Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu?!. (Ufuatiliaji Muungano Sehemu ya I)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,

Wakati tukiendelea na mjadala wa serikali 3 kuelekea kwenye katiba mpya, uoga mkuu kuhusu uwepo wa serikali 3, ni tishio la serikali tatu kuudhoofisha muungano hatimaye kurisk kuuvunja!. Watanzania bado hatujaruhusiwa kuhoji au kujadili kuhusu uhalali wa uwepo wa muungano kisheria, this is still it's a toboo topic!.

Wakati hayo yakiendelea, nina swali moja la msingi, ambalo jibu lake linahitaji kajiutafiti kadogo ka kina na kupata uthibitisho wa kimaandishi kuwa "Hivi Kweli Huu Muungano uliounganisha Tanganyika na Zanzibar ni Kweli Upo Kisheria na Kihalali?!... au ni Dhana Tuu?!.
Kisheria ni legaly, kihalali ni legitimacy, kitu kinaweza kuwepo kisheria legally lakini kikawa ni illegitimate, kama ilivyo kwa process ya kutungwa kwa ujauzito ni mimba tuu kupachikwa, lakini mtoto anayezaliwa kama anazaliwa ndani ya ndoa ni legitimate na akizaliwa nje ya ndoa ni illegitimate, hivyo na kwenye mataifa ni vivyo hivyo kuna mataifa halali kisheria yanaitwa De Jure na kuna mataifa sio halali kisheria yanaitwa De Facto, jee Tanzania ni De Jure au De Facto?.

1. Kwa vile Tanganyika huru yenye kiti kule UN, na Zanzibar nayo ni nchi huru, yenye kiti kule UN, muungano wowote wa nchi mbili hizi, ulipaswa kwanza kutanguliwa na "Instruments" za Kimataifa za Union!. Instruments hizo, zilibidi ziridhiwe kwanza (Ratified) na Mabunge ya nchi hizo mbili kwa kuwa ratified instruments, kisha zitungiwe sheria local laws, hizo instruments na local laws zake zipelekwe UN na kuwa filed na kuwa internationalized kuwa za kimataifa kwanza ndipo viti vya Tanganyika na Zanzibar vingekuwa merged na kiti cha nchi mpya Tanzania kingepandishwa!.

2. Instuments za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilikuwa drafted as local treaty wakati zilipaswa ziwe ni an International Instruments na (Hati za Muungano), zikasainiwa na Nyerere na Karume haste haste bila wananchi wa nchi husika hizo kuulizwa!. Baada ya kusainiwa zilibidi ziwe ratified na Bunge la Tanganyika na BLM kule Zanzibar. Ni Bunge la Tanganyika tuu ndilo lili ratify tukatunga sheria ya Muungano, The Union Act, Jee kuna yeyote aliyewahi kuzisoma hizo hansard za bunge la Tanganyika likiratify Union Instruments au sheria ile ya muungano Union Act ilitungwa juu kwa juu?!.

3. Kwa upande wa Zanzibar, hakuna ratification yoyote iliyofanyika!, bali Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Abedi Amani Karume aliwaita Wanabalozi waliokuwepo Zanzibar na kuwaeleza kwa kauli kuwa BLM limeridhia kuratify zile Acts za Union na Instruments zake, lakini Zanzibar hakuna kikao chochote cha BLM kuujadili muungano, Hakuna andiko lolote la ratification kutoka Zanzibar, wala hakuna sheria ya muungano kwa Zanzibar!. Ratification is a process na kufanyika kwa maandishi!, na sio kwa kauli, na kufuatiwa ama kutungwa kwa sheria mpya ama ku domesticate international laws and international instruments kuwa local laws. Kwenye muungano hiki kitu hakikufanyika kwa Zanzibar!.

4. Kufuatia kukosekana kwa ratification ya upande mmoja wa Muungano, jee kiti cha Zanzibar kule UN, kilifutika futika vipi kule UN na nafasi yake kukaliwa na Tanzania bila hizo instuments kuwasilishwa rasmi UN?!.

5. Wakati fulani nikiwa NY, nilipata fursa kupita pale ubalozini kwetu UN, enzi hizo wife wa mwana jf mwenzetu akiwa ni receptionist, niliomba kumsalimia Balozi enzi hizo akiwa Daudi Mwakawago, Wabongo wakimuona mbongo ambaye sio mserikali hapo ubalozini , they treat you like a shit!. Baada ya kueleza shida yangu, nilielezwa maswali yangu nilipaswa kuyaleta kitambo kwa maandishi hivyo hayakupata majibu!. Miongoni mwa mambo niliyouliza ni copy ya International Treaty ya Union btn Tanganyika and Zanzibar iliyowasilishwa UN ili kufuta Viti vya Tanganyika na Zanzibar na Kuzaa Tanzania!. Sikuonyeshwa!.

6. International Treaties zote za Kimataifa zinazofika UN, zinahifadhiwa katika Maktaba Maalum, hutolewa copy na kuwekwa kwenye UN Open Library ambapo iko wazi kwa yeyote mwenye UN Access kuiperusi na kuisoma. Hivyo nilipokwenda kwenye UN Library, hakuna any International Treaty iliyopelekwa na Serikali ya Tanganyika kukifuta kiti chake UN wala iliyopelekwa na serikali ya Zanzibar kukifuta kiti chake!. Kilichopo kule ni Note Verbale ya Tanzania mpya kuumuarifu Katibu Mkuu wa UN kuwa Tanganyika na Zanzibar zimeungana!. Hiyo Note Verbale ndio taarifa ya awali, instuments zingefuatia!. Jee kuna Yeyote aliwahi kuziona hizo instuments?!. Hivi kumbe kiti cha nchi kwenye UN kinaweza kufutwa kwa Note Verbale tuu ya kutoka nchi moja bila any instruments zozote kuisupport hiyo NV ili kujustify huo muungano?!.

7.Niliwahi kwenda pale Ofisi za Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa, nikiamini kuwa classified documents are unclassified baada ya kipindi cha miaka 30!. Nikaomba kuziona hizo classified documents za Muungano!, nikaelezwa kuwa declassified documents zilizopo kwenye public access ni zile documents za mkoloni tuu!. Classified documents za Tanganyika huru na Tanzania huru , they are unclassified but haziko kwenye public open access!, ili uzione, unapaswa kuandika barua rasmi ya kuomba kuziona, ukieleza lengo la kuziomba ni nini?!. Nikauliza tuu jee Hati za Muungano zipo mle?!. Nilijibiwa zipo!. Barua sijaandika na hati zijaziona!. Jee kuna mtu yeyote amewahi kuziona hizo hati halisi za muungano?!.

8. Kama hati za Muungano, au Mkataba wa Muungano kama ule ulioletwa humu jf, ndio mkataba wenyewe!, Niliwahi kusema hauna sifa za kuitwa mkataba kwa sababu umekosa kipengele kiitwacho "Privity to contract" sambamba na kukosekana kipengele cha kuvunjika kwa mkataba!. Ili mkataba uwe na sifa ya mkataba, lazima kuwepo na kipengele cha itakuwaje endapo mkataba huo utavunjika!. Hati za Muungano hazikuwa na kipengele hicho hivyo huo haukuwa mkataba halali bali ni makubaliano tuu ya Muungano kati ya Nyerere na Karume, yasingefit hata kuwa filed kwenye Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa, seuze kufika UN?!.

9. Kwa vile sasa hoja kuu ya mjadala wa katiba ni serikali tatu kwa lengo la kuulinda muungano!, swali la msingi sasa ni jee huu muungano tunaotaka kuulinda upo kiukweli kweli kihalali na kisheria, au ni dhana tuu muungano kama wanandoa wawili wanapochukuana na kuishi pamoja kama mume na mke kwa dhana ya ndoa, baada ya kuishi miaka miwili kisheria wanakuwa ni wanandoa kabisa, ila pasipo na hati ya ndoa, wanandoa hawa wanakuwa wanaishi kwenye dhana tuu ya ndoa hata wakiishi miaka 100!. Sasa jee huu muungano wetu ni wa kweli au ni dhana tuu ya muungano?!.

10. Kwa vile Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ipo, naombani wenye muda fuatilieni kuziona hati hizo, kwavile MFA ipo, mliopo huko fuatilieni hizo instuments zilizopelekwa UN mtuonyeshe vinginevyo huu muungano wetu purported to exit is the biggest living lie in history!.

My Take:
Nahisi mara tuu baada ya muungano, kwa Nyerere na Karume kutia saini kwenye hati zile mbele ya kadamnasi ya watu!, wanasheria makini, waligundua hati zile zilikuwa defective na makosa ambayo hayarekebishiki!, Hati zile zingeonekana zingeufanya mkataba wa muungano kuwa ni void contract, usiorekebishika, ambapo zingeufanya muungano usiwepo abinitio!. Naamini kilichofuatia ni mkataba ule kuchanwa chanwa kuchomwa moto au kutumbukizwa chooni tena kwenye choo cha shimo kwa matumaini, ungetengenezwa mkataba mwingine proper na kusainiwa tena kimya kimya ambao ndio ungepelekwa hata UN!, jambo ambalo halikufanyika hivyo kuufanya huu muungano wetu kuwepo kwenye dhana tuu ya muungano ndio maana tumekuwa tukiyaongeza with no reference ya hati zozote ambazo they don't exist anymore.

Mwenye kujua lolote kuhusu uhalisia hili atujuze,
vinginevyo fuatana nami kuufuatilia Muungano kwa lengo la kuudumisha! na sio kuuchokoa ili kuubomoa!.

Wasalaam

Pasco.

Update: 1
Nimefanikiwa kuipata document ya ratification ya Muungano kwa bunge la Tanganyika. Document ya ratification kama hii ilipaswa kuwepo Zanzibar, ila kule haipo!. Hakuna ratification process yoyote iliyofanyika kwa Zanzibar kuuratify muungano zaidi ya kauli ya Karume kwa wanabalozi kuwa BLM limeridhia!. Rafication haifanywi kwa kauli, its a process inayofanyika kwa maandishi kama tulivyofanya Tanganyika!.​
paperclip.png
Attached Files
Update: 2
Nimefanikiwa kuipata Document Tanzania iliyoiwasilisha UN kuuthibitisha muungano wetu, ila pia bado kuna maswali bila
majibu, NV hii imeandikwa inawasilishwa akiandamana na mkataba, ila kiukweli mkataba haukuwekwa!.
 
Mh! Hebu compare hiyo mistari miwili - green na yellow. Sijawahi kusikia kitu kisichokuwepo kikawa na kero.

Ha ha ha ha,
Siku ingine ukinifanyie reference usiniwekee hizo rangi bana (Yellow & Green), nina addiction nazo.
Otherwise nilikua namaanisha Kero za Muungano ndizo zinavuma zaidi kwa sasa kuliko hata Muungano wenyewe.
 
Mkuu Pasco kwangu mimi kwangu hakuna kitu muungano! na hata wewe unajua unatuchora tu! kipo kitu kinaitwa Mgandamizo or the the bulshit called Muungano kati ya Tanganyika na Znz. kivipi? hicho kinachoitwa muungano ni mali ya viongozi tu wa Tanganyika na wananchi wa Znz. Ndo maana hata Rais anasigina katiba kwa kuteuwa mawaziri kuongoza wizara ambazo si za muungano anateuwa watu kutoka ZNZ (wizara ya Afya) wizara ambayo haipo ZNZ na Watanganyika tunashangilia tu kama mazuzu. Lakini pia Watanganyika hawawezi miliki kiwanja ZNZ lakini Waznz wanamiliki huku Bara. Mi nadhani kama ungekuwepo muungano halisi tungekuwa na uwezo wananchi wa pande zote mbili kufanya kila tunaloweza katika kujitafutia mkate wa kila siku sehemu yeyote ya muungano bila bughudha. Nakumbuka nimewahi kujaribu kwenda unguja siku moja zamani kidogo nikazuiwa kwa sababu sikuwa na hati ya kuingia znz. miaka ya 90. Nilipofanya utafiti mdogo wa kienyeji nikaambiwa eti sisi watanganyika tunaingiza tabia mbaya ZNZ ikiwemo Ujambazi!!!! Mtanganyika kwenda sehemu nyingine ya Muungano anapata uangalizi maalum ili asi spread wanachokiita tabia mbaya!!!!!! kweli mbona wao wanaleta tabia za kiliberali huku kwetu! utamaduni wa kiliberali mbona huku Tanganyika hakuna? Pasco fanya utafiti mdogo tafuta maliberali (mashoga) 10 hapo Dar 5 Tanga wahoji asili yao utaona maajabu! kwa Dar utakuta 6 wanatokea huko kusiko na tabia mbaya! nchi ya wastaarabu wengine utakuta wana asili ya Mombasa hivyo hivyo tanga na sehemu nyingine waliberali wanapopatikana. lakini pia hawa watu wananyonya sana Tanganyika zipo ntaarifa kuwa hata umeme hawalipi!!! umeme unaozalishwa tanganyika !!! na hata kama wakilipa hawalipi sawa na sisi! ndo muungano huo tunaotakiwa eti tuuenzi???? hapana na ifufuliwe TANGANYIKA sasa ili tuheshimiane sasa!
 
Mkuu Pasco kwangu mimi kwangu hakuna kitu muungano! na hata wewe unajua unatuchora tu! kipo kitu kinaitwa Mgandamizo or the the bulshit called Muungano kati ya Tanganyika na Znz. kivipi? hicho kinachoitwa muungano ni mali ya viongozi tu wa Tanganyika na wananchi wa Znz. Ndo maana hata Rais anasigina katiba kwa kuteuwa mawaziri kuongoza wizara ambazo si za muungano anateuwa watu kutoka ZNZ (wizara ya Afya) wizara ambayo haipo ZNZ na Watanganyika tunashangilia tu kama mazuzu. Lakini pia Watanganyika hawawezi miliki kiwanja ZNZ lakini Waznz wanamiliki huku Bara. Mi nadhani kama ungekuwepo muungano halisi tungekuwa na uwezo wananchi wa pande zote mbili kufanya kila tunaloweza katika kujitafutia mkate wa kila siku sehemu yeyote ya muungano bila bughudha. Nakumbuka nimewahi kujaribu kwenda unguja siku moja zamani kidogo nikazuiwa kwa sababu sikuwa na hati ya kuingia znz. miaka ya 90. Nilipofanya utafiti mdogo wa kienyeji nikaambiwa eti sisi watanganyika tunaingiza tabia mbaya ZNZ ikiwemo Ujambazi!!!! Mtanganyika kwenda sehemu nyingine ya Muungano anapata uangalizi maalum ili asi spread wanachokiita tabia mbaya!!!!!! kweli mbona wao wanaleta tabia za kiliberali huku kwetu! utamaduni wa kiliberali mbona huku Tanganyika hakuna? Pasco fanya utafiti mdogo tafuta maliberali (mashoga) 10 hapo Dar 5 Tanga wahoji asili yao utaona maajabu! kwa Dar utakuta 6 wanatokea huko kusiko na tabia mbaya! nchi ya wastaarabu wengine utakuta wana asili ya Mombasa hivyo hivyo tanga na sehemu nyingine waliberali wanapopatikana. lakini pia hawa watu wananyonya sana Tanganyika zipo ntaarifa kuwa hata umeme hawalipi!!! umeme unaozalishwa tanganyika !!! na hata kama wakilipa hawalipi sawa na sisi! ndo muungano huo tunaotakiwa eti tuuenzi???? hapana na ifufuliwe TANGANYIKA sasa ili tuheshimiane sasa!

Acha pumba,tabia mbaya uliyoiona ni uliberali?huo uliberali unaletwa zanzbr na wataliano wakiwafanyia wamasai na dada zako wa kitanganyika kwenye mahoteli,au hujui kuwa watanganyika ndio wengi huku kwenye mahoteli?tabia mbaya mlizonazo ni pamoja na kukata viungo vya albino,kuuwa vikongwe,ufisadi,ujambazi,wauwaji,ombaomba ....
 
De jure -muungano upo tena wenye misingi imara lakini
defacto -kero za upande mmoja zimechosha kiasi kwamba wengi wanahisi kama haupo
 
De jure -muungano upo tena wenye misingi imara lakini
defacto -kero za upande mmoja zimechosha kiasi kwamba wengi wanahisi kama haupo
Muungano uliopo was supposed to be dejure kwa mujibu wa sheria!. Bila ratification then muungano uliopo ni defacto na ukizingatia pia serikali iliyoingiza Zanzibar kwenye dhana muungano ni defacto!. Jee defacto na dejure zinaweza kufanya muungano dejure ?. Muungano wowote ambao wananchi hawakuulizwa, unakuwa ni defacto no matter how many papers zitasainiwa!.
Pasco.
 
Yote tisa..
kumi ni kuwauliza tu wananchi 'je huu muungano wanauhitaji'?

sio mtu kijiapiza kuulinda muungano wakati labda wananchi wenyewe washauchoka

Mkuu The B.Boss, kama muungano uliingiwa bila wananchi kuulizwa, kuna ubaya gani sasa ndio tukailizwa kabla ya katiba mpya?!.
P.
 
Mi nahisi upo. Kwani si kuna picha na video tunaoneshwa jinsi Tanganyika na Zanzibar zilivoungana? Mapembe sijui yale, yana mchanga wa Tanganyika na Zanzibar wanaweka kwenye chungu kimoja?
Angalizo: Ile 26 April wasije wakatuondolea holiday hata kama muungano utakufa. :p
 
mimi nachojua hakuna muungano ila kuna "ushirikiano wa kichama kati ya ri-chama la magamba kutoka bara na visiwani"
 
Binafsi nishauchoka...
Nyerere atakutokea ndotoni, utabadili mawazo!. Sisi wa Kanda ya Ziwa, baada ya kukaoa kabinti kabichi kadogo kazuri cheupe kama hako!, hakuna kukaacha hata kafanye visa vipi!. Tukikaacha tuu kataposwa tena nahisi na bwana wa Kiarabu!, si unaijua ile michezo yao!, watakiharibu bure!. Mke kama bado unampenda, huna sababu ya kumuacha kwa maneno ya vijiweni!. Wengine ni makuwadi tuu akishaachwa watageuka washenga!.

Tatizo kubwa la mke huyu ni ghubu tuu la kudai talaka rejea na high maintenance cost kitu ambacho ni normal kwa nyumba ndogo zote!.
P.
 
Mi nahisi upo. Kwani si kuna picha na video tunaoneshwa jinsi Tanganyika na Zanzibar zilivoungana? Mapembe sijui yale, yana mchanga wa Tanganyika na Zanzibar wanaweka kwenye chungu kimoja?
Angalizo: Ile 26 April wasije wakatuondolea holiday hata kama muungano utakufa.
Unazungumzia sherehe ya muungano ni kama misa tuu ya ndoa au sherehe ya ndoa, ndoa sio misa wala sherehe, ni hati!. Muungano sio kuchanganya udongo ni za muungano ambazo they are no where to be seen!. Kuhusu ile holiday, tukiufuta, tutasheherekea birthday ya Nyerere ni April.
P.
 
mkuu Pasco hivi wafikiri ni fursa sawia sasa kujadili uwepo ama kutokuwepo kwa muungano??

kwangu mimi sion kama uko sahihi kuhoji haya kipindi hiki manake kwasasa tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele na kile tunachokifikiri kwamba ndicho sahihi.

kama hati ya Muungano iliwekwa kapuni for decades ikatulazimisha kuishi maisha ya usiri yenye chembe za kudidimizwa na kukandamizwa ya kuamuliwa na watu 2 ambao may be walipendana na kwa interest zao wenyewe. Kwasasa watabganyika tumechoka sana na kiukweli hatuna haja ya kuendelea kujadili juu ya muungano bali tunanatakiwa tutoe maamuzi tu kwamba its either unavunjika ama tunakuwa na serikali 3 baasi.

so far mm kama mm nikiambiwa nikapige kura juu ya muungano nita vote usiwepo.
 
Last edited by a moderator:
fuatana nami kuufuatilia Muungano kwa lengo la kuudumisha! na sio kuuchokoa ili kuubomoa!.
Kwa hiyo ulipoanza na theme kwamba Watanzania hatujaruhusiwa kujadili uwepo wa Muungano ulikuwa unatuzuga? Maana na wewe unafanya yale yale, kunilazimisha eti nidumishe, nisivunje, Muungano, kama mtoto anaekataa kula, unampanua mdomo unamtumbukizia likijiko la uji wa jana kwenye koromea atake asitake. Don't force feed me ma idea yako ya kudumisha Muungano, wengine hatuutaki!

niliomba kumsalimia Balozi enzi hizo akiwa Daudi Mwakawago. Ilishindikana!. Wabongo wakimuona mbongo ambaye sio mserikali hapo ubalozini , they treat you like a shit!.
Wabongo waliku treat like shit? Umeibuka ofisi za UN kama tunavyofanya huku kwenye maofisi ya kiswahili ukataka eti kuonana na balozi out of the blue, bila agenda, bila appointment, bila proper forms of ID, lazima waku treat like shit!


Niliwahi kwenda pale Ofisi za Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa, nikiamini kuwa classified documents are unclassified baada ya kipindi cha miaka 30!
Tanzania kuna kitu kama hicho? Ukiamini nyaraka zinakuwa unclassified baada ya miaka 30, ukiamini kwa mujibu wa utaratibu upi, au kwa sheria ipi?

Barua sijaandika na hati zijaziona!. Jee kuna mtu yeyote amewahi kuziona hati hizo za muungano?!.
Wamesema andika barua ya kuomba hati za Muungano, wewe unasema barua sijaandika na hati sijaziona. So? Unatusaidia vipi? Au tukusaidie vipi? Utazionaje na barua hujaandika? Unalalamika wakati utaratibu wao ulikushinda, halafu unatuuliza sisi kama tumeziona, kwa nini wewe hukufuatilia huo mchakato upata hati wewe utuonyeshe sisi?

Kama hati za Muungano, au Mkataba wa Muungano kama ule ulioletwa humu jf, ndio mkataba wenyewe!, Niliwahi kusema hauna sifa za kuitwa mkataba kwa sababu umekosa kipengele kiitwacho "Privity to contract" sambamba na kukosekana kipengele cha kuvunjika kwa mkataba!. Ili mkataba uwe na sifa ya mkataba, lazima kuwepo na kipengele cha itakuwaje endapo mkataba huo utavunjika!.

Hati za Muungano hazikuwa na kipengele hicho hivyo huo haukuwa mkataba halali bali ni makubaliano tuu ya Muungano kati ya Nyerere na Karume, yasingefit hata kuwa filed kwenye Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa, seuze kufika UN?!.
Hebu nionyeshe source moja tu inayosema mkataba lazima uwe na kipengele cha kuvunjika na pia kipengele cha privity to contract, tafuta hata kitu cha kuunga unga kwenye world wide web nzima uonyeshe ni wapi umetoa hicho kitu!

kama wanandoa wawili wanapochukuana na kuishi pamoja kama mume na mke kwa dhana ya ndoa, baada ya kuishi miaka miwili kisheria wanakuwa ni wanandoa kabisa, ila pasipo na hati ya ndoa, wanandoa hawa wanakuwa wanaishi kwenye dhana tuu ya ndoa hata wakiishi miaka 100!. Sasa jee huu muungano wetu ni wa kweli au ni dhana tuu ya muungano?!.
Yani hii argument hii ina defeat theme yako nzima. Couples wakiishi pamoja miaka miwili unasema kisheria wanakua wanandoa hata bila hati za kuoana. Kwa hiyo unatuambia Muungano huu wa miaka 50 nao umeshakuwa muungano kisheria bila hati! Yani unatumia mfano wa ndoa ambao hauboreshi, unapasua, hoja yako ya kudai hati!

Jee kuna yeyote aliyewahi kuzisoma hizo hansard za bunge la Tanganyika likiratify Union Instruments?!.
Is that evidence kwamba hazipo? Just because we haven't read them? Hati ya Muungano hakuna mtu amewahi kuitoa hadharani tukaisoma, lakini ipo, kuna picha Nyerere na Karume wanasaini. Mimi na wewe hatujaisoma haina maana haipo.

Sababu tunazozitoa za udhaifu wa Muungano nazo ni dhaifu. Tunasema Muungano una matatizo kwa vile vile hatuna kumbukumbu za kuundwa kwake. Hapana, tunataka Muungano uvunjwe kwa sababu unaleta hasara, hauna manufaa, sio kwa sababu tumepoteza rekodi ya vikao vya mabunge au hati. Lakini hati si muhimu. Nani amewahi kuona hati ya makubaliano ya kuunganisha Sumbawanga na Mtwara ndani ya Tanganyika?


"Hivi Kweli Huu Muungano uliounganisha Tanganyika na Zanzibar ni Kweli Upo?!... au ni Dhana Tuu?!]
Muungano upo, ndio maana leo kuna news story ndege la Rais ameazimwa Maalim Seif akaenda kubebea mkaa na mikungu ya ndizi. Tunauvunja huu Muungano very soon.

Hayo ya juu yake ya kutusihi tudumishe muungano na ma analysis ya kisheria hayakuwa "my take"? Au ni mawazo ya nani yale? Au ulinuia kuandika "my conclusion ..." ???
 
Ha ha ha ha,
Siku ingine ukinifanyie reference usiniwekee hizo rangi bana (Yellow & Green), nina addiction nazo.
Otherwise nilikua namaanisha Kero za Muungano ndizo zinavuma zaidi kwa sasa kuliko hata Muungano wenyewe.
Muungano ndio kero, kama usingekuwepo huu muungano kero zingetokea wapi za huo muungano ? Tuuvunje au tuurekebishe muungano na sio kero za muungano, huwezi kukata matawi ikisha ukasema kwamba umeukata mti, kwanza tukate mti ndio tumalize na matawi.

Zanzibar kwanza
 
Muungano ndio kero, kama usingekuwepo huu muungano kero zingetokea wapi za huo muungano ? Tuuvunje au tuurekebishe muungano na sio kero za muungano, huwezi kukata matawi ikisha ukasema kwamba umeukata mti, kwanza tukate mti ndio tumalize na matawi.

Zanzibar kwanza

Hili dubwana halirekebishiki,ni kulivunja kila nchi ibaki huru,zanzbr kwanza.
 
Back
Top Bottom