Swali: Hivi nini kitafuata baada ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa na wabunge wa CCM tu?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,693
36,062
Habari waungwana,

Huhitaji kuwa na Degree ya Political Science kuamini hili. Kwa hakika kabisa majimbo yote Tanzania bara yanakwenda kuchukuliwa na CCM kwa gharama yoyote. Ninaposema kwa gharama yoyote nadhani mmenielewa.

Labda tu Rais kwa sababu zake yeye mwenyewe aamue kuchagua baadhi ya watu kutoka upinzani wenye misimamo vuguvugu na kuwaongeza bungeni ili kuleta picha kimataifa kuwa bunge limeundwa na watu wa vyama tofauti.

Hao wote watakaokuwa bungeni Mimi nitawaita wanaCCM.

Je, bunge likiwa na wabunge wa CCM pekee mwanachi atapata faida gani? Nini kitafuata baadaye?
 
CCM watafurahia sana; wapigaji timu jiwe watafurahi na kushangilia sana. Sekta binafsi itazidi kufa kabisa, style ya kunyoa nywele itategemea Makonda na Rais wamenyoaje nywele.
 
CCM watafurahia sana; wapigaji timu jiwe watafurahi na kushangilia sana. Sekta binafsi itazidi kufa kabisa, style ya kunyoa nywele itategemea Makonda na Rais wamenyoaje nywele.
Ngoja tusubiri wengine watoe mawazo yao
 
Usijidanganye mkuu hizo ni propaganda tu,nakuambia kwamba 2020 CDM itavuna wabunge wengi sana,hivi unaweza kweli kumnyang'anya SUGU,HECHE,LEMA,MSIGWA etc UBUNGE wake kwa kutumia MTUTU?

Kama wapinzani wakishinda kwenye BOX la kura lazima watatangazwa otherwise wataleta "MASAKA"(MASSACRE)!!! Usijidanganye na Kafulila alivyonyang'anywa UBUNGE wale waliwekwa chini tu wakayamaliza na ndio maana alitulia tuli huku akila MITONYO na baadae akapewa UKATIBU TARAFA(DAS,RAS etc).
 
Nch yetu itakua imepiga hatua kubwa kwa kuwamaliza mamluki wa mabeberu Tena naomba mungu uchaguz ufanyije msimu huu wa Corona ili ukishindwa alafu ukaleta vurugu. Unasweka ndan Tena tuna kuchanganya na mgonjwa wa Corona ili upate adabu
 
Sasa si ndo patakuwa patamu kabisa hapo. Waingie wote CCM uone huo mtiti wake, utakuwa siyo wa kitoto.

Maana tutararuana wenyewe kwa wenyewe. Sasa hv tunakuwa wamoja kwa sababu kuna safu ya upinzani..

Kwa hiyo msiogope sisi CCM hata tukiingia kama woote ndo tutapata nafasi nzuri ya kuisimamia serikali. Otherwise 2025 tutawaambia nn watanzania?

CCM HOYEEE!!! JPM SAFIII!!!
 
Nch yetu itakua imepiga hatua kubwa kwa kuwamaliza mamluki wa mabeberu Tena naomba mungu uchaguz ufanyije msimu huu wa Corona ili ukishindwa alafu ukaleta vurugu. Unasweka ndan Tena tuna kuchanganya na mgonjwa wa Corona ili upate adabu

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu CCM hatuna roho mbaya hivyo ya uuaji, utakuwa mamluki wewe unataka tu kutuchonganisha na wananchi.
 
Usijidanganye mkuu hizo ni propaganda tu,nakuambia kwamba 2020 CDM itavuna wabunge wengi sana,hivi unaweza kweli kumnyang'anya SUGU,HECHE,LEMA,MSIGWA etc UBUNGE wake kwa kutumia MTUTU?

Kama wapinzani wakishinda kwenye BOX la kura lazima watatangazwa otherwise wataleta "MASAKA"(MASSACRE)!!! Usijidanganye na Kafulila alivyonyang'anywa UBUNGE wale waliwekwa chini tu wakayamaliza na ndio maana alitulia tuli huku akila MITONYO na baadae akapewa UKATIBU TARAFA(DAS,RAS etc).
Nipe tafsiri ya uchaguzi wa serikali za mitaa?
Mpinzani yupi alileta massacre?.
Kwenye maandishi yangu nimesema neno " Kwa gharama yoyote CCM itachukua majimbo yote" .
Kama upinzani ulipigwa chenga ya kitoto kwenye local government election 2019, watathubutu vipi kutegua mtego wenye ulaji zaidi kwa CCM wa majimbo na kiti cha urais
 
Subiri ikifika tusiandikie mate,uchafuzi wa serikali za mitaa hakuna aliyeangaika nao,ngoja uchaguzi mkuu ndio utajua.
 
Ngoja tusubiri wengine watoe mawazo yao

Wabunge wengi wa CCM hawana msaada bungeni wapo kuchukua posho na kuunga mkono hoja...

Sheria za ovyo zitapitishwa na bunge ili kuwafurahisha watawala na kuzidi kuwaumiza raia... Na hapo ndio mwisho wa CCM utakuwa umeshafika...
 
Back
Top Bottom