Swali kwa Rais Dr.Magufuli:Ni lini waliokula mishahara hewa watafikishwa Mahakamani?

Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa, rejea swali hapo juu. Mi sina uwezo wa kukuona nikuulize swali hili. Ila nakuamini sana ktk utendaji wako. Wengi wamefikishwa mahakamani kwa ufisadi ila hawa waliokula mishahara hewa ya watu takriban elfu 19 kwa muda mrefu ni lini utaanza kuwakamata na kuwashtaki na ikiwezekana warudishe fedha hizi za umma?
Magufuli huwa anaongea na wanaccm na si watanzania wote,ndo maana unapata shida kuuliza uliza maswali,ile Kiki haikukusu wewe bali wanaccm
 
Tanzania bhana na wakikamatwa kuna watu watalalamika kwamba nchi haina demokrasia.
Huyo mtu atakuwa mjinga kama wewe atakayepinga kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa watu wote walioiba fedha za umma!
 
Magufuli huwa anaongea na wanaccm na si watanzania wote,ndo maana unapata shida kuuliza uliza maswali,ile Kiki haikukusu wewe bali wanaccm
Kwanini nikiuliza kwa mwamvuli wa uzalendo, shida ipo wapi?
 
Kwanini nikiuliza kwa mwamvuli wa uzalendo, shida ipo wapi?
Mkuu mie sikulaumu kwa kuuliza kwako bali naamini hukuwa mlengwa wa ile hotuba,lakini pia naomba ujue wazalendo wa awamu hii,hatuulizi maswali ya namna hii,sisi tunasifu tu na kuabudu
 
Soma.vizuri kanuni na sheria za utumishi wa umma. Kuna siku watakuja kulipwa pesa nyingi sana wale. Mtumishi wa umma hafukuzwi kama unavyofukuza malaya baada ya kumaliza shida zako.mlikurupuka mtajuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kila mtu anaeiunga mkono serikali juu ya jambo fulani ni CCM mimi sio mtumwa wa chama chochote cha kisiasa bali serikali inapofanya vema naiunga mkono na inapofanya utopolo nakosoa.
 
Back
Top Bottom