Swali kwa Dkt. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa Dkt. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyani Ngabu, Aug 30, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Je, utakaposhinda uraisi utaweka wazi mshahara wako (mshahara wa raisi) ambao kwa ufahamu wangu mimi unalipwa kutokana na kodi za wananchi?
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Mbona ashasema kuwa ataupunguza for twenty % mkubwa? Fuatilia hotuba zake!
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hilo nakuomba jihakikishie atalifanya. Zaidi ya hapo wewe mwananchi utachangia kuupanga mshahara huo nakuhakikishia hilo. Usisahau kuwa wewe mwananchi ndiye mwajiri
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo keshasema mshahara wake utakuwa public knowledge? Maana kusema tu utaupunguza kwa asilimia flani haina maana wananchi wakitaka kujua unalipwa mshahara kiasi gani basi watapata hiyo taarifa kwa urahisi....
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Siwezi kujihakikishia bila ya yeye kutamka. Mimi namtaka yeye mwenyewe kwa maneno yake aseme na tumweke kwenye rekodi.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hii mbona simpo mkubwa? Kama unaufahamu aupatao Ki'wete basi Slaa ataupunguza kwa hiyo % akikabidhiwa rungu!
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  genekai. Anachosema au kumaanisha NN ni kwamba hata huo anaopata Kikwete ni sirikali. Uwekwe hadharani, au hata Dr haujui?
   
 8. M

  Miruko Senior Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 173
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nitapunguza mshahara wa rais kwa 20% - Dkt.Slaa

  *Wabunge, wakuu wa mashirika kupunguziwa 15%
  *Lengo kupunguza matumizi ya anasa serikalini

  Na Tumaini Makene

  MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa amesema ufisadi unaoisumbua Tanzania kwa sasa ni tishio la hatari kuliko vita na amepania kupunguza matumizi ya anasa serikalini kwa kuanza na mshahara wa rais.

  Hayo yamo kwenye ilani ya uchaguzi wa CHADEMA iliyozinduliwa juzi katika Uwanja wa Jangwani, Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw, Freeman Mbowe na kukabidhiwa kwa Dkt. Slaa ili kuitumia kusaka kura za Watanzania kuingia ikulu.  Anasema: "CHADEMA itabana matumizi ya serikali ya anasa yasiyo na umuhimu kwa taifa na kuunda serikali ndogo inayozingatia tija ya matumizi ya fedha, ufanisi na utendaji...tutapunguza mishahara na posho za viongozi wote wa juu wa kisiasa kuanzia rais hadi wakuu wa mikoa kwa asilimia 20.

  "Mishahara na posho za wabunge zitapunguzwa kwa asilimia 15 huku mishahara na posho za watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za umma itapunguzwa kwa silimia 15...tutapanua wigo wa mapato ya kodi, ikiwemo kufuta misamaha holela ya kodi.

  Katika kitabu cha ilani ya CHADEMA cha kurasa 104, Dkt. Slaa amefafanua mambo atakayotekeleza katika miaka mitano ijayo, huku akitumia dibaji ya kitabu hicho kuweka wazi msimamo wa wake katika mapambano dhidi ya ufisadi.

  Akinukuu maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere aliyewahi kutoa kauli ya namna hiyo bungeni, Dkt. Slaa alitoa tafsiri ya ufisadi akisema kuwa mfumo huo unadidimiza tawala mbalimbali duniani bila kushughulikiwa kikamilifu, unasimama kama tishio kwa mstakabali wa nchi.

  "Unapozungumzia ufisadi unazungumzia mfumo na muundo wa utawala ambao umetengeneza utamaduni wa kuishi kiunja ujanja, matumizi mabaya ya madaraka na vyeo, ufujaji wa mali za umma na wizi wa fedha za umma.

  "Utaratibu wa kubebana, ajira zinazotegemea kujuana, mahusiano ya watawala na watawaliwa ambayo msingi wake ni woga, vitisho na kujiona watu wanastahili zaidi kuliko wengine...pasipo kuushughulikia kwa makusudi unasimama kama tishio na hatari kwa Tanzania kuliko vita.

  "Mwalimu Nyerere alisema kuwa "ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi wa maslahi ya wananchi wakati wa amani kuliko vita" (Bungeni, Mei 17, 1960, kikao cha 35 cha bajeti)," alisema Dkt. Slaa.

  Ilani hiyo ya CHADEMA iliyobebwa katika falsafa yao ya 'nguvu ya umma' inaeleza kuwa Tanzania inahitaji uongozi wa kizalendo, adilifu, makini, wenye upeo, ili kujenga jamii iliyo na uhuru wa kweli, usawa, wajibu na fursa kwa kila Mtanzania, kama anayotaka kuunda.

  Ilani hiyo imeainisha vipaumbele tisa, ikionesha mapungufu ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maeneo hayo, huku wakionesha sera mbadala katika sekta hizo, iwapo wakichaguliwa kuongoza serikali baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu.

  Katika ilani hiyo imeelezwa kuwa CHADEMA wataweka mazingira ya kila mtoto wa Kitanzania kupata fursa ya elimu kwa kuwa ndiyo nguzo kuu ya maendeleo na nyenzo ya haraka na ya uhakika katika kujenga taifa la kisasa, ambapo wananchi wenye elimu duni au wasiokuwa na elimu, hawawezi kuiwajibisha serikali yao wala wao kuwajibika.

  Inaeleza kuwa mfumo wa elimu nchini una matatizo mawili, ambayo ni uduni wa elimu yenyewe, inayozungumzia wingi wa vitu badala ya ubora wa kile kinachopatikana, tatizo lingine ni kuwa elimu hiyo 'inataalumisha' zaidi badala ya 'kutaalamisha', hivyo haiwasaidii wahitimu kujitegemea.

  Kuhusu huduma zingine za jamii kama vile afya, maji na uendelezaji wa makazi na nyumba, CHADEMA wameonesha kasoro zilizopo mpaka sasa wakisema kwa muda mrefu zimetelekezwa na Serikali ya CCM, ambapo wao wamesema huo ndiyo msingi wa nguvu kazi kwa taifa lolote lile.

  "Serikali ya CCM imetelekeza hospitali na zahanati nyingi za umma. Leo hii kwenda kutibiwa katika hospitali nyingi za serikali ni kama kucheza bahati nasibu. Kina mama wanajifungulia sakafuni, idadi ya watumishi wa kada za afya bado ipo chini kwa asilimia 65.

  "Katika Serikali ya CHADEMA...huduma ya bima ya afya itakuwa hitaji la lazima kwa kila Mtanzania, bila kujali kama ni mfanyakazi wa serikali au la. Ili kuwawezesha wananchi vijijini na wale wasio na ajira katika mfumo rasmi...itatenga fedha za kutosha kufikia asilimia 15 ya bajeti ya afya kama ilivyo katika mikataba ya kimataifa.

  "CHADEMA inaamini kuwa maji ni uhai, bila maji hakuwezi kuwa na kilimo cha uhakika wala uzalishaji wa maana viwandani... badala ya kusema kilimo kwanza, tuseme maji kwanza, maana maji ndiyo msingi wa kilimo bora...angalau asilimia 60-70 ya wananchi wapate maji safi na salama 2015," inaeleza sehemu ya Ilani hiyo.

  Katika kuendeleza makazi na nyumba CHADEMA inaeleza cahma hicho kitalivunja Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kushindwa kuleta mabadiliko kama ilivyokusudiwa.

  Badala yake itaunda Mamlaka ya Taifa ya Uendelezaji Makazi na Nyumba yenye nguvu na muundo wa kusimamia ujenzi katika makazi ya watu, miundombinu na ubora wa makazi hayo ili yaendane na maisha ya kisasa ambayo Watanzania wanayatamani na kuyastahili.

  Pia inaeleza kuwa moja ya hatua watakazochukua katika kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu ni pamoja na kutungwa kwa sheria inayozuia ubaguzi kwa watu hao lengo likiwa ni kuwawezesha waishi maisha bora ili watoe mchango wao kwa taifa kama Watanzania wengine.

  Zingine ni kuharakisha utekelezaji wa mfuko maalumu kwa ajili ya kuwawezesha kushiriki fursa za kiuchumi kwa njia ya mikopo, mafunzo maalumu kuwapatia stadi za maisha kupitia vyuo vya VETA, ajira za upendeleo pale wanapokuwa na sifa stahiki, kuwahakikishia mazingira bora shuleni na sehemu nyingine za kujifunzia.

  Katika kilimo, inaeleza kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kukosekana kwa mipango thabiti na ya muda mrefu, huku wakiamini kuwa kwa sasa na muda mrefu ujao, kilimo ndiyo nguzo kuu ya uchumi.

  Inaeleza kuwa wao 'wanaamini' katika kilimo bora na si kilimo kwanza, hivyo watahakikisha matumizi ya mbolea ya asili na mboji kwa maeneo husika, kuanzisha maeneo maalumu kwa ajili ya kilimo cha kioganiki, shule za sekondari za kilimo zitatoa mafunzo kuandaa maisha ya kilimo cha kisasa.

  Pamoja na uwekezaji katika utafiti wa kilimo, watahakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ya kioganiki ambayo wanaamini yatashindana katika soko la dunia, baada ya kuwa yamezalishwa kwa kutumia gharama nafuu, mtindo unaotumika China na India.

  Mipango ya CHADEMA katika kilimo inajumuisha uzalishaji wa mazao na ufugaji, ambapo inaeleza watahimiza ufugaji bora ili wafugaji wapate faida kutokana na kazi yao pia wataanzisha ushirika wa masoko ili waweze kuwa nguvu ya kuuza mazao yatokanayo na mifugo.

  Pia wameelezea namna gani kila Mtanzania anayo fursa ya kujenga na kumiliki uchumi imara na shirikishi, kwa nia ya kukuza uchumi endelevu, ili kuondokana na utegemezi na umaskini wa nchi kwa kutumia kwa makini, uzalendo na uadilifu rasrimali za taifa kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

  "Lengo kuu la CHADEMA kuhusu uchumi ni kujenga uchumi imara na shirikishi, ili hatimaye mafanikio yeyote ya uchumi ya kitakwimu yaendane na kuboreka kwa hali za wananchi kunakoambatana na kupungua kwa gharama za maisha.

  "Hivyo basi, Serikali ya CHADEMA itatilia mkazo katika kukuza uzalishaji kwenye uchumi mdogo kama msingi wa ukuaji wa uchumi mkubwa ili kujenga taifa za wazalishaji badala ya taifa la wachuuzi tu. Kufikia haya, tunahitaji serikali makini sana, imara na bora zaidi, yenye uadilifu na upeo mkubwa.

  "Inayoweza kusimamia uchumi na rasrimali zetu, la sivyo Watanzania wataendelea kuwa watazamaji na sio washiriki wa uchumi na rasrimali zao...ukuaji wa uchumi nchini miaka ya karibuni haujawa na manufaa kwa wananchi wa kawaida, umaskini unaongezeka kila uchao.

  Kwa ufupi CHADEMA wamesema kuwa uchumi wa Tanzania ni uchumi uliolala, wakiwa na maana kuwa kinachoonekana kama shughuli mbalimbali za kiuchumi ni kiduchu ya kile kinawezekana kufanyika. Pia ni uchumi bandia kwa sababu vitendo vya ufisadi vilivyoathiri shughuli mbalimbali:

  Za kiuchumi hadi ngazi za juu za Serikali, vimesababisha kile kinachoripotiwa katika vipimo mbalimbali hakiakisi ukweli hasa wa kiuchumi nchini. Hivyo kutokana na hayo mawili uchumi wa nchi unahitaji kuamushwa na kusahihishwa.

  Kwa ujumla ilani ya chama hicho yenye vipaumbele tisa, ambavyo vyote vimebebwa na kipaumbele cha 'uongozi bora na mfumo mpya wa utawala', imesema kuwa kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais wa CHADEMA, Watanzania watakuwa wamechagua mabadiliko, ubora na maendeleo.

  "Hatuwezi kuendelea kuongozwa na nadharia kuwa maendeleo ni 'wingi wa vitu' kama ambavyo Serikali (CCM) imekuwa ikifanya. Serikali ya CHADEMA itaweka mkazo katika maendeleo ya watu na kuhakikisha kuwa maendeleo ya vitu yanakuwa kwa ajili ya maendeleo ya watu," imesema ilani hiyo.

  Vipaumbele hivyo tisa ni elimu, huduma bora za jamii, kilimo bora, uchumi imara na shirikishi, uongozi bora na mfumo mpya wa utawala, ajira na ujira bora kwa kila Mtanzania.

  Vingine ni kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuzingatia matishio ya kissasa na mbinu za kisasa, kukuza nafasi ya Tanzania katika diplomasia ya kimataifa na tisa; kuinua na kukuza sanaa, michezo na utamaduni wa Mtanzania. Source: Majira
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  Du!, hivi kumbe kuna watu walimdhania huyu jamaa anaweza kushinda urais ndio maana alipania sana hadi kukamia kuwa 2015 atagombea tena na atashinda, sasa huku kususa kote kumbe ni hasira za kuukosa urais!.

  Pasco
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Aug 4, 2015
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco mmevamia nyumba ya jirani na kuleta sokomoko sasa mnachekelea!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. mweusi asili

  mweusi asili JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2015
  Joined: Nov 11, 2014
  Messages: 485
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  ivi mshahara anaolipwa kama katibu mkuu wa chama umepungua ili fedha zingine za luzuku zifike huku kijijini kwetu angalau tujenge ofisi za chama?!
   
 12. k

  kabongo1980 Member

  #12
  Aug 4, 2015
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 57
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hazijapungua mkuu. Ila kiukweli jamaa ana hasira sana za kuukosa uraisi na akubali tu kwamba waamuaji ni wenye chama hapa namzungumza Mzee Mtei. Yeye kuasisi chama ndiko kunakowafanya wanakula wanavaa na wanaendesha magari na baada ya miaka 5 wanakula m200 na upuuzi. Kwa sisi wachaga tunasema wakishapokea inabidi wapeleke kilo 2 ya sukari kwa mzee sasa kama kapumzishwa ili hata Lowassa akikosa uraisi ruzuku iongezeke basi jamaa akubali tu yaishe wenye mali yao washaongea a simple is that. Period over my dead body sema na mbowe aache kutumia haya maneno yanawaumiza wenzake. Over my dead body
   
Loading...