Swali kwa mheshimiwa Zitto !!!!

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,715
92
Za saa hivi mheshimiwa !

Pole sana kwa kazi, na hongera kwa kulitumikia taifa letu.
Mimi binafsi nina maswali machache ambayo ningependa uyaclear wewe binafsi na sio kama chama. Tokea kifo cha mama Mbatia (Mungu amrehemu) kumetokea, maneno meeeengi sana ya kisiasa hasa tena hapa yakiongozwa na wafuasi wa Chadema tawi la JamboForums. Sasa mheshimiwa, wewe kama Zitto (sahau siasa kwa dakika moja) unachukuliaje hili suala zima la watu kuhusisha kifo cha mama Mbatia na siasa, wengi wakisema kwamba wewe zitto ulitaka kuuliwa. Kwa kweli hata kama tunataka maendeleo ndani ya vyama vyetu, nafahamu fika kwamba kuna dirty taactics ambazo hutumiwa, lakini hii ni MBAYA SANA TENA SANA kwa taifa letu.

Naamini wengi watasema mie chizi kwa kuwa napingana nao, lakini vile vile naamini chizi huyo huyo katika maneno kumi atakayoongea basi angalau hata moja linaweza likawa na maana. Mheshimiwa tukumbuke kwamba maendeleo ya nchi yetu, mapenzi ya nchi yetu, na maendeleo ya kisiasa ni mambo ya kidunia tu hivyo jiangalie wewe mwenyewe katika kutetea ule ukweli unaoufahamu na kupinga yale yasiyo ya kweli ( Kama na hili pia litakuwemo ndani).

Kwa kweli, Zitto sitokuficha umefika katika hatua nzuri sana, na katika hatua hiyo sidhani kama wengi walio wapinzani wako, na hata wale walio karibu yako watapenda ufanikiwe zaidi yao, KUMBUKA NIMESEMA WALE WAPINZANI WAKO NA HATA WALE ULIO NAO KARIBU hivyo jiangalie sana na watu wanaosema wako karibu na wewe maana watu hao hao (hapa JF) washasema ulitaka kuuliwa (huku wakiwa hawana proove ukiangalia hawakuwa katika eneo la tukio )

Sasa najua unaweza ukawa busy, hivyo ukachukua muda mrefu kujibu lakini natumaini hata kama itachukua muda mwingi angalau upitie hapa na udondoshe walau maneno machache !

Shukrani !
KadaMpinzani for JF !
 
huu sasa utoto; kama unataka kupata mawazo ya Zitto kuhusu yanayosemwa jamboforums na unataka ayajibu yeye "kama binafsi na siyo chama", nenda kwenye tovuti ya Chadema kuna email yake na namba yake ya simu au nenda kwenye tovuti ya Bunge upate namba yake umpigie na kumuuliza. Akikujibu njoo utuambie (kama tunataka kujua).

Inaonekana wewe huwezi kuanzisha hoja isipokuwa kutumia wengine. Kuna mahali popote ambapo umeona Zitto kadai kuwa ni yeye alikusudiwa katika ajali hiyo? sasa yeye atacontrol vipi ndege kuruka juu ya kichwa chake?

umeshindwa kumnyonga mwanakijiji sasa wamtaka Zitto,

hii aibu kakangu, acha hizo!
 
Inappropriate, I Will Be So Suprised Kama Zitto Atarespond Hapa. Kada Kaka Watu Wakipanga Kukuua Hutajua Sasa Sijui Unataka Zitto Aseme Nini, Weather Kulikua Na Mpango Huo Au Hakukuwepo Yeye Hatojua Lolote Na Hata Kama Amekuja Gundua Chochote Usitegemee Kwamba Atakisema Humu.
 
Nimejitolea kufanya kazi ambayo wewe ungeifanya. Zitto amesema hiyo ni ajali kama ajali nyingine yoyote ile. Kuelewa chanzo cha ajali ni kupatikana kwa huyo dereva na kutasaidia kuelewa mazingira ya ajali nzima. Sasa hivi yuko kwenye kampeni za Udiwani. Unaweza ukitaka kumpigia simu namba yake iko kwenye tovuti ya Bunge.
 
Mkjj,
Kama hivyo ndivyo sasa kwanini rafiq lako mwafrika wa kike ana andika mambo ya ajabu juu ya kifo cha marehemu? Ni tabia mbaya sana, kwani in away ni uchochezi......asidhanni kwamba yuko mbali, anadili na watu wenye long arms and memories!!!.
 
sasa Zitto huo ni mtazamo wake, na yeye mwenyewe pia hana la kusema kwa wale wanaofikiria vinginevyo. Sasa mnataka Zitto aje na kusema "mwafrika wa kike" asifikirie hivi au vile? Uwezo wa kumuamulia mtu kufikiri aliupata wapi?

Hivi unafikiri kweli ni mwafrika wa kike peke yake anayefikiri kuwa kuna kitu kwenye ajali hii? Nenda Dar leo usikie minong'ono na ushahidi " wa kitu" unavyoelezewa. Hilo siyo kosa la wale waliofika eneo la ajali.
 
kazi yake mola..haina makosa..anafanya atakalo anafanya awezalo kwani Dunia ni yake na hakuna.....
 
Mkjj,
Kama hivyo ndivyo sasa kwanini rafiq lako mwafrika wa kike ana andika mambo ya ajabu juu ya kifo cha marehemu? Ni tabia mbaya sana, kwani in away ni uchochezi......asidhanni kwamba yuko mbali, anadili na watu wenye long arms and memories!!!.


mhh naona nilishaanza kutishiwa hapa.

hakuna chochote mtakachonifanya nahizo long arms zenu!
I have lived long enough to know my way in and out!
usinitishe hapa maana siogopi vitisho!
ameshindwa mama yangu kunitisha wewe utaweza?
 
KADA....

unawaona hao CHADEMA?mhhhh suala umelielekeza kwa mheshimiwa ZITTO na lipo straight forward wanakuja kujibu wao,basi bado wanaambizana na wengine watakuja kumjibia.........kazi kweli kweli watu hawa.
 
Ujinga ni kutumia hoja ya vitisha, all of you who are trying to threaten others are doomed to failure. Tanzania haitajengwa kwa hoja za vitisho, whether long arm, lolipop or whatever, humu zitawale hoja tu.
 
KADA....

unawaona hao CHADEMA?mhhhh suala umelielekeza kwa mheshimiwa ZITTO na lipo straight forward wanakuja kujibu wao,basi bado wanaambizana na wengine watakuja kumjibia.........kazi kweli kweli watu hawa.

engineer, swali halikuelekezwa kwa Zitto, kwani kama angetaka kufanya hivyo kuna njia za kutafuta jibu bila kuweka hadharani. Aliliweka swali hilo ili wengine na sisi tulisome na kulitolea maoni. Kwa vile hawezi kutafuta namba ya Zitto au kujaribu kumPM ili apate mawazo yake ndiyo nimeona nimsaidie maana hawezi kuchinja, amezoea vya kuchinjiwa!!
 
KADA....

unawaona hao CHADEMA?mhhhh suala umelielekeza kwa mheshimiwa ZITTO na lipo straight forward wanakuja kujibu wao,basi bado wanaambizana na wengine watakuja kumjibia.........kazi kweli kweli watu hawa.

bana mkuu wee acha tu ! wataona kitu soon kizuri !
 
kadambonakiswahili chako kimepindapinda?? mwanzoni nilidhania typing error lakini nimekuja kugundua unazungumza kiswahili chenye baadhi ya lafudhi ya kihindi. Isijeikawa ulishawahi kufanya kazi office moja na RA au labda weye ndiwe.....

ni comments na doubts zangu tu hizo
 
nashukuru mkuu nilifungua inbox nikajua utatuma baadae

Lakini KadaMpinzania ajibu comments zangu hapa kwa faida yangu na wengine
 
MKjj....

unajua mie naheshimu sana maoni na mawazo ya kila mtu,lkn hapo naona KADA hana makosa na ndio maana ameuliza kwa nia safi tu lkn safi sana kumjibia mheshimiwa zitto kwani umetwambia he is na kampeni huko alipo.

KADA.....

hawa watu kama wangepewa ufunguo wa KUGAWA RIZKI hapa duniani sijui ingekuwaje ..............eeeeeee leo wamepewa ufunguo wa MODERATORS tu hapa JF hatuna raha,mhhhhhhhhhh lkn tupo TUATABANANA HAPA HAPA.
 
Huu ni utoto na kutokuwa na hoja. Kwangu mimi huu ni umbea wa mitaani. Kafa Amina, mengi yakazungumzwa. Jamani hebu kwenu na imani na mnako abudu
 
Eng. Moh'd : kwa majibu yako, naona title ya Mhandi(th)i lingekufaa zaidi ya hilo la Engineer!!! (with a light touch)
 
Watanzania wengi wana chicken vision, mambo mengi tunayaangalia kwa upeo mfupi sana, nakubaliana na BWM watanzania ni wavivu wa kufikiri!
Ushahidi kwamba zitto alikuwa target, ni pale tu hata zitto mwenyewe leo asingekuwa hai au ni mahututi hospital! sasa kuanza kutafuta contents za kilichotokea baada ya tukio ni sawa na kufanya postmorterm! it doesnt help anything or reverse the case!!

Mazingira ya tukio yanaashiria zitto alilengwa, si lazima apatikane dereva aseme ukweli ulivyo,hadi leo kifo cha moringe inasemwa ni ajali tu, lakini pengine ilikuwa planned!

Kila mtu ana uhuru wa kutoa tafsiri ya matukio vile anavyoona, ni bora kuwa doubtful and you take care kuliko kuwa confident and finally you loose!
 
Back
Top Bottom