Swali:Je Prof Kabudi amefit kwenye nafasi aliyonayo?

Gemini6

Senior Member
Jun 21, 2017
153
250
Wakuu salam,ama baada ya salam mi mgeni humu,ila nawaulizeni jinsi waziri wetu wa sheria anavyojibu maswali bila mihemko wala jazba.Je nini aongeze ama apunguze ili ajitofautishe na watangulizi wake? Ni hilo tuu!
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,503
2,000
Natamani waandishi wa habari wamuulize huyu Kabudi na mwenzake Polepole wanasemaje juu ya Katiba ya Warioba yaliyoililia mchana na usiku hasa baada ya CCM kuitupa jalalani na kumtuma Chenge atuandikie Katiba anayofikiri inawafaa watanzania. na kweli Chenge akaandika, eti ndo tunaisubiri tuipigie kura kuahalalisha. Mungu iokoe Tanzania. Ooh! Lord, save us from this Vampire, namely Chama Cha Makinikia (CCM).
 

G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,752
2,000
Anaweza kuwa mzuri tu kama hatokuwa tayari kupokea maagizo kutoka juu,otherwise his performance won't be all that good
Duniani hakuna mtu yeyote yule anayeongozwa ambaye hapokei maagizo kutoka juu....hata wewe kuna vitu ambvyo unafanya kulingana na mkuu wako ambaye yuko juu yako kma umeajiliwa.
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Nilimuona juzi bungeni anacheka tu! Pale spika anaposema eti kama Wabunge wa upinzani wanasema hapana kwenye bajeti basi wasipewe fedha za maendeleo!

Nilitegemea kwa gwiji kama yeye angeomba mwongozo kwa spika kutoa somo murua kabisa kama kisheria imekaaje!

matokeo yake wanawaachia wanawake kama jenister muhagama ambaye unaona kabisa hajui chochote
 
  • Thanks
Reactions: SDG

Konsciouz

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,827
2,000
Huyu jamaa ni mnafiki tu kama walivyo ccm wengine.
Ni mtu mwenye dharau sana mwenye kujikuta mjuaji.
Na kikawaida mtu ambaye alikua anaona hii ni NYEKUNDU lakini akipata ulaji hiyo NYEKUNDU akaanza kuiita NYEUPE huyo mtu anakua amefeli moja kwa moja.

Huyu mzee ni FALA.
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,037
2,000
Kwa kifupi anafuata muelekeo wa mtangulizi wake, Siasa haswa za CCM zinaua sana ubora utaalam wa wataalaam wetu hawa.
 

Gemini6

Senior Member
Jun 21, 2017
153
250
Mimi sio mdau wa siasa ila nikimwangalia jamaa,nice kama anajiamini kdg kwa nafasi yake,tofauti na yule mtangulizi wake aliyekana dissertation yake ya phd
 

ALF

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
208
250
Ameshaingia kwenye siasa chochote kinaweza kutokea
Ameanza kubadilika, nilisikitika sana siku watu walipokumbushia swala la KATIBA MPYA, kwenye maelezo yake akasema hakuna umuhimu wa katiba akasema katiba inaandikwa moyoni sio kwenye makaratasi, akaendelea kuna nchi hazina katiba ilioandikwa kama Uingereza, Israel nk na mambo yanakwenda vizuri. Tumuache rahisi afanye kazi na tusimiungilie.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
73,378
2,000
Wakuu salam,ama baada ya salam mi mgeni humu,ila nawaulizeni jinsi waziri wetu wa sheria anavyojibu maswali bila mihemko wala jazba.Je nini aongeze ama apunguze ili ajitofautishe na watangulizi wake? Ni hilo tuu!
Hana ujanja wowote , ni lazima atii maagizo ya aliyemtuma tu , ukiingia ccm akili yako unaiacha mlangoni .

Sema Tundu Lissu atamnyoosha .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom