Swali: Kama Mbowe na wenzake wamekutwa na kesi ya kujibu, nafasi ya kujitetea ni kuomba adhabu ipunguzwe?

Dr Restart

JF-Expert Member
Jul 15, 2021
3,257
16,999
Hili ni swali ambalo bila shaka sisi tusio na uelewa wa sheria kwa mapana yake tunajiuliza.

Katika hukumu iliyosomwa na Jaji Tiganga, mahakama imewakuta na kesi ya kujibu watuhumiwa wanne.

Maana yake ni kuwa hatia imeonekana. Je, wanapaswa kujitetea adhabu ipunguzwe ama wafutiwe makosa?

Je, DPP ana uwezo wa kuondoa shauri mahakamani ambalo tayari mahakama imewakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu?

Naomba kuelimishwa.
 
Jambo la muhimu kwa akina Kibatala kwa sasa, ni kuhakikisha wazee wa mchongo hawafanikiwi kuwatambua mashahidi wao kwa majina na anuani zao!

Yaani wakifanikiwa tu, basi wamekwisha!
 
Hawajakubali makosa.
Sasa wanatakiwa wajibu
Yaani wajitetee .
Sema urafiki wa mbowe kwa kamanda urio utamgharimu sana
Haya yote yasingetokea Kama asingejenga urafiki na huyo kamanda urio.
 
Ni utaratibu wa kawaida kabisa au ni sawa na kumpa haki mshtakiwa ya kusikilizwa na kuleta ushahidi wake against ushahidi na vielelezo vya upande wa mashtaka alafu mahakama itapitia utetezi wao na vielelezo vyao na kutoa hukumu (AMRI)
 
Ndio Hapo ndio atasema anamfahamu vipi urio,Kama alikuwa anawasiliana nae ,Kama alishawahi kumuita na kumtuma kazi,Kama alishawahi kumtumia hela n.k
Nilishasema hii kesi anayejua ukweli ni mbowe mwenyewe na kamanda urio.
Kama hayo mawasiliano waliyatengeneza ili ionekane mbowe anapanga mipango ya ugaidi.
Mbowe mwenyewe atasema
Wanasheria mtusaidie...... inamaana hapa Mbowe ndiyo anaanza kujibu hoja za mashahidi wa Jamhuri?
 
Ndio Hapo ndio atasema anamfahamu vipi urio,Kama alikuwa anawasiliana nae ,Kama alishawahi kumuita na kumtuma kazi,Kama alishawahi kumtumia hela n.k
Nilishasema hii kesi anayejua ukweli ni mbowe mwenyewe na kamanda urio.
Kama hayo mawasiliano waliyatengeneza ili ionekane mbowe anapanga mipango ya ugaidi.
Mbowe mwenyewe atasema
Okay, nimekuelewa vizuri mkuu
 
Hili ni swali ambalo bila shaka sisi tusio na uelewa wa sheria kwa mapana yake tunajiuliza.

Katika hukumu iliyosomwa na Jaji Tiganga, mahakama imewakuta na kesi ya kujibu watuhumiwa wanne.

Maana yake ni kuwa hatia imeonekana. Je, wanapaswa kujitetea adhabu ipunguzwe ama wafutiwe makosa?

Je, DPP ana uwezo wa kuondoa shauri mahakamani ambalo tayari mahakama imewakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu?

Naomba kuelimishwa.
Kukutwa na kesi ya kujibu si kwamba umekutwa na hatia.Bali Jaji ameona kwamba kulikuwa na sababu za kuonesha kwamba sheria ilivunjwa.Sio GUILD VERDICT.Guilt verdict inafikiwa baada ya utetezi kuleta HOJA zao pamoja mashahidi wao ili kuthibitisha innocense yao.katika hatua hii DPP anaweza kuleta ombi la kutokutaka kuendelea na kesi(Sijajua athari ya kisheria ikoje na kanuni ziansemaje ila wajuzi wataongezea(Mimi sio DPP wala wakili) na nafikiri hili linaweza kutokea hasa kwa kuzingatia kwamba wangefanya hivyo kabla ya huu uamuzi wangekuwa wamekimbia kesi ila katika hatua hii tayari wameshajenga HOJA kwamba kesi yao sio ya kubumba mbele ya macho ya sheria.
 
Back
Top Bottom