Swali: Hivi haiwezekani kupiga kura kwa kutumia simu zetu za mikononi

darubin ya mbao

JF-Expert Member
Aug 3, 2016
1,893
4,023
Itifaki imezingatiwa,

Niende moja kwa moja kwenye mada, nimekua nikijiuliza hili swali kwanini tusitumie simu zetu za mkononi kupiga kura, hii itaokoa muda , gharama na ile adha ya kuwataka watu wakapige kura kwenye vituo walivyojiandikishia.

Nimepata wazo hili baada ya kuona mfumo fulani wa ugawaji wa mbolea kwa wakulima ambapo mkulima anaingiza taarifa zake kwa maana ya jina, mahali anapoishi, na namba ya kitambulisho cha mpiga kura kisha mwishoni anaweka idadi ya hekari anazolima , sasa huu mfumo ukiingiza namba ya mpiga kura mara mbili itakwambia kitambulisho hichi kimeshatumika kufanya usajili

Na baada ya usajili huo taarifa za mkulima huonekana kwenye App ya YARA connect ambapo kila kitu alichoingiza kitaonekana pale, ukitaka kuona ninachokisema bonyeza *149*46*16# kisha fuata maelekezo ni rahisa na ipo user friendly

Pia kuna hii mifumo ya kununua vifurushi vya mitandao ya simu za mkononi inaweza kuwa modified kidogo tu na kuwezesha upigaji wa kura, kama ambavyo tunachagua aina ya kifurushi basi kwenye kura tunachagua wagombea tunaowataka

Hapo juu nimetolea kama mifano tu ili mada ieleweke kwa wepesi lakini najua wataalamu wa IT wanaweza kutengeneza mfumo wa USSD tofauti na hiyo niliyoielezea hapo , na hivyo kufanya zoezi la kupiga kura liende kidigitali.
 
CCM wataleta wataalamu wa kuchakachua na watapanga matokeo miaka 5 kabla ya uchaguzi.
 
Hiyo njia haitaaminika hata kidogo.
Kwa sababu chama kimojawapo watatumia pesa kuwakodi wadukuzi na kufanya udanganyifu halafu wananchi hawataelewa ukweli kwa maana kila mtu yuko nyumbani kwake.
 
Nadhani watanzania ndio tunaongoza duniani kwa kuwa na mapendekezo.
 
Tena hii ni hatari zaidi
yeah!
Haya makampuni ya simu kuna mengine yapo share na serikali ,vodacom walikuwa wanavujisha maongezi ya kina kinana na Membe ambao walikuwa makada wa CCM sembuse kura za wapinzani
 
Ni kweli mkuu kama hyo ya sasa hivi tu wananchi wanakwenda kupiga kura laivu,zoezi zima linaonekana wazi na kuna mashahidi wa kila chama na bado watu wanapindua matokeo halaf leo hii useme watu walale tu nyumbani watumie simu si ndio itakuwa hatari zaidi.
Watadukua balaa
 
Back
Top Bottom