Swali kwa mh.waziri mkuu kupitia mh. Ole medee (mb) arumeru magharibu

kaka, Vincent Augustino,

Ole Medee huyo Naibu Wizara ya Ardhi!!! amulize nani maswali sasa? na ardhi wameshapeana vigogo?

Tuko jimboni na huu utata umetokea kwenye jimbo lake, kama hatalifanyia kazi 2015 si mbali na walioliwa 10,000 ni watu wa kawaida na zinawauma kweli kweli. Ajabu walingojea Waarusha wapige kura kesho yake wakabandika orodha
 
Mh. Ole Medee wengi wa wapiga kura wako hawatakuelewa kama hutamuuliza waziri katika kipindi cha maswali ya hapo kwa hapo swali lifuatalo.

Mh. Waziri Mkuu, mwaka huu Halmashauri ya Arusha vijijini imekuwa ikifanya jitahada za kuwapatia wananchi viwanja vilivyopimwa na tayari viwanja vimetolewa katika maeneo ya Gomba Estates na Burka, naipongeza serikali kwa jitihada hizo; swali

1. Hivyo viwanja ni kwa ajili ya Watanzania wote au ni kwa ajili ya kundi dogo lenye uwezo wa kifedha kwani bei za kiwanja inaanzia TShs. 4,000,000 hadi 32,000,000 pesa ambayo hata mfanyakazi wa serikali hawezi kumudu.

2. Pale ambapo waombaji ni wengi kuliko viwanja vilivyopo (mfano Burka) ni utaratibu gani unatumika ili kutoa haki/nafasi kwa kila mwombaji pasipo kubagua? Na Jee wote waliolipia viwanja wametumia majina yao halisi?

Akiuliza swali kama hilo (1) ajiandae kula 'ban' 2015 kupitia kura za maoni.
 
Akiuliza swali kama hilo (1) ajiandae kula 'ban' 2015 kupitia kura za maoni.

Ni bahati mbaya kwa kuwa Naibu Waziri tena wa Ardhi hawezi tena kuuliza swali kwani yuko upande wa Serikali. Hata hivyo akicheza vizuri karata yake na hilo tatizo litamjenga kisiasa na alilifumbia macho litambomoa kisiasa.
 
Back
Top Bottom