Swali: Jee Spika Anayo Mamlaka Kuzuia Muongozo wa Spika au ni Udikteta Tuu?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali: Jee Spika Anayo Mamlaka Kuzuia Muongozo wa Spika au ni Udikteta Tuu?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 19, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,631
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Mimi ni mfuatiliaji wa vikao vya bunge letu tukufu kwa kufuatilia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kupitia TV na mara moja moja nipatapo nafasi, hutinga kabisa katika viwanja vya bunge.

  Nijua mimi, uendeshaji wa vikao vya bunge, unatawaliwa na taratibu, sheria na kanuni, lakini tangu spika wa sasa, Mhe. Anna Makinda, aushike uspika, kumekuwa kukitokea mivurugano ya hapa na pale kuhusiana na uendeshaji wa bunge letu.

  Mfano hai ni tukio lililotokea leo asubuhi bungeni mjini Dodoma, mara baada ya kipindi cha maswali ya moja kwa moja kwa waziri mkuu, kuna mbunge alisimama kuomba muongozo wa spika.

  Mhe. Makinda alikataa kuusikiliza hoja ya muongozo huo na kudai, ili kuutumia muda vizuri, hakuna muda wa kusikiliza miongozo sasa mpaka wakati mwingine, hii ikiwa ina canotation meaning kuwa muongozo uliotakwa kuombwa, ni "wastage of time", hivyo spika ameupuuza ilikuutumia muda wake vizuri!.

  Kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya Kanuni za Bunge mwaka 2007, inatoa maelekezo jinsi spika atakaliendesha bunge

  8. Kwa kuzingatia matakwa na masharti yaliyowekwa na kiapo
  cha kazi zake na kwa madhumuni ya utoaji wa maamuzi na
  uendeshaji wa Shughuli za Bunge kwa haki na bila upendeleo, Spika:-
  (a) Ataendesha shughuli za Bunge na kutoa
  maamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala
  upendeleo wowote, kwa kuongozwa na Katiba,
  Sheria za nchi, Kanuni hizi, Kanuni nyingine
  zilizopo, maamuzi ya maspika wa Bunge
  waliotangulia na pia kwa kuzingatia uzoefu
  pamoja na mila na desturi za mabunge mengine
  yanayofuata utaratibu wa kibunge
  unaofanana na unaofuatwa na Bunge la Tanzania;
  (b) Hatafungwa na msimamo utakaowekwa au
  makubaliano yatakayofikiwa na Kamati yoyote
  ya Chama cha Siasa kinachowakilishwa Bungeni.

  Nauliza Jee ni kweli spika wetu, analiendesha bunge bila upendeleo?.


  Ibara ya 68

  68.-(1) Mbunge anaweza kusimama wakati wowote na kusema
  maneno "kuhusu utaratibu", ambapo Mbunge yeyote ambaye
  wakati huo atakuwa anasema atanyamaza na kukaa chini na Spika
  atamtaka Mbunge aliyedai utaratibu ataje Kanuni au sehemu ya
  Kanuni iliyokiukwa.
  Taarifa kuhusu utaratibu na Mwongozo
  (2) Mbunge aliyedai utaratibu atalazimika kutaja Kanuni au sehemu
  ya Kanuni ya Bunge iliyokiukwa.
  (3) Baada ya kutaja Kanuni au sehemu ya Kanuni ya Bunge
  iliyokiukwa Mbunge aliyesimama kuhusu utaratibu, ataketi mahali
  pake kusubiri maelekezo na uamuzi wa Spika.
  (4) Spika anaweza, ama papo hapo kutoa uamuzi wake juu ya
  jambo la utaratibu lililotajwa au kuahirisha uamuzi ili alifikirie zaidi
  jambo hilo na kutoa uamuzi baadaye au kutoa uamuzi na baadaye
  kutoa sababu za uamuzi huo, vyovyote atakavyoamua.


  (7) Hali kadhalika, Mbunge anaweza kusimama wakati wowote
  ambapo hakuna Mbunge mwingine anayesema na kuomba
  "Mwongozo wa Spika" kuhusu jambo ambalo limetokea Bungeni
  mapema, ili Spika atoe ufafanuzi kama jambo hilo linaruhusiwa au
  haliruhusiwi kwa mujibu wa Kanuni na taratibu za Bunge na majibu
  ya Spika yatatolewa papo hapo au baadaye, kadri atakavyoona
  inafaa.

  Jee inawezekana Spika, Mhe. Anne Makinda, anauwezo mkubwa kabisa wa viwango vya mind reading, telepathy, precogninition na intuition kwa kusoma swali la muongozo ulioombwa na kuujua ni wastage of time na hivyo kuutupilia mbali muongozo uliiombwa bila hata kuusikiliza ili "kuutumia muda wa bunge vizuri?!.

  Kanuni zinamtaka spika kutoa maamuzi ya papo kwa papo, au baadae, lakini Spika Makinda, amemkabidhi naibu spika bila kutoa fursa ya kusikiliza muongozo wa spika ulioombwa mapema!.

  Hivi hivi vichwa tele vya kutumainiwa vilivyoko bungeni, vina sababu yoyote ya kumuachia Spika Makinda, kujiendeshea bunge yeye anavyoona inafaa hata kama ni ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni?!.

  Pasco.
   
 2. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  well said..
   
 3. i

  iseesa JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni Spika Mwoga, Asiyejiamini na "Partisan" kwa sababu huikatalia zaidi Miongozo inayoombwa na wapinzani wa CCM au wapinzani ndani ya CCM. Si ilisemekana kuwa aliwekwa na Mafisadi?
   
 4. maphie

  maphie Senior Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hatuna spika, tuna kiranja
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,873
  Trophy Points: 280
  Mkuu lakini hata huyo kiranja kama hafai si tunampiga chini kwa nini tuendelee kuvumilia ujinga? Hakuna mahali ambapo wabunge wanaweza kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye?
   
Loading...