Swali: Kuna mtu amewahi tumia chumvi ya mawe na ikamsaidia?

sontable

JF-Expert Member
Apr 13, 2018
288
500
Mapembelo!

Jamani katika pitapita humu mitandaoni nakutana na hoja mbalimbali kuhusiana na chumvi ya mawe kuwa inaweza kukusaidia kukufungua au kukuzuia usipatwe na madhara yatokanayo na nguvu za giza. Hivyo nilikuwa naomba kama mtu amewahi tumia hii mbinu na ikamsaidia na namna ya kuitumia

Swali ni je Kuna chumvi maalumu ya mawe au ni hii hii tunayoona sokoni na je Kuna dawa nyingine ya kuchanganyia au ni chumvi pekee na dozi yake ikoje

Mwenye majibu au ufahamu na Hilo anisaidie nitasoma kila comment

Mwalimi siso
 

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,676
2,000
Mkuu msingi wa tiba yeyote ya kiroho ni imani ,ukiwa na imani basi itakuponya kabisaaaa katika matatizo mbali mbali ,ila kama huna imani itakuwa shida ...

Chumvi ni silaha kubwa katika ulimwengu wa kiroho ,
Inaondoa nuksi mikosi na vifungo vya kichawi ,
Pia inasafisha mwili kwa kuondoa mapepo machafu yanayo kuzonga ,
Na pia chumvi inavuta ,mpenzi ama wateja ,
Na pia ni kinga kwa mambo mbali mbali ya kirohi
 

zed B

JF-Expert Member
Jul 12, 2018
956
1,000
Hii chumvi ya mawe nilikiwa naiona tu nyumbani mfuko tele kadri siku zinavyozidi kwenda naona mfuko unapungua nikicheki jikoni naona chumvi ya unga ikisha inaagizwa nyingine sasa najiuliza chumvi ya mawe mbona haitumiki kwenye mboga alafu inaishaa kwa kasi. Baada ya kukumbana na nyuzi za mshana ndy nikaelewa matumiz yake.
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,520
2,000
Wewe tia chumvi baba, dunia ilishaharibika hii walozi wamekuwa wengi kuishi imekuwa kama mashindano, fuatilia na mafundisho ya kunyunyiza na kumwaga damu ya Yesu ya Mwl. Mwakasege kwa wale wakristo.....uswazi unaweza kushtukia hata misosi kama unga na mchele vinapungua kwa spidi ya 5G...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom