Swali kwa Mheshimiwa Membe kuhusiana na Sakata la Gesi Mtwara

Masikini wala huna taarifa kwamba kiwanda kinajengwa Lindi na uzalishaji utaanza ndani ya miezi 9. Kubonyeza keyboard ni rahisi kuliko kufikiria hiko unachotaka kuandika...!!

Nchi ya ajabu sana hii. Wanalia fedha zile kutochukuliwa na wahindi wenye uraia wa nchi mbili na ambao wangekwenda kuzificha India na Canada, badala ya kujenga kiwanda kitakachoinua uchumi wa nchi wa kuzalisha ajira, kuchangia kodi na kuchochea biashara! Sasa kiwanda kimeanza kujengwa wamebaki midomo wazi na sasa wamerukia kwenye tawi lingine. Kuna watu wameshika kila nafasi kubwa hapa nchini na sasa wanataka kuishi magogoni lakini zaidi ya kujinufaisha binafsi na familia zao, hakuna lolote la kijivunia kwa wananchi wao. MEMBE UNAOGOPWA MZEE, ENDELEA KUwATIA HOMA JAPO NAJUA HUJAOTESHWA
 
Mkuu hoja yangu iko wazi sana. Kwanza mimi siomwana CCM kwa taarifa yako hivyo hakuna kundi lolote linalowakilishwa.

Mkuu ukienda chuo vyuo vikuu vyote nchini ili uwe Rais wa serikali za wanafunzi lazima uonyeshe unao uwezo wa kushawishi, kujenga hoja na kutetea maslahi ya unaowangoza. na historia ndio inayotumika yaani ulitetea nini au nani wapi n.k wenye historia nzuri wengi wamekuwa Rais ama viongozi wa juu na wameendelea kuwa viongozi bora hata baada ya kutoka chuo mifano unayo mingi sana.

Ukienda nchi za wenzetu wanatangaza nia mapema sana kuanzia miaka miwili kabla ya uchaguzi lengo ni kusema nipo clean, ninao uwezo na nimefanya issue moja mbili tatu nimefanikiwa na uwezo wa kuwa commander in Chief ninao anzia kwa Obama fuatilia records zake na ndio zilizompatia credit.

Tuje suala la Mtwara, kungekuwa ni Bomba la maji limepasuka wanaCCM wote including Membe wangekua Mtwara leo
hii wakiwapa pole na kutoa tamko haraka haraka bomba lijenge wananchi wasife kwa kukosa maji. Naamini membe angetoa hata magari yake kuwasaidia wananchi lakini kwa sababu wanannchi wanataka haki yao si Membe wala Kinana
wana Nape wameenda Mtwara wote wamekaa kimya.

Hata wanamtwara wanapodai haki yao hawakujua watapigwa mabumu na risasi hadi kufa, walijua serikali ya CCM ni sikivu na viongozi wake ni sikivu including membe (designated President) atawasikiliza na kuwatatulia kilio chao.

Swali: Kikwete alijisifu sana kuumaliza mgogoro wa Maziwa makuu akiwa kama waziri wa mambo ya nje (kwa wakati ule kweli ilikua issue) na tukaona kweli anaweza kwa kiasi fualni.

Kwa sasa hot issue ni Mtwara ambako ndiko unatoka wewe tuonyeshe diplomacia yako, uwezo binafsi na watu waliokuzunguka kuonyesha kweli wewe ni mtu mwenye uwezo na unastahili kukabidhiwa nchi 2015.


hivi mara ngapi tumesikia migogoro kule mererani na hivi karibuni kule ngorongoro na bado haijapata ufumbuzi. Mbona hakuna aliyedai Lowassa, 'kipenzi cha watanzania na mzee wa maamuzi magumu' aende kule akasuluhishe? Haupendi urais. Kwa kukaa kimya sifa yake ya urais imetoweka? Kweli hawa ndo wale Comrade Saanane anawaita wala mishikaki ya mwaka mpya Monduli! Nothing between their ears.
 
Mawaiba, nachelea kusema kwamba wewe si mkazi wa Mtwara. Yaani hata ujui Membe ni mbunge wa jimbo gani na wala gas inayosababisha vurugu inatoka wapi. Sasa kama hujui haya utatuaminisha vipi hayo ya Membe kuwekeza?

Membe hana kitega uchumi Mtwara, ni wapinzani wake tu wamekuwa wakihusisha vitega uchumi vya Shebi matelephone na ukaribu wake Membe na Shebi. Mzee wa mamvi alituma watu wake Mtwara kwenda kujaribu kumuhusisha Membe na hoteli ya Shebi mix na kuambulia patupu. Kama kuwekeza Membe angewekeza kwao Lindi kuliko gundulika gas nyingi mara tatu ya gas ya Mtwara. Tatizo la watanzania ni kuzani kila mwanasiasa ni mfanyabiasha wa aina ya mamvi na tujisent.

Kutaka Membe atoe tamko juu ya gas kwenye wizara ambayo hausiki na mkoa ambao hausiki ni jaribio jingine la kundi la mamvi kutafuta wimbo wa kutokea. Membe ndiye aliyeufanya moto wa gas usiingie Lindi baada ya kuongea na viongozi 300 wa Mkoa wa Lindi.

Na sisi JF wakati mwingine tunasikitisha; jana umeletwa uzi wa Membe kuchochea vurugu Mtwara leo tunamtaka aje atoe tamko.

Ni kweli unachonena, imefikia mahali ambapo watu wanakurupuka kutaka kumpaka matope mtu bila sababu ya msingi. Kuna hoja za msingi kuhusu Membe ni vyema zikawekwa wazi ili wananchi wazijadili baadala ya hizi za kuokoteza tu. Membe kwao ni mkoa wa Lindi si Mtwara.
 
kiongozi mzuri utamjua wakati wa matatizo ataonyesha leadership skills zake, membe is quite means he is afraid of taking a stand he is not a leader.
 
Back
Top Bottom