Swali je unajua uchemshaji bora wa mayai?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
10665944_291784751030242_7052493680325281164_n.jpg
14953_291784887696895_7425109999600428084_n.jpg
10672375_291784921030225_681405288880103053_n.jpg
10696352_291784994363551_62684683227817185_n.jpg

Yai la kuku utalichemsha kwa dakika ngapi.png

Tunapozungumzia kula kuku kwa ajili ya Afya zetu tunazungumzia kuku wetu wa kiasili au tunapozungumzia umuhimu wa kula mayai zaidi tunakusudia mayai bora ya kuku wetu wa Asili na mapishi yenye ubora zaidi ktk màyai si kuyakaanga bora zaidi ni kwa kuxhemsha na ukihitaji kukaanga basi si kwa mafuta mengi na pendelea

mafuta asili mimi binafsi huwa natumia mafuta ya mzaituni kwani mzaituni una kawaida ya kuua sumusumu ktk vyakula vilivyopitiwa na hizo sumu

SWALI JE UNAJUA UCHEMSHAJI BORA WA MAYAI ?

Leo nitakujuza vizuri.
Ili kuchemsha mayai vizuri
fuata maelezo yafatayo:

1.weka mayai kwenye sufuria kisha
ongeza maji adi yafunike
mayai,yazidi mayai kwa inchi moja
(1inch). hakikisha ni maji baridi ya
kawaida.Ukianza kuchemsha mayai
na maji ya moto ni lazima mayai
hayo yapasuke.

2.Ongeza nusu kijiko cha chai cha
Baking soda au zaidi kutokana na
wingi wa mayai.watu wengine
hutumia chumvi badala ya baking
soda.ni vyema kujua kwamba
baking soda hufanya kazi vizuri
zaidi kuliko chumvi.
Baking soda huraisisha
kumenya,husaidia ganda la
yai kubanduka kirahisi.

3.Bandika sufuria hilo jikoni na
uchemshe mayai kwa kati ya
dakika tano .chemsha mayai
kwa moto kwa wastani,moto mkali
sana husababisha mayai kupasuka

4.Mayai yakiiva tu,toa mayai
kwenye maji ya moto na kisha
yatumbukize kwenye maji ya
baridi,maji baridi yenye barafu
yanafaa zaidi,acha kwa dakika tano
au zaidi ili mayai yapo.
Hii husaidia selii na kuta za
yai kushikana vizuri na
kufanya kazi ya kumenya
kuwa rahisi

5.Toa mayai kwenye maji
baridi,weka kwenye taulo ili
kukausha .

6.Gonga sehem ya juu/kichwa cha
yai taratibu ili kuvunja gamba la
yai,menya yai hilo.
Mpaka hapa mayai tayari kabisa
kwa kula au kutengenezea chakula

kingine.
 
Wakuu mayai yangu matatu yananiuma.
Nimechemsha yamepasukiamo. Halafu nayamenya yapo tepetepe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom