Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 20,372
- 30,311
Lini bunge litachukua hatua ya kuwafukuza bungeni kutokana na kupoteza sifa za kuwa wabunge ?Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho.
Ikaripotiwa na hata kusemwa na mmoja wa waliofukuzwa uanachama Bungeni Dodoma (Jesca Kishoa) kuwa wapo waliofukuzwa uanachama ambao walikata rufaa kupinga kufukuzwa kwao uanachama. Mamlaka ya rufaa imeripotiwa kuwa ni Baraza Kuu la CHADEMA.
Ni miezi mingi sasa imepita tangu akina Halima Mdee wafukuzwe uanachama na baadhi yao kukata rufaa. Lini hasa rufaa zao zitasikilizwa na uamuzi wa mwisho kichama kutolewa juu yao? Ukimya huu ni baraka za kificho kuwa akina Halima Mdee waendelee na mambo yao ukiwemo Ubunge?