Swali kwa kina dada, Tunavumilia ili iweje?

Dah!! :doh::doh: Haya mambo banaa ona sasa hadi nimekosa hamu ya kula:hungry::hungry: usiku huu inatubidi:hail::hail: na:pray2::pray2: sana ili yasije kukuta halafu mtu ukaanza:fencing::fencing:kama sio :A S-cry::A S-cry: na:faint::faint:na :A S-confused1::A S-confused1:halafu una :rip::rip::rip: sababu ya :A S-heart-2::A S-heart-2:
 
Nimekua nikijiuliza sana kuhusu mahusiano.

1. Dada ana mpenzi wana miaka,sio mume wala mwanaume hana mpango wa kuoa,
wanafanya kazi mikoa tofauti, ajabu mwanaume anampa mwanamke masharti ya kufika kwa mwanaume.
Dada akienda lazima atoe taarifa kabla na hata ukitoa taarifa sio kwamba lazima atakuruhusu, anaweza kusema usije nina wageni wa ofisini. Dada akienda wageni hakuna na ananuniwa
inabidi aondoke tu. Akirudi kwake mwanaume ndio analeta mapenzi na dada anapata amani kua alimkosea laaziz,hivi huyu mwanamke hapa huwa anang'ang'ania nini?
Kama hamjaoana hakujali, ndani ya ndoa si itakua balaa?

2. wapenzi wqanaishi mikoa tofauti, mwanaume aakienda mkoa anaoishi mpenziwe hamjulishi, dada anaambiwa na wanaomjua huyu kaka kuwa tumemuona,kaka akiulizwa anajibu nipo ila nina mambo mengi nitakutafuta. Kaka anamaliza kilichomleta hadi anaondaoka bila kumtafuta mpenzi wake,bibie akipiga simu kumuulizia kaka anajibu nimeondoka ilikua ghafla!!
Dada anaandaa safari kwenda kwa kijana na zawadi kafungasha, wakiwa kwa mwanaume mapenzi kunoga lakini kaka akienda mkoa anaoishi mdada anajificha.
Mdada anavumilia eti kweli kazi nyingi,jamani kweli au ndio mapenzi upofu?

3. Utakuta dada ana mpenzi ambaye siyo mume, siyo mchumba wala siyo baba mtoto.
Mwanaume ana visa na mbaya zaidi ni mpigaji hadi dada tunakupeleka hospitali lakini ukipona umerudi na style ya maisha ni ile ile kupigana.
Hivi hapa kinachomfanya dada huyu kuvumilia mateso na aibu hii ni nini? Na anavumilia ili aolewe au ndio kupenda?

Kama kweli mapenzi Upofu mbona visa tunavyotendwa tunaviona, TUNALALAMIKA,tunalia tunafuta machozi halafu bado tunajipa moyo, Hivi huwa nini kinatufanya tuendelee kuvumilia?

Endelea kuvumilia na usichoke utapata thawabu mbinguni, tena mbinguni unajilimbikizia mema usichokoze banaa
 
Huyo dada ni mjinga (samahani kama ni nimetumia lugha nzito. Hivi anahitaji mtu kumwambia kuwa huyo jamaa anamtumia tu, tena kama taili la spea?

watu wengine bwana (awe KE au ME) nadhani wana matatizo ya akili....

Nimemchukia sana huyu binti...Kwani asipokuwa na mwanamume ndo atakuwa ame..R.I.P??

Nimechoka mwenzeni na hawa watoto... Mzee DC!!
Ni watu wazima ila wanataka kujifanya watoto
 
Kwa mtazamo wangu;
Wa kwanza - Attitude yake huyo dada ya kumridhisha mwanaume wake ndo inamfanya adharauliwe na kuchezewa na huyo kaka - hajaonesha her stand juu ya jinsi anavyokua treated vibaya... We are what we are and we, we can not be what we are not. Na huo dada anakua hivyo kumridhisha mwanaume kua ampende kumbe anaharibu, it beta arudi her normal self. Huyo mwanaume yuko comfy akiwa kwa the girl coz yuko huru. Hawi huru akiwa kwake sababu obviously ana mwanamke who is most important na maybe kapanga kumuoa na he would do anything for her..

Wa pili personally nashindwa hata kuelewa, moja ya kipimo kua the guy anakujali ni kukuruhusu kwenda kwake at what ever time or for what ever period.... Inawezekana kweli huyo mkaka yuko busy

Wa tatu Inawezekana huyo dada kapitia wanaume wengi wenye problems kibao na hatimae kampata the guy yuko fit katika kila sector i.e financially, physically, treatment (usichanganye kupigwa na kutreatiwa vibaya - mana mwingine very sensitive but kipigo hapo hapo), vitu kama kujali family ya mwanamke, kuwepo kwa ajili yake kwa lolote yani kwa ufupi reliable in every way!!! Sisemi it is right - but kwa perspective hio I can understand kama akifikilia what is kupigwa if the guy is right.

Pia kuvumilia kunatokana na ukweli kua katika maisha hata uwe mjanja kiasi gani lazima upitie kupat mpenzi atakae kushika maskio - ni kuomba tu Mungu alokushika maskio awe na busara.

Namuomba Mungu ampe ujasiri na macho ya kuona,anateseka na aweza teseka zaidi. mwambie wapo wanaume wenye uwezo wa kumpenda zaidi na kumthamini as well as kumuheshimu.Atulie awe na imani na subira na amuombe Mungu,atampa,yeye hapendi tuteseke kwa excuse ya nampenda sana......!
 
Endelea kuvumilia na usichoke utapata thawabu mbinguni, tena mbinguni unajilimbikizia mema usichokoze banaa

Niitafute thawabu mbinguni kwa kero za mtu za makusudi
Labda angekua mume watu wangesema mengine labda kuna watoto au dini inakubana lakini mpenzi!!!!!!
Hiyo thawabu aipate yeye kama ataweza kuvumilia hivyo visa
 
Hiyo dio adha ya long distance relationship, hapo tafuta tu wa kukupa company hivihivi kutu hii hapa
 
Namuomba Mungu ampe ujasiri na macho ya kuona,anateseka na aweza teseka zaidi. mwambie wapo wanaume wenye uwezo wa kumpenda zaidi na kumthamini as well as kumuheshimu.Atulie awe na imani na subira na amuombe Mungu,atampa,yeye hapendi tuteseke kwa excuse ya nampenda sana......!
Kweli kabisa michelle unateseka kabla hujaolewa! je ukiolewa ufanyeje sasa? anzamaisha mapya achana nae huyo utakufa na presha bure
 
Endelea kuvumilia na usichoke utapata thawabu mbinguni, tena mbinguni unajilimbikizia mema usichokoze banaa

Thawabu kwa kuvumilia mateso na wakati huo unatenda dhambi maana hujaolewa na mnafanya mapenzi Nafikiri ni tabia ya wamama kuvumilia tangu zamani
 
Wanaume tumeumbwa mateso mateso kuhangahika
Wanawake wameumbwa kuvumilia
Lol!!!
 
Dah haya mapenzi jamani. Dah tuweni na akili jamani wanawake, tunaweza kuishi bila hawa viumbe ni uamuzi tu. Wakati ukifika kama kuna kuolewa tutaolewa tu, kwa nini kuizika nafsi na roho kwa mtu asiyekupenda wala kujali? Dah hebu tufungukeni. Kama mtu ni sababu ya huzuni yako why unamganda? Wanaume wapo kibao wazee kwa vijana kama shida ni mapenzi, but kwani tumekosa nini hadi kujitesa namna hio? Dah mi mtu wala sifikirii mara mbili. Kinachotakiwa ni furaha na amani bwana. Kama mtu akupi furaha we wa nin

Si ndio hapo, na ajiendeage zake tu kha! na apite kama wenzie walivyopita bwana, shida ya nini maisha yenyewe mafupi
 
  • Thanks
Reactions: LD
Huyo dada ni mjinga (samahani kama ni nimetumia lugha nzito. Hivi anahitaji mtu kumwambia kuwa huyo jamaa anamtumia tu, tena kama taili la spea?

watu wengine bwana (awe KE au ME) nadhani wana matatizo ya akili....

Nimemchukia sana huyu binti...Kwani asipokuwa na mwanamume ndo atakuwa ame..R.I.P??

Nimechoka mwenzeni na hawa watoto... Mzee DC!!

mkubwa huwa hachoki.......lol
endelea kuwavumilia,kuwasikiliza na kuwaelimisha zaidi na zaid.,
 
Dah!! :doh::doh: Haya mambo banaa ona sasa hadi nimekosa hamu ya kula:hungry::hungry: usiku huu inatubidi:hail::hail: na:pray2::pray2: sana ili yasije kukuta halafu mtu ukaanza:fencing::fencing:kama sio :A S-cry::A S-cry: na:faint::faint:na :A S-confused1::A S-confused1:halafu una :rip::rip::rip: sababu ya :A S-heart-2::A S-heart-2:

Hahaha wewe bana!
 
Si ndio hapo, na ajiendeage zake tu kha! na apite kama wenzie walivyopita bwana, shida ya nini maisha yenyewe mafupi

Nimekumbuka wimbo wa pwani,
.....'usinitumie vibaya mtoto wa mwenzio wapo walionianza na wapo watakanimaliza"....

Jamani lakini nako kubadilisha sana mahusiano kama kiti cha daladala siyo vizuri hata kidogo......jamani msiache "kupambana"......lol

Kusema pambana ni rahisi sana, na hasa yanapokuwa kwa mwenzio,
manake kupambana kwingine ni kujitafutia R I P mapema....lol
 
Dada ana boyfriend wake na katika mahusiano yao anaona jinsi mwanaume wake anavyotoka na wadada wengine, haachani naye kabisa maana kila anapoongea na mwanaume kuhusu tabia yake hiyo anabembelezwa. Mwisho wa siku anakubali kuolewa na mwanaume huyu huyu asiye mwaminifu, huyu dada anakuwa anafikiria nini kichwani kwake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom