Swali kwa Ayubu Rioba: Siku hizi sera ya Taifa inaruhusu taasisi za kidini kunufaika na fedha za walipa kodi kupitia TBC?

Kimingi hakuna swali

Mimi hi mkristu, na nimestruggle Sana kuona swali liko wapi

Huwezi kuandika maelezo page tatu justifying what you want people to believe and expect it to be a question

You bias took you far down the road exposing your hatred and intolerance over other religions
I suggest that, you are troubled by gross incompetency that makes you unable to discuss the topic at hand.

You cant even differentiate between an argument and an arguer.

You better stay a spectator, if you don't mind.
 
Hoja ishakua MTU

Hata uandike kiyunani

Unless unapeactice zile test zenu za bar

Hakuna substance kabisa

Endelea kubishana
 
I suggest that, you are troubled by gross incompetency that makes you unable to discuss the topic at hand.

You cant even differentiate between an argument and an arguer.

You better stay a spectator, if you don't mind.
Zungumza kiswahili we mama.
 
Mbona hakuna kipindi cha Wahindu wanaomuabadu Krishna au Wahindi wanaoishi Tanzania sio raia halali?

Viwepo na Vipindi vya Washia,Wasunni, Waislamu wa Bakwata na wa Sheikh Ponda.

Viwepo vipindi vya Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Walutheri, Mashahidi wa Yehova, Gwajima, Mwamposya, Mzee wa Upako.

Kuwepo vipindi vya mabohora na wabahi pia.
Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.
Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana.
Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana.
Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.
Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki.
Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha.
Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.
Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi.
Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.
Vinginevyo TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi.
Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote.
Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.
 
..Mbona huku hoji haya hapo kabla..kwanini baada ya tangazo la mashindano ya kusoma qur'an tukufu? kwanini leo?
Tulia punguza mihemko soma tena. Kuna tofauti kati ya ibada na makongamano jamaa kaeleza vzr sana. Shida kuna watu ukigusa dini yao tu hata km una hoja ya msingi wao ni kujaa upepo tu!!
 
Wahindu wanaokwenda kwenye mahekalu kumuabudu Krishna kipindi chao kipo lini?
Wana TV zao hao kama ilivyo kwa shule, na wala siwaoni tukichangamana, binafsi huwa siwakumbuki kama tunao, Mkuu umeshaona tunaoleana na hao watu, oa uone chamtemakuni
 
Mbona hakuna kipindi cha Wahindu wanaomuabadu Krishna au Wahindi wanaoishi Tanzania sio raia halali?

Viwepo na Vipindi vya Washia,Wasunni, Waislamu wa Bakwata na wa Sheikh Ponda.

Viwepo vipindi vya Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Walutheri, Mashahidi wa Yehova, Gwajima, Mwamposya, Mzee wa Upako.

Kuwepo vipindi vya mabohora na wabahi pia.
Sunni, Shia na wengine wote ni waislam, wanasoma Qur'an moja.
Chochote kinachosemwa ni kwa niaba ya waislam wote.
Hivyo hivyo pia kwa wakristo, Biblia ni ile ile, ndiyo maana kwenye kipindi cha asubuhi au usiku tunawasikia viongozi wa madhehebu tofauti tofauti wakifikisha neno la Mungu.
Kuhusu wahindu, buddha nk, waombe TBC itawasikiliza.
 
Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.
Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana.
Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana.
Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.
Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki.
Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha.
Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.
Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi.
Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.
Vinginevyo TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi.
Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote.
Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.

Nakujibu kwa mtindo wa point counter point kama ifuatavyo:

Umesema: Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe. Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana. Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana. Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.

Jibu: Nimejieleza sana kwenye sehemu ya “mapingamizi tarajiwa" na majibu yake. Tunu ya uvumilivu haiwezi kutafsiriwa kuhalilisha kila kitu, kila mahali na kila wakati. Inayo mipaka. Mfano umesema, "wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana." Sioni kama unaelewa vema dhana ya uvumilivu. Huwezi kuingia msikitini ukasema "Yesu ni Mungu" halafu ukavumiliwa na Waislamu. Vivyo hivyo, huwezi kuingia Kanisani ukasema "Mtume Mohammed Ndio Njia Pekee ya Kwenda Kwa Mungu" halafu ukavumiliwa na Wakristo. Lakini ukisimama gulioni ukayasema hayo, unaweza kuvumilika. Soma eneo hilo la “mapingamizi tarajiwa" na majibu yake, halafu uje na mawzo ya maboresho ambayo ni specific. Ni baada ya hapo maneno haya yanaweza kuwa na maana inayojadilika: “Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.”

Umesema: Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki. Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha. Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.

Jibu: Unachokisema hapa ndio sababu ya baadhi ya watu kuukataa Uislamu. Kwa hiyo, kuuleta Uislamu kwa njia ya TBC, chombo cha wote, ni ubabe wa kidini. Vivyo hivyo, kuna sababu zinazowafanya Wakatoliki wasiwe Walutheri, au Walutheri wasiwe Waanglikana. Kutumia TBC, chombo cha umma wote kumlazimisha mtu kusikiliza mafundisho ya dini aliyoikataa tayari ni kukiuka katiba ya nchi kifungu kile cha uhuru wa kuabudu, ibara ya 19(1).

Umesema: Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi. Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.

Jibu: Kuhusu lugha nisema mawili. Mosi, ni suala la kitaaluma. Mwalimu yeyote anajua kuwa KUTAFSIRI ni mbinu mojawapo ya ualimu. Lakini kusoma kurani ya kiarabu kwa masaa sita mfululizo ni suala tofauti. Pili, sera ya Taifa ya lugha ya Kiswahili kama mbinu ya kujenga umoja wa kitaifa bado imesimama mpaka hapo itakapofutwa. Inapaswa kuheshimiwa na TBC. Na hilo ni jukumu la TBC kwa mujibu wa sheria ya Bunge iliyoianzisha.

Umesema: Vinginevyo TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi. Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote. Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.

Jibu: Hoja kwamba, utaratibu huu ubaki kama ulivyo kwa kuwa umetumika kwa miaka mingi haina mashika. Historia inasema kwa makabila ya WASEGEJU na WAZIMBA kwa miaka mingi walikuwa na utamaduni wa kula watu. Hiyo pekee haiwezi kuwa sababu ya kukubali utamaduni huo uendelee. Lazima hoja nzuri ijengwe. Hujajenga hoja nzuri bado kuonyesha ni kwa nini utaratibu wa sasa “Ubaki kama ulivyo”. Usisahau kuwa kuna walipa kodi wasio na dini, na hivyo wenye haki ya kuona kodi yao haitumiki kuwahudumia wenye dini.
 
Wewe kama huwakumbuki basi fahamu tunao, wapo watu weusi wameoa au kuolewa na wahindi, wanalipa kodi, wanatoa ajira na wameajiriwa pia hapa nchini. Upofu wako hawafanyi kuwa nusu Watanzania ni raia kamili wa nchi hii.
Wana TV zao hao kama ilivyo kwa shule, na wala siwaoni tukichangamana, binafsi huwa siwakumbuki kama tunao, Mkuu umeshaona tunaoleana na hao watu, oa uone chamtemakuni
 
Salamu Mpya ya Rais Samia ndio Mwarobaini wa tatizo la salamu za kidini kwenye matukio ya kiserikali.

Vipindi vya "inueni mioyo" na "Quran tukufu" kupitia TBC na RTD vimekuwapo muda mrefu, na vimeongezeka siku hizi.

Kwa hiyo hoja yangu inazo sababu za muda mrefu na sababu za karibuni.

Sasa nasema: Kwa kuwa Vipindi hivi vinavunja ibara ya 4(1) na 19(2) za Katiba ya Tanzania, basi ni batili.

Nataka tujisahihishe.
Tujisahihishe kwa utawala wa chama hikihiki chenye ukabila na udini ambao uko kama kinyonga? Kwa midomo hakuna udini wala ukabila ila kwa matendo vipo kwa juhudi na maarifa... labda huyu mama atafanikiwa kama sote tutamuunga mkono
 
Hiko kitabu ni uongo mtupu kama ilivyo Biblia hakina utukufu wowote
Edwayne, huo ni mjadala tofauti.

Anzisha bandiko jingine kama hautajali.

Hapa tujadili jambo moja tu: uvunjifu wa ibara ya 4(1), 19(1) na 19(2) za katiba ya Tanzania (1977)
 
Lakini si wanachukuliwa kodi zao hao watu wa dini?

Nashauri tufikiri pamoja kwa mujibu wa kanuni ya jurisprudence ifuatayo:
  1. Katiba inakataza tendo X;
  2. Kitendo hiki hapa Y ni sawa na kitendo X kinachokata zwa na katiba;
  3. Kwa hiyo, kitendo hiki Y ni batili kikatiba.
 
Nakujibu kwa mtindo wa point counter point kama ifuatavyo:

Umesema: Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe. Ni kweli kuna kupishana kwenye dini zetu, waislamu wataamini kile ambacho wakristo hawakiamini, hivyo pia wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana. Haya yasemwe kwenye vyombo kama hivi ili kuzidi kuimarisha tunu ya uvumilivu kwa kuwa hata mitaani tumechanganyika sana. Kufanya ibada hizi kwenye vyombo kama TBC kunawalazimisha watu kama wewe kuzoea maisha ya kuvumilia, hasa pale unaposikia mafundisho yanayoenda kinyume na imani yako.

Jibu: Nimejieleza sana kwenye sehemu ya “mapingamizi tarajiwa na majibu yake.” Tunu ya uvumilivu haiwezi kutafsiriwa kuhalilisha kila kitu, kila mahali na kila wakati. Inayo mipaka. Mfano umesema, "wakristo watasema Yesu ni Mungu, ingawa waislam hawaamini hilo, lakini wanalazimika kuvumiliana." Sioni kama unaelewa vema dhana ya uvumilivu. Huwezi kuingia msikitini ukasema "Yesu ni Mungu" halafu ukavumiliwa. Lakini ukisimama gulioni ukasema hivyo, utavumilika. Soma eneo hilo la “mapingamizi tarajiwa na majibu yake”, halafu uje na mawzo ya maboresho ambayo ni specific. Ni baada ya hapo maneno haya yanaweza kuwa na maana inayojadilika: “Utaratibu wa sasa ni mzuri kuliko unavyotaka iwe.”

Umesema: Kuhusu matumizi ya Lugha ya kiarabu kwenye kuendesha ibada za kiislam, hilo halikwepeki. Moja wapo ya msingi muhimu wa ibada za waislam ni lugha. Hakuna ibada kama haitumiki lugha ya kiarabu.

Jibu: Unachokisema hapa ndio sababu ya baadhi ya watu kuukataa Uislamu. Kwa hiyo, kuuleta Uislamu kwa njia ya TBC, chombo cha wote, ni ubabe wa kidini. Vivyo hivyo, kuna sababu zinazowafanya Wakatoliki wasiwe Walutheri, au Walutheri wasiwe Waanglikana. Kutumia TBC, chombo cha umma wote kumlazimisha mtu kusikiliza mafundisho ya dini aliyoikataa tayari ni kukiuka katiba ya nchi kifungu kile cha uhuru wa kuabudu, ibara ya 19(1).

Umesema: Madai ya kung'ang'ania Kiswahili pekee kwa sababu za kuimarisha umoja wetu hazina msingi. Ndiyo maana kuna wakati hata viongozi wanatumia lugha nyingine za kigeni au za makabila yao ili kufikisha ujumbe fasaha kwa wasilkilizaji.

Jibu: Kuhusu lugha nisema mawili. Mosi, ni suala la kitaaluma. Mwalimu yeyote anajua kuwa KUTAFSIRI ni mbinu mojawapo ya ualimu. Lakini kusoma kurani ya kiarabu kwa masaa sita mfululizo ni suala tofauti. Pili, sera ya Taifa ya lugha ya Kiswahili kama mbinu ya kujenga umoja wa kitaifa bado imesimama mpaka hapo itakapofutwa. Inapaswa kuheshimiwa na TBC. Na hilo ni jukumu la TBC kwa mujibu wa sheria ya Bunge iliyoianzisha.

Umesema: Vinginevyo TBC ni chombo cha walipa kodi wa Tanzania, ni haki yao kutumia chombo hicho bila kujali vyombo vingine ulivyotaja hata kama vitapewa masafa marefu zaidi. Utaratibu huu umetumika miaka mingi, umekubalika na pande zote. Ubaki kama ulivyo kwa afya ya umoja wetu.

Jibu: Hoja kwamba, utaratibu huu ubaki kama ulivyo kwa kuwa umetumika kwa miaka mingi haina mashika. Historia inasema kwa makabila ya WASEGEJU na WAZIMBA kwa miaka mingi walikuwa na utamaduni wa kula watu. Hiyo pekee haiwezi kuwa sababu ya kukubali utamaduni huo uendelee. Lazima hoja nzuri ijengwe. Hujajenga hoja nzuri bado kuonyesha ni kwa nini utaratibu wa sasa “Ubaki kama ulivyo”. Usisahau kuwa kuna walipa kodi wasio na dini, na hivyo wenye haki ya kuona kodi yao haitumiki kuwahudumia wenye dini.
Naona MTU anapractice sheria

Kazi IPO

Hasa ukiwa biased na extreme imani

Self righteousness haijawahi kuacha MTU salama

Be a learner maana hoja yako imeshakua MTU
 
Back
Top Bottom