Swali kwa Dr Slaa na JF kwa ujumla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa Dr Slaa na JF kwa ujumla

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eliphaz the Temanite, Jun 24, 2010.

 1. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mustakabari wa Nchi yetu unachukua mwelekeo ambao si tu unatishia kuipeleka nchi katika mikono ya watu wachache lakini pia tuko katika ukingo au huenda tayari tuna kuwa remote controlled na watu hawa wenye pesa zao(Mafisadi).

  Tunashuhudia jinsi gani ufisadi ulivyooanza kama kiwingu kidogo na kuendelea kukuwa na kuleta utando mkubwa na giza nene. Angalia serikali na mamalaka yake iliyonayo inavyoshindwa kuchukua hatua dhidi ya watu hawa licha ya ushahidi na vyombo vya habari kupigia kelele!

  Wachache wanaopiga kelele uovu huu ndio wamekuwa walengwa wakuu majimboni mwao wakitaka kung'olewa kwa gharama yeyote ile!

  Maswali ninayojiuliza kwanini serikali haichukui hatua dhidi ya hawa watu mathalani, ufisadi wa bandarini unaoripotiwa na vyombo vya habari kila kukicha mpaka wafanyabiashara wanahamia Mombasa na kuikosesha serikali mapato kiasi hiki?

  Wakati haya yote yakitokea ninajaribu kuwaza mustakabari wa nchi hii punde wingu hili litakapofunika na kusababisha giza totoro?

  Watanzania tufanye nini kuubadili mwelekeo huu ambao nguvu yake imefikia hatua ya kuishinda hata serikali?
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mlishaambiwa na mnajua la kufanya. Muhimu ni kuyatekeleza hayo!
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Mbona hili liko wazi. Hivi leo hii ukifungua duka na ukamkabidhi mtu aliendeshe, na unaona wateja wanakwenda kununua bidha kama kawaida,baada ya muda bidhaa zinakwisha na fedha haipo ,duka linafilisika,utamfanya nini mtu uliyempa kazi ya kutunza duka hilo? Mtunza duka huyo ni CCM, sasa watanzania tunataka mpaka Mungu ashuke mzima mzima aje atuambie cha kufanya? Mbona akili tunazo? Kuendelea kuichagua CCM ni kujitakia ufakara wa milele Tanzania
   
 4. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  La kufanya kila mmoja nalijua, lakini njia ya klifanya ndiyo tunatofautiana. La kufanya ni kuiondosha ccm once and for all period. Lakini mimi naona kabisa hakuna njia nyingine ya kufanya kuindosha ccm zaidi ya matumizi ya nguvu. Kama JWTZ haiwezi kuwasaidia watanzania katika hili, basi wananchi wachukue jukumu la kuingia mitaani mpaka watoke. Sanduku la kura kamwe haliwezi kuwa suluhisho la kufikia lengo la kuifurumisha ccm kwenye ikulu yetu.

  MAPINDUZI MAPINDUZI MAPINDUZI MAPINDUZI MAPINDUZI MAPINDUZI MAPINDUZI - NI LAZIMA DAMU IMWAGIKE KAMA KWELI TUNAIPENDA TANZANIA YETU.
   
 5. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Off-course Mimi na wewe tunalijua la kufanya, Lakini leo hii kuna Watz ambao wako tayari kuuza kura yake kwa nusu kilo ya chumvi na ndio majority wanaowapa kiburi CCM. Kama anafikia hatua ya kusema hahitaji kura ya mfanyakazi yeyote, mjenga nchi, anapata wapi kiburi na uhakika wa kuongea hadharani namna hiyo!
  Na kama ndio hivyo kwamba majority wanaowapa kura wako vijijini wasio jua nini kinaendelea, wanapinzani wanatumia mbinu gani kuwafikia na kuwaangazia ukweli!
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  It is known kuwa tatizo kubwa ni CCM!!!!!!!!!!!!!!
  Kura za ndio kwa CCM ndo sababu lilyotufikisha hapa.
  Tuiadhibu tu CCM kwa kuinyima kura na tutaona badiliko soon.
   
 7. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ndy twaweza kuinyima kura.......but r u sure hawataiba??????? hawamiliki kitu gani katika mfumo mzima wa Uchaguzi?????????????? Hawa kuwang'oa ni kwa m***** tu......Tumeshachoka sasa............................................
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,896
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ccm haitaweza kuangushwa kwenye sanduku la kura,they will rig the elections no matter what....Unless washindwe kwa kishindo ili hata kama wakiiba waumbuliwe.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,419
  Likes Received: 81,465
  Trophy Points: 280
  Mkuu wakishindwa kwa kishindo basi nao wataiba kura kwa kishindo ili kugeuza matakwa ya Watanzania, lakini pia kutokana na wapiga kura wengi ndani ya nchi yetu hasa wale wa vijijini hata mijini pia kuwa mbumbumbu sidhani kama hili litatokea katika miaka ya karibuni labda mwaka 3010.
   
 10. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #10
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  JMushi na Wana JF,
  Nadhani askari anayeenda vitani kwa kukata tamaa ameshindwa hata kabla vita haijaanza.i) Tuwe na ujasiri, tunaoelewa tuwaelimishe na kuwatia ujasiri wale ambao au hawaelewi au hawajui uhusiano kati ya kura yao moja moja na hali mbaya ya maisha au maisha magumu wanayoishi. Watanzania kwa uzoefu wangu ni watu wasikivu sana, na ndiyo maana pamoja na nguvu ya Taifa ya CCM na Serikali hali ya ushindi ilikuwa wazi kabisa Bussanda na Biharamulo. Sisi wenyewe tuchukue hatua, tuwe "proactive" kila mmoja alipo na kwa kupitia marafiki zake. Multiplier effect principle ikitumika mabadiliko yatatokea katika nchi hii. ii) Kura zinahitaji tu kulindwa. Hakuna short cut, wala hakuna dawa wala uchawi katika hili. Hatutazuia rigging kwa maneno. We need to strategise and take action. We did it in Biharamulo and Bussanda and the results were visible. Wote wenye kukataa ufisadi, tusiukatae kwa maneno bali tuukatae kwa matendo. Wangapi kwa maneno tunaupiga vita lakini kugombea kila kukicha tunatangaza nia kupitia CCM. Kwa hali hii tusiwalau watanzania wa vijijini, kwani kama hata wasome bado wanaona ubunge unapatikana kupitia CCM tu, basi safari bado ni ndefu sana. Mabadiliko radical yanatakiwa kwetu sisi kabla ya wananchi, ambao wengi kukitokea Leadership watafuata bila wasiwasi. iii) Kimsingi mabadiliko yanaletwa na Rasilimali watu. Fedha ni nyenzo muhimu lakini, pre condition ni rasilimali watu. Kama wote wanaoandika kwenye jamvi hili tungelikuwa proactive, na kuamini kwa dhati tunayoandika, nina hakika mabadiliko yatatokea kwa sababu chachu muhimu sana na rasilimali watu inayofahamu Taifa linahitaji nini, Taifa linaelekea wapi na namna gani tuliepushe kutoka kwenye hatari hiyo. Lets play our part it can be done. Kukata tamaa ni dhambi mbaya isiyosameheka.
   
 11. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Mbona hawafanikiwi kumwibia Dr. Slaa kule karatu?

  Ukilia lia mwizi kila siku kweli utaibiwa. Abiria chunga mzigo wako na utafika salama.
   
 12. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  May be kuna Kuna ufumbuzi wa Kisayansi! Afterall Political Science ni nini? Hatuwezi kulichimba, tukangundua root cause! Then tuka-device a plan ya kuing'oa CCM! Naambiwa Obama ni kati ya Wagombea wachache nchini Marekani ambayo wamewahi kuendesha campaign kwa ufanisi wa hali ya juu! Nina uhakika kabisa mafanikio hayo hayakuja kama ajali ama hayakuja kwa sababu alifanya yale ya kila siku! Kulikuwa na mpango kabambe uliotekelezwa kwa umakini mkubwa.

  Vyama vyetu vya upinzani vinatakiwa vianze kwa malengo na mikakati! Haiingii akili mgomea yuleyule five times consecutively anshindwa anarudi, anashindwa anarudi, Chama makini haifanyi hivyo! Tutaendelea kuwapa sifa tu CCM! Maana hakuna jipya!
  Upinzani uanze kwa kulenga makundi maalumu, mikoa na wilaya, madhalani vyuo vikuu ambako ninauhakika kabisa vijana wanaielewa rythim na mdundo wa ngoma, its just a matter of inviting them to play!

  Halafu no matter how the constraints may be tujitahidi kufanya kile tunachowaahidi wananchi! Kidogo kidogo watu wataanza kufumbua macho!
   
Loading...