Swali: Kukubalika kwa Lema Arusha ni nguvu yake binafsi au nguvu ya chama?

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
633
Wakuu zimepita siku nyingi sasa hatujasikia habari mpya kutoka Arusha.
Mimi binafsi nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara Lema amekuwa akisumbuliwa na jeshi la polisi kwa lengo la kunyamazisha.
Swali: Je, nini watu wa Arusha wanapenda, ni Lema au CHADEMA? Je, kumnyamazisha Lema ndio kuwanyamazisha wana Arusha? Kwamba asipokuwepo Lema ndio utakuwa mwisho wa harakati Arusha?

Nawasilisha
 
Wakuu zimepita siku nyingi sasa hatujasikia habari mpya kutoka Arusha.Mimi binafsi nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara Lema amekuwa akisumbuliwa na jeshi la polisi kwa lengo la kunyamazisha.Swali: Je, nini watu wa Arusha wanapenda, ni Lema au CHADEMA? Je, kumnyamazisha Lema ndio kuwanyamazisha wana Arusha? Kwamba asipokuwepo Lema ndio utakuwa mwisho wa harakati Arusha?Nawasilisha
Wenye nguvu kuliko chama wako CCM akina Lowasa...
 
Wakuu zimepita siku nyingi sasa hatujasikia habari mpya kutoka Arusha.
Mimi binafsi nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara Lema amekuwa akisumbuliwa na jeshi la polisi kwa lengo la kunyamazisha.
Swali: Je, nini watu wa Arusha wanapenda, ni Lema au CHADEMA? Je, kumnyamazisha Lema ndio kuwanyamazisha wana Arusha? Kwamba asipokuwepo Lema ndio utakuwa mwisho wa harakati Arusha?

Nawasilisha

....kama unayohoja nyingine.
 
Chadema tu siyo Lema, kwa jinsi inavyijionyesha hapa ars cdm hata wakiweka jiwe litashinda
 
Wakuu zimepita siku nyingi sasa hatujasikia habari mpya kutoka Arusha.
Mimi binafsi nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara Lema amekuwa akisumbuliwa na jeshi la polisi kwa lengo la kunyamazisha.
Swali: Je, nini watu wa Arusha wanapenda, ni Lema au CHADEMA? Je, kumnyamazisha Lema ndio kuwanyamazisha wana Arusha? Kwamba asipokuwepo Lema ndio utakuwa mwisho wa harakati Arusha?

Nawasilisha

Wewe mbunge wa jimbo lako ni nani? Kabla ya kuskia ya arusha, hebu niambie habari mpya kotoka ktk jimbo lako kwanza.
 
Arusha hata kama kungsimamishwa mtu kutoka mirembe na yule mmama mzanzibar wa Magamba ageshinda chizi maana tumeishachoka na matusi ya CCM
 
Chadema inakubalika sana Arusha, wakati huo huo, Lema mjengaji mzuri sana wa hoja na nimesikiliza mara kadhaa oct 2010. my view.
 
Lema anakubalika binafsi kutokana na mchango wake katika harakati za kupigania ukombozi wa nchi hii si Arusha tu bali nchi nzima kwa ujumla.
Hivi majuzi aliswekwa lupango kupinga unyanyaswaji anaofanyiwa na polisi hasa mkuu wa polisi wilaya.

Tabia yake ya kutokuogopa na kusema kweli ndiyo inayompaisha hapo Arusha bila mashaka.
Lakini pamoja na yote hayo sikio halizi kichwa, kwa maana hiyo umaarufu wa G. Lema bado unapatikana chini ya viongozi imara, madhubuti toka ngazi ya juu unaofanya watu wakikibali CDM zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.
 
Mnaulizia kama vile hapa arusha ni hollywood vile??? Leteni habari za wabunge wa majimbo yenu ndo muulize habari za jimbo na mbunge wa jimbo ya wengine.

Hakuna haja ya kutaharuki bro. Sina nia mbaya Arusha na wala hakuna sababu ya kufanya hivyo.
Sina hakina kama umeisoma mistari yote na kuielewa. Mbona ni hoja ya kawaida tu hii. Ningeweza kusema hata Sugu from Hip hop to Parliament. Kimsingi hoja yangu ipo pale pale kwamba kitendo cha kumsumbua Lema pengine kwa nia ya kumnyamazisha, je ndio namna ya kuzima vuguvugu la harakati za wana Arusha? Kwa mantiki kwamba kama umaarufu wake unatokana na mwenyewe individually, then akinyamaza watu wate watanyamaza, ila kama wana Arusha wanapenda sera za CDM basi ni aluta continua.

Sasa sababu ya kuwa mkali hapa nini ndugu yangu!
 
Wakuu zimepita siku nyingi sasa hatujasikia habari mpya kutoka Arusha.
Mimi binafsi nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara Lema amekuwa akisumbuliwa na jeshi la polisi kwa lengo la kunyamazisha.
Swali: Je, nini watu wa Arusha wanapenda, ni Lema au CHADEMA? Je, kumnyamazisha Lema ndio kuwanyamazisha wana Arusha? Kwamba asipokuwepo Lema ndio utakuwa mwisho wa harakati Arusha?

Nawasilisha
Na mimi naomba unijibu swali hili kwamba...wanachama waliopo CCM ukiwepo wewe mwenyewe na jk,mnaogopa ccm au mnamwogopa Lowassa..!!??Jibu tafadhaliii..
 
Watanzania hawana muda wa kum-judge mtu, wanaangali chama.
 
Na mimi naomba unijibu swali hili kwamba...wanachama waliopo CCM ukiwepo wewe mwenyewe na jk,mnaogopa ccm au mnamwogopa Lowassa..!!??Jibu tafadhaliii..

Binafsi sina utamaduni wa kulumbana kwa vitu visivyo na msingi, sikupenda nikujibu hili swali lako.
Lakini kwa kuwa umeomba kujibiwa, basi mimi naanza hivi:
1.Kwa kuzingatia wachagiaji wengine hapo juu na heshima yangu kwao, nakushauri usome upya michango yao.
2.Kwa kuwa nimetoa ufafanuzi wakati ninamjibu DaudiMchambuzi, nakushauri usome tena upya pale.
3.Mimi si mwanachama wa chama chochote kwa kuwa ni hiari ya mtu kuwa mwanacha au kuacha, mimi nimeridhika kubaki kuwa mpiga kura wa kwawaida na huo ndio mchango wangu ktk demokrasia.

Ushauri wangu: Kama mtu unakuwa hujaelewa topic, bora ukapita tu kimya kimya kama wenzio.
 
Lema ana nafasi ya ushawishi Arusha na chadema pia,anajua kujenga hoja! ni kama mesi akiwa Barcelona na mesi akiwa argentina!
 
Back
Top Bottom