Swali: Hivi kiyoyozi (AC) huwa kinatengeneza oxygen au kinapooza tu hewa iliyoko mahali husika?

Rekondoboshiki

JF-Expert Member
Nov 24, 2017
228
280
Hilo ndilo swali langu kwa sasa,
Hivi kiyoyozi (AC) huwa kinatengeneza oxygen au kinapooza tu hewa iliyoko mahali husika?
 
AC inazungusha hewa ile ile iliyopo ndani haiongezi wala kupunguza kitu. Kama ni split unit hewa ya moto inaingia juu inapita kwenye fins/radiator za chuma joto linachukuliwa na ile radiator linatolewa nje kupitia gesi iliyopo ndani ya AC hewa hiyo hiyo inatokea chini ikiwa imepoa.

Hili ni dhahiri kwa kuangalia tu kuwa hakuna sehemu ya kuingizia wala kutolea hewa kwenye split unit kuna bomba la gesi na maji ti.

Window unit ni yale yale sema muundo tofauti unaweza ukakuchanga ukafikiri hewa ya nje inaingia.
 
Ingekuwa inaingiza oxygen nisingekuwa naumwa kichwa nikiingia kwenye ofisi yenye AC au kwenye gari lenye AC.
 
Kwa kuongezea tu, majengo makubwa na marefu kama PSPF tower au Uhuru heights tower hua wanatumia 'forced air a/c systems' au 'central a/c'

Izi a/c ni special, zinatoa hewa nje, inaichuja, inaisafisha, inaipa ubaridi murua na kuiingiza ndani ( forced air) kwa kuipump kwa blower( ina watts za kutosha) na kuisambaza kwenye vyumba vya floor zote kuimarishsa ventilation, humidity na temperature control.

Ukiingia baadhi ya benki kubwa ukicheki kwenye ceiling utakuta kuna 'outlet grill' kwa ajili ya kuingiza hewa safi na baadhi chache kwa ajili ya kufyonza hewa chafu.
 
Ingekuwa inaingiza oxygen nisingekuwa naumwa kichwa nikiingia kwenye ofisi yenye AC au kwenye gari lenye AC.
wale team maalumu ya uokoaji wa mateka walipitishia wapi kupitia AC gesi yenye sumu/dawa ya kufanya magaidi na mateka wapatwe usimgizi?
ikiwa haiingizi wala kutoa hewa?
 
wale team maalumu ya uokoaji wa mateka walipitishia wapi kupitia AC gesi yenye sumu/dawa ya kufanya magaidi na mateka wapatwe usimgizi?
ikiwa haiingizi wala kutoa hewa?

Hiyo sio AC, ni ventilation system nzima ya jengo ambayo inahusisha AC na vitu vingine ikiwemo njia za kutoa na kuingiza hewa "Air Ducts", exhaust fans, dehumidifiers etc.
 
Back
Top Bottom