Swali: Hivi mke au mume wa mtu ni nani hasa?

na wewe

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
231
397
Za mda huu wadau,

Tukiacha wale ambao wapo kwenye ndoa, nieleze msingi wa swali langu ili wadau muweze kutusaidia wale tusiojua maana ya mume au mke wa mtu.

Iko hivi, watu wengi hasa na mimi huwa tunasema kuwa, "Mimi siwezi tembea na mume au mke wa mtu" lakini katika mazingira fulani fulani, mtu huyo huyo anakuwa na mahusiano na mtu ambaye kwa namna moja au nyingine alishawahi kuishi maisha ya kindoa kwa muda fulani halafu akawa na maisha ya kipekee tena au maisha ya kisimbe.

Sasa je,
Msimbe sio mume au mke wa mtu?
Mtu aliyewahi kuishi maisha ya ndoa kwa zaidi ya miaka kadhaa na akazaa au hadi wakajenga huyo sio mke au mume wa mtu.

NB: Unaweza kuta mtu anasema huyu bado ni mke au mme wangu maana bado hatujapeana TALAKA. Kumbuka tayari hasa watu hawaishi pamoja lakini bado kuna mmoja anaamini kuwa bado ni mwenza wake, lakini wakati huo huo kitaratibu za ndoa kwa mfumo wa ndini, ni ngumu sana ndoa kuvunjika maana tunaamini alichokiungamanisha Mungu hakuna wa kukitenganisha.

Naomba wenye uelewa mpana katika hili mtusaidie.
 
Mkuu mbona hiyo rahisi sana kuelewa,haihitaji hata tuition. Mke wa mtu ni mke wa mtu.
 
Umeandika vyema kwa ufafanuzi ukauliza kisha ukajijibu mwenyewe,,Sasa sijui bado huelewi nini hapo?
 
Back
Top Bottom