Swali kwa great thinkers wa JF

Kwenye huu uzi watu wamechangia maoni yao hata hivyo wengi wamekwepa kutoa jibu kama ni uzembe au la.
Nihitimishe hoja yangu kwa kusema mbunge anaetetea kiti chake cha ubunge kushindwa ndani ya Chama wakati wa kura za maoni ni Uzembe.

Nina sababu kadhaa.
1. Wapiga kura wanaopiga kura za maoni ndani ya vyama vya siasa wengi wao kwa asilimia kubwa bado wanasumbuliwa na maadaui wa taifa waliowahi kutajwa na rais wa awamu ya kwanza hayati mwl JK Nyerere hasa umasikini.

2. Democrasia yetu ni Changa ndani ya vyama vya siasa na nje ya vyama vya Siasa.

3. Rushwa imekuwa sehemu ya maisha yetu hivyo mtu kumpigia kura kiongozi yeyote bila chochote imekuwa ni jambo gumu sana kama kukuta boat imepaki stend ya mabasi.
 
Je ni uzembe wa khali ya juu kwa mbunge ambaye anatetea nafasi ya ubunge wake kushindwa kwenye kula za maoni ndani ya Chama?
Kushindea kwenye kura ya maoni si uzembe.

Kuna kupa picha halisi kuwa asilimia kubwa ya wenzio hawakubaliani na ww..
Sasa ni kazi yske kuangalia kutokukubaliwa huko kumeanzia wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom