SWALI: Hivi sheria ya NEC inasemaje kama mgombea mmoja akishindwa kuendelea na kampeni

Emmadogo

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
4,126
3,751
Je hicho chama kinaruhusiwa kuleta mtu mwingine?
Je uchaguzi utaahirishwa?
Je uchaguzi utaendelea sababu mda wa kuchukua form na kurudisha utakuwa umeisha?
Au watabadili sheria kama itakuwa ni mtu wa chama kilichopo madarakani.Maana hapo si itakuwa ni kama washapoteza uchaguzi

Naomba ambao wanaijua sheria ya uchaguzi

NB: Sina nia yoyote ya kumdhuru mgombea yoyote. Maana kuna wengine hawachelewi
 
Kwa anayejua kuhusu hili atusaidie tafadhali maana Lumumba hali si shwari.
 
Akisemacho mtu ndicho kilichojaa moyoni mwake acha kuwaza mabaya juu ya binadamu mwenzio
 
Mgombea Akifariki Uchaguzi Unahairishwa.Akisimamisha Mwenyewe Kampeni Au Kuacha Kupga Kampeni Uchaguz Unaendelea Kama Kawaida.Mpaka Anasimamisha Kufanya Kampeni Inamaana Had Chama Wamekubaliana.
 
Kuahirishwa kwa tarehe ya uchaguzi ni kutokana na sababu mbili tu;

1. Kifo cha mgombea mwenyewe wa Urais au mgombea mwenza wake. Hii ilitokea katika uchaguzi wa mwaka 2005 pale mgombea mwenza wa Freeman A. Mbowe wa CHADEMA toka Zanzibar (simkumbuki jina) alipofariki katikati ya harakati za Kampeni.

Uchaguzi ulisukumwa mbele kwa mwezi mmoja zaidi ili kuwapa fursa CHADEMA kufanya mchakato upya wa uteuzi wa mgombea mwenza wao. Anna Komu aliteuliwa kuziba nafasi hiyo.

2. Iwapo mgombea wa Urais au mgombea mwenza kutoka chama chochote vinavyoshiriki uchaguzi itathibitibitika pasipo shaka yoyote chini ya jopo la madaktari wasiopungua watano kuwa ni mgonjwa na afya yake haiwezi kumruhusu kuendelea na mchakato wa uchaguzi, basi Tume ya uchaguzi baada ya chama husika kutoa taarifa, haitakuwa na option nyingine zaidi ya kutangaza tarehe nyingine ya mbele ya uchaguzi ili kuruhusu chama hicho kuteua mgombea mwingine kujaza nafasi hiyo.

Mfano wa magonjwa hayo ni yale yanayosababishwa na ajali kunakopelekea muhusika kupooza na kulazwa hospitali kwa muda unaozidi mwezi mmoja hata kuathiri kampeni zake na chama chake

Huu ndiyo ufahamu wangu, naweza kusahihishwa nilipokosea na au kama kuna sababu nyingine niliyoisahau, ikaongezwa!

Demokrasia wakati mwingine ina gharama zake na ni kama hii.

Chukulia mfano mgombea wa chama kama CHAUMA ambaye hana impact yoyote ktk uchaguzi huu ndo akapatwa na moja ya janga hapo juu. Kutakuwa hakuna way out zaidi ya sheria ya uchaguzi kushika mkondo wake!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom