Swali kwa Katibu Mkuu (CCM) Kanali mstaafu Abdulrahmani Kinana na viongozi wakuu wengine

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Leo hapa Dodoma,Katibu Mkuu wa CCM Kinana ametoa taarifa ya vikao vya kesho na keshokutwa. Katibu Mkuu Kinana amesema,na ni kweli,kuwa Kamati Kuu(KK) itaketi kesho kupitisha jina la mgombea wa Uenyekiti wa CCM Taifa.

Kikao cha Kamati Kuu kitafuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kabla ya Mkutano mkuu maalum. Kinana amesema kuwa jina moja tu la Rais John Pombe Magufuli litajadiliwa na kupitishwa na KK kuwa mgombea wa Uenyekiti.

Sasa swali,jina hilo limepatikanaje na limepatikana lini? La nyongeza,kama kuna jina moja tu,kuna haja na mantiki gani ya vikao vya KK na NEC? KATIBA IHESHIMIWE!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Mafisadi chadema mpaka Leo hawajapeleka gharama walizotumia kwenye uchaguzi mkuu 2015.
 
Nimeamini maneno ya Mzee Mwanakijiji...." mafisadi wako radhi [kuchagua] UKAWA ya Lowassa kuliko CCM ya Magufuli!
 
Mzee Tupa Tupa ulikuwa kila siku humu ukituaminisha kuwa wajumbe wamejipanga kuleta sintofahamu Dodoma kumbe hukuwa na taarifa sahihi. Tusaidie kumhoji Mbowe wenu kwa nini amegeuka kuwa mfalme wa Chadema? Na pia jina Lowasa kuwa mgombea uraisi 2015 lilipatikana vipi?
 
Wewe uko wapi usiyeona sintofahamu niliyoiripoti?

Mzee Tupatupa
 
....nashangaa misukule ya lumumba imeishia kupiga kelele tu, nadhani jiwe la Tupatupa litakuwa limetua utosini!

jadilini mada!
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom