Swali kwa CCM taifa: Ni kwanini serikali haijashusha bei mafuta ya taa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa CCM taifa: Ni kwanini serikali haijashusha bei mafuta ya taa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bagain, Dec 15, 2011.

 1. b

  bagain JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Ninaomba viongozi wa ccm taifa mjibu hili swali. wakati wananchi walipolalamikia kupanda kwa bei ya mafuta ya taa ilifika point nanyi kupitia vikao vyenu mkaonyesha kusikitishwa na hili jambo hata kufikia hatua ya kutoa taarifa.

  Pamoja na taarifa yenu kwa umma kuwa mnashauri bei ishushwe LAKINI HADI LEO HII MAFUTA YA TAA BEI INAZIDI KUPANDA.


  Je ni kweli mlikuwa na nia thabiti ya kutaka bei ipungue au mlikuwa mnatudanganya watanzania?

  Je serikari ilikataa ushauri wenu ? Na kama ilikataa mbona hamkutoa hiyo taarifa ili wananchi tujue?


  Mwisho: je nanyi wabunge wa tanzania ambao wengi ni ccm mnaona bei ya mafuta ya taa ni sawa? Kumbukeni ninyi ndio mliyoipitisha bajeti.

  Naomba majibu.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  samahni naomba niulize, kwani ccm taifa ndo wadhibiti wa bei?
   
 3. b

  bagain JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60  wadhibiti wa bei ni ewura kwa nijuavyo, lakini bei ya mafuta ya taa ilipandishwa wakati wa bajeti ya mwaka huu. Serikali ilipendekeza kupitia waziri wa fedha, wabunge nao wakaridhia. Baadae ccm wakaja na ushauri kwa serikali iangalie upya bei ya mafuta ya taa, lakini hadi leo mambo yanakwenda hivyohivyo tu.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  CCM ni chama cha siasa na mara nyingi matamko yake ni ya kisiasa zaidi... wanatafuta umaarufu wa kisiasa
   
 5. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hawashushi kwa sababu hakuna kati yao anae tumia mafuta taa, na kama yupo hiyo bei kwao ni ndogo mnoo kulinganisha na wao wananacho kipata...
   
Loading...