Swali kuhusu Chadema na Ushauri wa Mabere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kuhusu Chadema na Ushauri wa Mabere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabaDesi, Sep 8, 2010.

 1. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Chadema wamepigwa chini na Mkulu 'Tutendee' kwenye juhudi zao za kumuwekea pingamizi JK asigombee Uraisi.
  'Tutendee' amewaambia kuwa kama hawaridhiki na maamuzi yake wanaweza kwenda mbele.
  Chadema IMESHAURIWA na Mabere Marando kuwa isijisumbue kwenda mahakamani kwa vile itakuwa ni kupoteza muda.
  Chadema imekubali USHAURI wa Mabere kirahisiii na imesema badala yake itapelekea kesi yake kwenye Mahakama ya Wananchi Wapiga kura.
  Nauliza hivi:
  Hivi Chadema imewezaje kukubali ushauri huu wa mheshimiwa sana Mabere kirahiisi wa kuacha kwenda mahakamani kutafuta haki???
  Kwa nini Chadema wasiipeleke kesi hii mahakamani ili angalau ikawa inawasumbua tu jamaa???
  Kwani Chadema walikuwa na nini cha kupoteza kwa kuipeleka kesi hii mahakamani??

  Hiviii, wakati wa Vita si tunaambiwa ni vizuri tukatumia kila silaha tuliyo nayo ili hata kama hatumpigi adui basi angalau tunamu-unsettle ili angalau akose tu amani jamani??

  Hivi Chadema wanaweza kukubali kweli kirahiisi kukubali ushauri wa mheshimiwa Marando ambaye ameingia chama 'Juzi' tu kwa jambo muhimu kama hili???

  Kwa nini nisianze kuwaza kuwa Chama chetu Mkombozi hakichangi vizuri Karata zake????
   
 2. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni hivi. Prof. Baregu ameelezea kwa kirefu ushauri wa wanasheria. Ni kwamba rufaa hii itachukua muda mrefu hata mpaka baada ya uchaguzi 31 Oktoba 2010. Kwa sheria ya Uchaguzi Rais akishajulikana hakuna tena cha kumzuia mahakamani.
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa hapa mabere yuko sawa, unajua ukiipeleka mahakamani maana yake huna haki ya kuzungumza lolote hadi mahakama itoe hukumu, na kwa mtindo wa kimahakama it will take ttime may be mpaka uchaguzi umeisha na baadae pengine mshindwe (na nnaamini mtashindwa tu na ndio maana akaamua kuwashauri)

  tunawatakia kila la heri ktk kampeni
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi una taarifa ata Kesi za akina Chenge na Mramba zapigwa dana dana mpaka uchaguzi uishe
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  masuali ya sheria hayaingiliani na siasa acha uongo

  masuali ya sheria yana utaratibu wake na ndo maana kuna wakati mahakama inatoa maamuzi ambayo ni machungu kwa serikali na serikali haina budi kutagugumia
   
 6. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  labda pia inawezekana hakukuwa na strong arguments
   
 7. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ushauri ni mzuri sahihi na unatekelezeka. Kumbuka kila mtu alijua haki haitatendeka, ndivyo ilivyokuwa. Kuna mahakama inayotoa haki nayo ni ile ya wananchi kwa namna yo yote na ikifika hapo ni mwisho wa reli. Ndivyo Chadema inakusudia ifanyiwe. Tusubiri ndivyo itakavyokuwa
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Asante Mkuu Byasel kwa Ufafanuzi. Lakini Je Isingewezekana kusimamisha uchaguzi labda ili rufaa yao izungumzwe???
   
Loading...