Swali: Kama baba yangu mzungu mama yangu mbantu, kwa nini iwe halali kuitwa black na sio white? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali: Kama baba yangu mzungu mama yangu mbantu, kwa nini iwe halali kuitwa black na sio white?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Synthesizer, Jul 18, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Ubaguzi wa rangi ni jambo linalochukiwa na wengi wa watu walio na akili timamu. Hata hivyo, katika nyanja nyingi linahalalishwa bila wengi wetu kuelewa. Kwa mfano, kwa nini Obama anasemwa kuwa raisi wa kwanza "black" wa Marekani wakati mama yake ni mzungu na baba yake mbantu? Kama ni halali Obama kujiita "black" kwa nini si halali yeye kujiita "white" wakati uzaliwa wake ni kwa ratio ya 50:50 black and white?

  Nimeshashuhudia watu wakibeza pale mtu mchanganyiko wa mzungu na mbantu anaposema yeye ni mzungu. Kwa nini sio mzungu na bali ni "black"?

  Kwa maoni yangu bado Marekani haijawa na raisi "black". Obama ni raisi "coloured" wa kwanza Marekani. Kumuita Obama "black" ni kuaendeleza kanuni ya Amerika ya Kusini iliyokuwa imezama katika kutumia watu weusi kama watumwa, ambapo ili uwe white lazima usiwe na hata chembe ya ubantu katika ukoo wako.
   
 2. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wewe nawe unaonekana ni racist pia. Unataka aitwe mzungu kwa kuwa we ni mwaffrika na mzungu anataka aitwe mwafrika so nyote ni sawa. Asiyejari ubaguzi hatajari kuitwa black or white. Ubaguzi uko ubongoni mwa mtu. Kama Obama ni mzungu poa kama ni mwafrika poa ukweli unabaki palepale kuwa ni rais wa Marekana
   
 3. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Invarbrass, si kwamba sipendi Obama aitwe "black". Bali sipendi uhalalishaji (social endorsement/acceptance) kwamba Obama sio "white", wakati inahalalishwa kwamba yeye ni "black". Sijui kama unanielewa.
   
 4. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Synthesizer,nakuelewa mkuu. White/black na coloured zote ni lebo ambazo interpretation yake inabeba ama inferiority au seperiority feelings. Mhusiks anabaki kama alivo. Unajua racism is a very strange concept kwa sababu hakuna anayeweza kujitambua kuwa ni racist inagundulika katika jitihada zetu za kukataa au kutoa lebo kwa wenzetu. Ni hisia kuwa naonekana sifai au kumuona mwenzako hafai. Kwa hiyo unakuwa racist free kama hupati negative feelings unapoitwa black,jew, coloured. mzungu, mhindi, mwafrika na kadharika. Jaribu kuwa neutral kidogo then cast doubts hata kwa waafrika wenyewe utakuja kushangaa utakapogundua waafrika tuko rasist kuliko tunavyodhani. Mfano unajisikiaje majibu ya maswali yafatuatayo yakiwa ndio; 1. Kutawaliwa na rais mhindi(mtanzania mwenye asili ya kiasia) 2. Je. unaweza kumpa kura mhindi uka mwacha mwafrika kama mbunge wako endapo wagombea watakuwa hao na wanasifa wote except their race? Je ni wangapi wangetoa majibu ya ndio kwa maswali haya machache tu? Tujadili ndugu yangu mi natoa changa moto wala sikulaumu wewe maana nami huwa nadondokea mtego huohuo make sie ni wanadamu. usifunge mjadala>
   
 5. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Invarbrass, umeongea mambo muhimu sana. Nakumbuka hata niliwahi kuulizwa maswali juu ya ubaguzi katika jamii juu ya ndoa kati ya kabila na kabila au kati ya race na race; reaction gani unapata mwanao anaposema anaoa au kuolewa na kabila fulani, au race fulani kama mwarabu, mhindi, mzungu nk. Nikaambiwa hiyo pia ni kipimo kizuri cha kujijua uko katika ubaguzi.

  Lakini kitu ambacho kinawavutia wengi ni mabadiliko katika nchi kama ya Afrika Kusini ambako weusi walipigana vita dhidi ya ubaguzi uliokuwa ukifanywa na wazungu dhidi ya weusi, coloureds, wachina na wahindi. Wengi hata wamejiuliza kama utawala wa sasa wa weusi nchini Afrika Kusini ni wa Kibaguzi, kwa kuwa haujaweka mazingira yanayokubalika kwa mzungu, coloured, mchina au mhindi mzalendo kuwa raisi wa nchi, hata kama anaonekana ni kiongozi bora kiasi gani. Kuna waziri wao wa fedha anaitwa Trevor Manuel ambaye alionekana kuwa kiongozi makini sana, hata zaidi sana ya Zuma, na walikuwa wanataka sana awe raisi wa benki ya dunia, lakini hawakuwa tayari katakata awe raisi wa Afrika Kusini kwa sababu tu yeye ni coloured. Wanaona haikubaliki kuwa na raisi asiye mbantu baada ya kuwa wameshinda vita ya ubaguzi!

  Kwa hiyo nakubaliana na wewe kwamba at the end of the day wengi wetu ni wabaguzi bila kujua, tukidhani ubaguzi ni ule tu unaofanywa na mzungu dhidi ya mtu asiye mzungu!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Unatakiwa ujivunie kwa hilo.......maana yake ni kwamba Rangi nyeusi ni nzito kuliko nyeupe........na ina thamani
   
 7. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli na ndo maana wanaopigania ubaguzi wa wengi hupata zawadi za nobel kwa kuwa ni vigumu kuupinga ubaguzi. NA wakati huo huo ni ugonjwa mbaya sana kwa kuwa ki ubinadamu hakuna uwezekano wa kupata element inayopendwa na wabaguzi (mfano mwafirika kuwa mzungu) na hakuna uwezekano wa mtu kuondoa element isiyotakiwa (mfano mhindi kuufuta uhindi) sasa kwa kuweka qualification ambazo ni that natural katika kuamua mustakabali wa maisha ya mtu katika jamii ni uonevu mkubwa sana. SO tuupige vita ubaguzi kwa concept ya Mwenzetu MICHAEL JACKSON ya changes begining with a man in the mirror. Tusikate tamaa Synthesizer tu synthesise hii hali mpaka tufikie synthesis
   
 8. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Safari-n-safari I like your signature as it is translated.
   
 9. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Sio kila Race ni sawa Black is the Original Race na Race nyingine zimetokana na Black miaka ya nyuma. Sasa kama ukichanganya damu na Mbantu mtoto atatokea mbantu mwenye labda nyele tofauti na vitu vingine lakini atakuwa mbamtu. Hivyo ukichanganya na Black sio kweli kwamba uko 50/50 kama unavyosema hapa. Genetics za binadamu haziendi kwa nusu nusu kama hesabu.
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mixed race ya black n white mara nyingi unakuta mtoto anakua anafanana zaidi na mweusi kuliko mweupe japokua kuna mixed race zingine inatokea mtoto anakua mzungu kabisa mfano kwa wanaomjua mariah carey wengi wanadhani ni mzungu coz anafanana kabisa na yuko kama mzungu lakini kumbe yuko mixed... Bt majority ya mixed race they tend to lean more kwenye uweusi ndo maana wanabagulia.. Obama ukimuangalia mweusi kabisa lakini ana mama mzungu...
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Namtafuta Kiranga,yuko wapi?Hili li thread linahitaji mawazo yake. . . . . .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Huu nao ni ubaguzi . . . . . . .Lakini hata mimi nimeitazama post hii kiubaguzibaguzi hivi!
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Ubaguzi wa rangi ni ujinga wa hali ya juu sana.Lakini tafsiri yake ni ngumu,ni ngumu kwa sababu wote sisi ni wabaguzi,hivyo tafsiri utakayoitoa itakulinda tu,tayari unakua mbaguzi tena!
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Nipo,

  Mshataka kunifanya resident sage siyo? Humbled!

  Mawazo yangu mie ni kwamba "uhalali" huu unatoka wapi?

  Brazil mpaka leo mtu wa mixed race anakuwa considered "mulatto", si black wala white.

  Hizi habari za mtu wa mixed race kuwa considered black zina mizizi katika racist Europe/ Aryan movement/ Nazism, utumwa wa Marekani, Ku Klux Klan na wazungu wabaguzi waliotaka ku maintain racial purity kwa kanuni ya kwamba "ukiwa na tone moja tu la mtu mweusi basi na wewe ni mweusi".

  Kisayansi DNA ya mtu mweusi na ya mtu mweupe hazina tofauti, na tofauti inaishia kwenye ngozi. Kwa hiyo mtu mweupe, mweusi, mixed, wote kimsingi ni watu wenye tofauti za rangi tu, zaidi ya hapo hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba kuna tofauti ya kina.
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Bravo Kiranga,sasa inaonekana wanadamu tuna upofu mkubwa wa kutokujitambua japokua sayansi inatupa majibu ambayo ni kinyume na namna tunavyotaka iwe.Inaonekana rangi ya ngozi inakuwa tofauti kwa sababu za kimazingira zaidi.Halafu huo "uhalali" wenyewe tunaupata kwa misingi ile ile ya kibaguzi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kisayansi Obama ni shombe.
   
Loading...