Swali kwa CHADEMA: Lini rufaa za akina Halima Mdee na wenzake 18 zitasikilizwa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,515
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Ikaripotiwa na hata kusemwa na mmoja wa waliofukuzwa uanachama Bungeni Dodoma (Jesca Kishoa) kuwa wapo waliofukuzwa uanachama ambao walikata rufaa kupinga kufukuzwa kwao uanachama. Mamlaka ya rufaa imeripotiwa kuwa ni Baraza Kuu la CHADEMA.

Ni miezi mingi sasa imepita tangu akina Halima Mdee wafukuzwe uanachama na baadhi yao kukata rufaa. Lini hasa rufaa zao zitasikilizwa na uamuzi wa mwisho kichama kutolewa juu yao? Ukimya huu ni baraka za kificho kuwa akina Halima Mdee waendelee na mambo yao ukiwemo Ubunge?
 
Hakuna aliefukuzwa uanachama wala aliekata rufaa, hili unaloliona ni igizo kama yalivyo maigizo mengine, ili kuwahadaa wanachama wao waweze kukichangia chama kwa madai kwamba sasa hivi chama hakipati ruzuku kutoka serikalini.

Ila nyuma ya pazia kinapata ruzuku kama kawa ila inaliwa na mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu na genge lao huku mitandaoni. Usipoteze muda na nguvu zako kuwaamini wanasiasa hata siku moja.
 
Kuhusu Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee: Mambo yako wazi ila wahusika wako kimya

Thread starterPetro E. Mselewa Start dateApr 27, 2021
Tagshalima mdee kuhusu maalum mambo wabunge wazi
1 of 4
Next
Last
Jump to new
Ignore
Watch

Petro E. Mselewa
Verified Member ✅
Apr 27, 2021
Add bookmark
#1
Mwanzo mwanzoni niweke wazi, kama ilivyo kawaida yangu, kuwa mimi si mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini au nje ya nchi hii. Nikiongozwa na uzalendo na utanzania wangu, huwa naunga mkono hoja zozote za kuujenga utaifa wetu na kuleta maendeleo ya Tanzania yetu. Natazama hasa mantiki na uzito wa hoja bila ya kujali ameisema nani na ni wa chama gani.

Pili, naomba kumpa pole Ndugu Jesca Kishoa kwa 'kulazimika' kufuta kauli yake kuwa 'alishaondolewa CHADEMA' ili kulinda Ubunge wake pale alipobanwa na kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika Daktari Tulia Ackson Mwansasu. Kishoa ni kama aliteleza katika kusema hivyo na akaifuta kauli yake 'kinyonge na kwa huruma' sana. Kuna wakati siasa huutweza hata utu angalau tu mambo yaende.

Hoja yangu hapa ni kuanika baadhi ya 'facts' ambazo zitaonyesha kuwa sakata la Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee liko wazi ila wahusika wanajifanya kutoona na hivyo kulinyamazia. Fuatana nami hapa ujionee yaliyo ya wazi;

Mosi, akina Halima Mdee walishtakiwa na KUFUKUZWA UANACHAMA na kilichokuwa chama chao cha CHADEMA. Mchakato wa hilo na UAMUZI huo ulitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika na hata Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikaeli Mbowe. Sitaki hapa nizungumzie utaratibu uliofuatwa kufikia UAMUZI huo kwakuwa sisi wafuatiliaji hatuna ushahidi juu ya hilo la utaratibu.

Pili, akina Halima Mdee walitangaza kukata rufaa ndani ya CHADEMA kupinga UAMUZI huo. Hadi hapa iko wazi kuwa kuna UAMUZI uliotolewa na CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee na huo UAMUZI ndiyo uliokatiwa rufaa na wahusika hao. Ifahamike pia kuwa UAMUZI huo unawafanya akina Mdee KUTOKUWA WANACHAMA wa CHADEMA hadi pale utakapobadilishwa na mamlaka ya rufaa ndani ya CHADEMA.

Tatu, katika uga wa kisheria, KUKATA RUFAA hakufuti UAMUZI uliofikiwa hadi pale rufaa itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi mwingine. Ndiyo kusema, kuanzia siku ya KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee, UAMUZI ule umebaki hata sasa. Ni kwamba, wote WALIOFUKUZWA UANACHAMA, si wanachama wa CHADEMA. Wanachopambania kwenye rufaa zao ni KUREJESHEWA UANACHAMA WAO ndani ya CHADEMA. Kama wao kwasasa ni wanachama wa CHADEMA, wamekata rufaa ili kupata uamuzi upi tena?

Nne, nakubaliana na Naibu Spika Daktari Tulia (alipokuwa akimueleza Jesca Kishoa Bungeni) kuwa kwa mujibu wa Katiba kila Mbunge lazima atokane na chama cha siasa. Tena, kupoteza UANACHAMA wa chama cha siasa ni kupoteza nafasi yoyote ya kisiasa ya kuchaguliwa kama Ubunge na Urais. Natofautiana na kaka na mtani wangu Pascal Mayalla aliyeandika humu JF kuwa Mbunge ANAPOTEULIWA hawezi kuondolewa na chama chake. Chama cha siasa kinaweza kumfukuza mwanachama wake na uongozi unakomea hapo.

Tano, akina Halima Mdee, kuanzia siku ya UAMUZI wa CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA, hawakupaswa kuendelea kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu iko wazi: SI WANACHAMA wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania kuwawezesha kuwa Wabunge wa Viti Maalum. Sikugusia mchakato wa kupatikana kwao kwakuwa sina ushahidi nao. Nazungumzia kilichotokea baada ya wao kutangazwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Wahusika wanaujua ukweli huu lakini wamekuwa kimya. Fedha za umma zinaendelea kuwalipa wasio Wabunge. Kulingana na Naibu Spika, Ofisi ya Spika haina TAARIFA YA KUFUKUZWA UANACHAMA WA CHADEMA kwa akina Halima Mdee. Hili lina ukweli gani? Linabadilije UAMUZI wa CHADEMA? Tuwe wakweli katika hili na kutenda yatupasayo kutenda kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi yetu.
 
Verified Member

Asante sana Mkuu. Ubarikiwe.
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Ikaripotiwa na hata kusemwa na mmoja wa waliofukuzwa uanachama Bungeni Dodoma (Jesca Kishoa) kuwa wapo waliofukuzwa uanachama ambao walikata rufaa kupinga kufukuzwa kwao uanachama. Mamlaka ya rufaa imeripotiwa kuwa ni Baraza Kuu la CHADEMA.

Ni miezi mingi sasa imepita tangu akina Halima Mdee wafukuzwe uanachama na baadhi yao kukata rufaa. Lini hasa rufaa zao zitasikilizwa na uamuzi wa mwisho kichama kutolewa juu yao? Ukimya huu ni baraka za kificho kuwa akina Halima Mdee waendelee na mambo yao ukiwemo Ubunge?
Inaonyesha hukuwa TANZANIA UMERUDI LINI? RUFAA ITASIKILIZWA MZEE HUU WA JULY
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Ikaripotiwa na hata kusemwa na mmoja wa waliofukuzwa uanachama Bungeni Dodoma (Jesca Kishoa) kuwa wapo waliofukuzwa uanachama ambao walikata rufaa kupinga kufukuzwa kwao uanachama. Mamlaka ya rufaa imeripotiwa kuwa ni Baraza Kuu la CHADEMA.

Ni miezi mingi sasa imepita tangu akina Halima Mdee wafukuzwe uanachama na baadhi yao kukata rufaa. Lini hasa rufaa zao zitasikilizwa na uamuzi wa mwisho kichama kutolewa juu yao? Ukimya huu ni baraka za kificho kuwa akina Halima Mdee waendelee na mambo yao ukiwemo Ubunge?

Katika uga wa kisheria, KUKATA RUFAA hakufuti UAMUZI uliofikiwa hadi pale rufaa itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi mwingine. Ndiyo kusema, kuanzia siku ya KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee, UAMUZI ule umebaki hata sasa. Ni kwamba, wote WALIOFUKUZWA UANACHAMA, si wanachama wa CHADEMA.

akina Halima Mdee, kuanzia siku ya UAMUZI wa CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA, hawakupaswa kuendelea kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu iko wazi: SI WANACHAMA wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania kuwawezesha kuwa Wabunge wa Viti Maalum.
Imeisha hiyo
 
Kuhusu Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee: Mambo yako wazi ila wahusika wako kimya

Thread starterPetro E. Mselewa Start dateApr 27, 2021
Tagshalima mdee kuhusu maalum mambo wabunge wazi
1 of 4
Next
Last
Jump to new
Ignore
Watch

Petro E. Mselewa
Verified Member ✅
Apr 27, 2021
Add bookmark
#1
Mwanzo mwanzoni niweke wazi, kama ilivyo kawaida yangu, kuwa mimi si mwanachama wala mshabiki wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini au nje ya nchi hii. Nikiongozwa na uzalendo na utanzania wangu, huwa naunga mkono hoja zozote za kuujenga utaifa wetu na kuleta maendeleo ya Tanzania yetu. Natazama hasa mantiki na uzito wa hoja bila ya kujali ameisema nani na ni wa chama gani.

Pili, naomba kumpa pole Ndugu Jesca Kishoa kwa 'kulazimika' kufuta kauli yake kuwa 'alishaondolewa CHADEMA' ili kulinda Ubunge wake pale alipobanwa na kutakiwa kufanya hivyo na Naibu Spika Daktari Tulia Ackson Mwansasu. Kishoa ni kama aliteleza katika kusema hivyo na akaifuta kauli yake 'kinyonge na kwa huruma' sana. Kuna wakati siasa huutweza hata utu angalau tu mambo yaende.

Hoja yangu hapa ni kuanika baadhi ya 'facts' ambazo zitaonyesha kuwa sakata la Wabunge 19 wa Viti Maalum wakiongozwa na Halima Mdee liko wazi ila wahusika wanajifanya kutoona na hivyo kulinyamazia. Fuatana nami hapa ujionee yaliyo ya wazi;

Mosi, akina Halima Mdee walishtakiwa na KUFUKUZWA UANACHAMA na kilichokuwa chama chao cha CHADEMA. Mchakato wa hilo na UAMUZI huo ulitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika na hata Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikaeli Mbowe. Sitaki hapa nizungumzie utaratibu uliofuatwa kufikia UAMUZI huo kwakuwa sisi wafuatiliaji hatuna ushahidi juu ya hilo la utaratibu.

Pili, akina Halima Mdee walitangaza kukata rufaa ndani ya CHADEMA kupinga UAMUZI huo. Hadi hapa iko wazi kuwa kuna UAMUZI uliotolewa na CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee na huo UAMUZI ndiyo uliokatiwa rufaa na wahusika hao. Ifahamike pia kuwa UAMUZI huo unawafanya akina Mdee KUTOKUWA WANACHAMA wa CHADEMA hadi pale utakapobadilishwa na mamlaka ya rufaa ndani ya CHADEMA.

Tatu, katika uga wa kisheria, KUKATA RUFAA hakufuti UAMUZI uliofikiwa hadi pale rufaa itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi mwingine. Ndiyo kusema, kuanzia siku ya KUWAFUKUZA UANACHAMA akina Halima Mdee, UAMUZI ule umebaki hata sasa. Ni kwamba, wote WALIOFUKUZWA UANACHAMA, si wanachama wa CHADEMA. Wanachopambania kwenye rufaa zao ni KUREJESHEWA UANACHAMA WAO ndani ya CHADEMA. Kama wao kwasasa ni wanachama wa CHADEMA, wamekata rufaa ili kupata uamuzi upi tena?

Nne, nakubaliana na Naibu Spika Daktari Tulia (alipokuwa akimueleza Jesca Kishoa Bungeni) kuwa kwa mujibu wa Katiba kila Mbunge lazima atokane na chama cha siasa. Tena, kupoteza UANACHAMA wa chama cha siasa ni kupoteza nafasi yoyote ya kisiasa ya kuchaguliwa kama Ubunge na Urais. Natofautiana na kaka na mtani wangu Pascal Mayalla aliyeandika humu JF kuwa Mbunge ANAPOTEULIWA hawezi kuondolewa na chama chake. Chama cha siasa kinaweza kumfukuza mwanachama wake na uongozi unakomea hapo.

Tano, akina Halima Mdee, kuanzia siku ya UAMUZI wa CHADEMA wa KUWAFUKUZA UANACHAMA, hawakupaswa kuendelea kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu iko wazi: SI WANACHAMA wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania kuwawezesha kuwa Wabunge wa Viti Maalum. Sikugusia mchakato wa kupatikana kwao kwakuwa sina ushahidi nao. Nazungumzia kilichotokea baada ya wao kutangazwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum.

Wahusika wanaujua ukweli huu lakini wamekuwa kimya. Fedha za umma zinaendelea kuwalipa wasio Wabunge. Kulingana na Naibu Spika, Ofisi ya Spika haina TAARIFA YA KUFUKUZWA UANACHAMA WA CHADEMA kwa akina Halima Mdee. Hili lina ukweli gani? Linabadilije UAMUZI wa CHADEMA? Tuwe wakweli katika hili na kutenda yatupasayo kutenda kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi yetu.
Hivi unafikiri bunge halina akili?Hivi unafikiri spika hana pakujitetea hata akiitwa mahakamani? Mchezo mzima wanaujuwa ulivyoenda mpaka wakawafukuza uanachama isivyo halali unafikiri hayo majina ndugai aliyateua yeye bila kuletewa na tume ya uchaguzi>?Inamaana anavyo vielelezo husika na akiitwa mahakamani anavitoa ambayomitakuwa aibu kubwa kwa katibu mkuu CHADEMA na mbowe pia CHADEMA walipeleka majina lakini wakashindwa kupatana wakazungukana hilo linajulikana kila mtu anataka apeleke wa kwake sasa hoja yangu je hakuna mahakama ya kumshitaki sp0ika na mwanasheria ili kubatilisha uwepo wao bungeni? Na je kama hawakupeleka majina kwanini wasipeleke wanayoona yana faaa kuwa wabunge? Wanaona ishu yao itabuma itafichuka hapo hawawezi kwenda mahakamani hata siku moja mbowe na genge lake ni wahuni haijapata kutokea
 
CHADEMA walichukua hayo maamuzi kuwatuliza wanachama wao ila kama kweli walikuwa na nia ya kuwafukuza wangeshaitisha kikao cha baraza kuu ili watoe maamuzi.
Wengine wabunge wa viti maalumu ni wake wa viongozi wa CHADEMA hapo unaona wazi kuna mchezo unaendelea.
Unajua maamuzi ya Rufaa ya kina Mdee ikiwa watarudishiwa uanachama wao na nafasi zao bado wao kina Mdee ndio watapaswa kuwasilisha kwa Spika nakala za Rufaa yao na sio Chama kuwasilisha nakala kwa Spika. Kazi ya Chama iliisha kwa kuwafuta na kuwasilisha barua kwa Spika, Spika ndio akaamua kufanya yale anayofanya sasa.
 
Ni taarifa rasmi iliyotolewa na CHADEMA kuwa Halima Mdee na wenzake 18 walifukuzwa uanachama wa CHADEMA kwa makosa mbalimbali waliyoyatenda dhidi ya chama chao. Walifukuzwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Ikaripotiwa na hata kusemwa na mmoja wa waliofukuzwa uanachama Bungeni Dodoma (Jesca Kishoa) kuwa wapo waliofukuzwa uanachama ambao walikata rufaa kupinga kufukuzwa kwao uanachama. Mamlaka ya rufaa imeripotiwa kuwa ni Baraza Kuu la CHADEMA.

Ni miezi mingi sasa imepita tangu akina Halima Mdee wafukuzwe uanachama na baadhi yao kukata rufaa. Lini hasa rufaa zao zitasikilizwa na uamuzi wa mwisho kichama kutolewa juu yao? Ukimya huu ni baraka za kificho kuwa akina Halima Mdee waendelee na mambo yao ukiwemo Ubunge?
Malisa Godlisten jibu
 
Back
Top Bottom