MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kwa mara ya kwanza wakati mh JPM akihutubia bunge baada ya kuapishwa kua Rais wa JMT, ile hotuba ilisisimua taifa, watu walibubujikwa machozi kwa kudhani kua sasa taifa jipya linazaliwa, ilikua ni hotuba ya aina yake ambayo kwa kuisoma tu mtu unaweza kufikiria makubwa sana ambayo hayajawahi kutokea tokea nchi ipate Uhuru.
Lakini hivi sasa ni tofauti kabisa na matarajio ya wengi, ni taabu kwa makundi yote katika jamii.Maisha ndio yanazidi kua magumu hakuna hata matumaini ya kurejea kwa hali ya kawaida,hakuna awezaye kuitabiri hali yake ya maisha ya kesho.
Chaguzi ndogo za marudio juzi baadhi ya watu walihisi huenda ukawa ndio kipimo tosha kua CCM inapendwa sana,Lakini kwa werevu walipata kunena kua CCM hata ichukiwe na wanamchi wote wakiwemo makada wake haitoshindwa kutokana na kuwekeza kwa sehemu kubwa sana kwenye mamlaka za Tume ya Uchaguzi kuanzia mwenyekiti wa tume mpaka kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini.
Sababu ya alushindwa kwa CCM haitotengenezwa na kuchukiwa kwake na wananchi bali ni mamlaka za Uchaguzi kua huru. Huu ndio mzigo ambao wapinzani nchi wanao na huwezi kuukwepa.
Mpaka sasa hakuna jambo lililojaa utashi na kubeba ajenda kuu ya taifa ambalo wananchi wanaweza kushawishika kuipenda CCM na utawala wake.