtukana mwanae ni jambo dogo... Wandugu huko uraiani kuna mambo/balaa makubwa kuliko matusi !! Je tukiyamwaga humu sijui
mtatokea wapi?
 
kulelea mtoto uswahilini ni kazi sana. Maana hata wewe mzazi ukijitahidi kulea ktk maadili, bado atasikia matusi kutoka kwa majirani. yaani hamna privacy kabisa full muingiliano
 
Heheheh...akizoea sana nyama si ndio kama haya ya kutaka kudokoa chunguni..

hamu inaisha ya nyama hatadokoa. ila bana mtaani kwetu wakati nakua kulikuwa na mama ambaye mpaka leo yupo ndani ya ndoa yake na mumewe....akiita mtoto wake akiitika naama, basi mama anamalizia na tusi ....halafu embu njoo huko!!!
sasa sijui ni nini hapo watu8
 
Last edited by a moderator:
hasira kwa waume zao wanazimalizia kwa watoto

Hili pia linawezekana...maana maisha ya huyo mama ni ya kushinda nyumbani tu na mumewe hata sijui anafanya kazi gani
 
Mh! kwel iyo tabia ipo namshukuru mungu cwezagi kumuita mtt wangu hata mjinga ww nahic atakua ivo..nna jiran yangu uyo mh! mtt akienda kucheza haitwi kwa jina lake utackia we mbwa njoo na mtt akickia tu sauti ya mama anaitika nakuja...mpaka mschana wakaz naye ameiga anatukana wtt ivo ivo..
 
hapo mama kakulia matusini kwa hiyo mtoto ataogelea matusi...mwanae kama wa kiume mkewe atakoma kwa matusi kama wa kike wanae wajiandae kulishwa matusi.....

Uswazi kwetu ni kawaida.....

Mama anamuita mwanae mbwa sasa kama mtoto mbwa sijui mama ni farasi....


In short malezi mabaya

pia uswazini kwetu matusi ni kawaida yaani ni lugha halali kabisaaaaaaaaaaaaaaa.

Kipindi nipo chuo nakumbuka tulipita na wenzangu mitaa fulani ya manzese(enzi hizo ilikuwa uswazini haswa) watoto walikuwa wakicheza mpira bahati mbaya au nzuri wakaupiga ukafika tulipokuwepo kiroho safi tukauokota na kumpelekea dogo mmoja alikuwa almost 5-6 shukrani yake aliporomosha mbonge wa mtusi tukashikwa butwaa...
 
Back
Top Bottom