Swali: Kuna mtu amewahi tumia chumvi ya mawe na ikamsaidia?

sontable

JF-Expert Member
Apr 13, 2018
262
528
Mapembelo!

Jamani katika pitapita humu mitandaoni nakutana na hoja mbalimbali kuhusiana na chumvi ya mawe kuwa inaweza kukusaidia kukufungua au kukuzuia usipatwe na madhara yatokanayo na nguvu za giza. Hivyo nilikuwa naomba kama mtu amewahi tumia hii mbinu na ikamsaidia na namna ya kuitumia

Swali ni je Kuna chumvi maalumu ya mawe au ni hii hii tunayoona sokoni na je Kuna dawa nyingine ya kuchanganyia au ni chumvi pekee na dozi yake ikoje

Mwenye majibu au ufahamu na Hilo anisaidie nitasoma kila comment

Mwalimi siso
 
Mkuu msingi wa tiba yeyote ya kiroho ni imani ,ukiwa na imani basi itakuponya kabisaaaa katika matatizo mbali mbali ,ila kama huna imani itakuwa shida ...

Chumvi ni silaha kubwa katika ulimwengu wa kiroho ,
Inaondoa nuksi mikosi na vifungo vya kichawi ,
Pia inasafisha mwili kwa kuondoa mapepo machafu yanayo kuzonga ,
Na pia chumvi inavuta ,mpenzi ama wateja ,
Na pia ni kinga kwa mambo mbali mbali ya kirohi
 
Hii chumvi ya mawe nilikiwa naiona tu nyumbani mfuko tele kadri siku zinavyozidi kwenda naona mfuko unapungua nikicheki jikoni naona chumvi ya unga ikisha inaagizwa nyingine sasa najiuliza chumvi ya mawe mbona haitumiki kwenye mboga alafu inaishaa kwa kasi. Baada ya kukumbana na nyuzi za mshana ndy nikaelewa matumiz yake.
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom