Swali hili Baya na halikufaa kuulizwa Mbowe kutoka kwa kinywa Cha Rais

Kwanza nianze kwa kutoa kongole kwa wamama wote nchini Tanzania, nikiri kama wanavyokiri wenzangu ya kuwa nyinyi ni jeshi kubwa na nguzo imara kwa Taifa letu.

Pili nichukue fursa hii kumpongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakika nitakuwa mnafiki nisiposema kongole kwa kazi unayonifanyia ya kuliponya Taifa ambalo wewe enzi hizo ulishiriki kuliingizia kirusi maradhi ambacho Sasa unahangaika kuliponya hakika sie watoto wa mjini tunasema ULILIKOROGA Sasa UTALINYWA.

Tatu nitumie fursa hii kumpongeza kiongozi, ama Mwenyekiti wa chadema Taifa kwa hotuba yake aliyoitoa Jana mkoani Iringa hakika ni hotuba nzuri Sana ikiongozwa na ya mama Samia.

Kimsingi niende kwenye hoja

Moja ya kauli aliyoitoa Mbowe wakati akihutubia wakina mama wanachadema ni hii ''nilipo Toka gerezani nilipokea wito wa kuitwa Ikulu, NAMI nilikubali na nikatii kwenda siku ile ile, nilipofika Ikulu Mama Samia(Rais wa nchi)aliniuliza kwani Mbowe una shida gani''? ''Nikamjibu ya kuwa mama Mimi Sina shida''

Napata maswali mengi hapa;

Hivi ni Watanzania wangapi leo hii tunaweza itwa na Rais wa nchi na kuulizwa swali Ili na tukamjibu hivyo? Je Kwa Nini Rais aulize swali la namna hii kwa mtu kama Mbowe aliyekaa gerezani siku zote hizo?

Hivi pata picha swali kama hilo wangeulizwa wale wakina Pascally Mayala, waliotangaza kuacha uandishi wa habari Ili waende kuunga mkono juhudi Tena juhudi za ovyo kuitawala za akina mwendazake na wenzake wangeulizwa swali la namna hiyo wangejibuje?

Je Rais wa nchi ni sahihi kweli kumuita mtu Ikulu Tena haraka baada ya kutoka jera, na kumuuliza swali la namna hiyo swali ambalo halikuwa na masilai kwa wanachadema wote Bali masilai kwa Mbowe pekee?

Najiuliza swali kama ilo wangeulizwa wakina Mashinji, peter lijualikali,Halima mdeee Esteher Matiko na wenzake Nini kingejili kwa masilai ya Taifa?

Najiuliza swali Ili wangeulizwa wakina nani wale sijui wangejibuje?

Swali Ili ni swali fikirishi sanaaa najiuliza leo hii akiitwa Zitto zuberi kabwe angejibuje?

Najiuliza ningeulizwa Mimi leo sifi leo unashinda gani pale pale ningejibu Mimi nigeuze KIBARAKA wako,niwe kama MSIBA na mwendazake,ila unipe ruzuku. Na stori zingeishia pale kesho yake ningefungua kijarida kama kile kinaitwa sijui mwanahabari,sijui machinga na kusema wewe ndiye Mkombozi wetu na ningeweka PC Yako na picha mme yaani baba ambae ni mme wa Raisi nikasema wewe ni Jembe letu.

Mpaka Sasa najiuliza swali Ili angeulizwa Dr Slaa, walah sijui angejibuje jaman jaman nisaideni nyinyi mngejibu?
Mni ningejibu njaa tu mama
 
Aulizae ana akili zaidi, yaani sawa na kuuliza kwa nini unanitafuta? Unanifuata fuata? Unanionaje? Unanisumbua, unaniingilia, unanitibulia, hayo yote ni sahihi kumuuliza. Kumbuka kushika tu madaraka Mbowe akasimamia kidete katiba, mara akavamia tozo, mama ilimkera sana, akajiuliza mbona kipindi cha hawamu ya tano, kuhusu katiba akuitafuta kwa nguvu?
 
Mkuu kajifunze kwanza R&L ndiyo uje uandike tena
Acha zako. Jamaa kaandika vizuri sana na message delivered. Ni suala la mother tongue problem. Uliwahi mwona Mwendakuzimu akitofautisha "r" na "l" pamoja na PhD yake? "Nireteeni Gwajimaaaaaa...."!
 
Swali hilo lina maana kubwa sana linabeba!?? Sema Fasihi yako ndogo.

Mtafute Mwl. wa Kiswahili akupe darasa.
 
Kwanza nianze kwa kutoa kongole kwa wamama wote nchini Tanzania, nikiri kama wanavyokiri wenzangu ya kuwa nyinyi ni jeshi kubwa na nguzo imara kwa Taifa letu.

Pili nichukue fursa hii kumpongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakika nitakuwa mnafiki nisiposema kongole kwa kazi unayonifanyia ya kuliponya Taifa ambalo wewe enzi hizo ulishiriki kuliingizia kirusi maradhi ambacho Sasa unahangaika kuliponya hakika sie watoto wa mjini tunasema ULILIKOROGA Sasa UTALINYWA.

Tatu nitumie fursa hii kumpongeza kiongozi, ama Mwenyekiti wa chadema Taifa kwa hotuba yake aliyoitoa Jana mkoani Iringa hakika ni hotuba nzuri Sana ikiongozwa na ya mama Samia.

Kimsingi niende kwenye hoja

Moja ya kauli aliyoitoa Mbowe wakati akihutubia wakina mama wanachadema ni hii ''nilipo Toka gerezani nilipokea wito wa kuitwa Ikulu, NAMI nilikubali na nikatii kwenda siku ile ile, nilipofika Ikulu Mama Samia(Rais wa nchi)aliniuliza kwani Mbowe una shida gani''? ''Nikamjibu ya kuwa mama Mimi Sina shida''

Napata maswali mengi hapa;

Hivi ni Watanzania wangapi leo hii tunaweza itwa na Rais wa nchi na kuulizwa swali Ili na tukamjibu hivyo? Je Kwa Nini Rais aulize swali la namna hii kwa mtu kama Mbowe aliyekaa gerezani siku zote hizo?

Hivi pata picha swali kama hilo wangeulizwa wale wakina Pascally Mayala, waliotangaza kuacha uandishi wa habari Ili waende kuunga mkono juhudi Tena juhudi za ovyo kuitawala za akina mwendazake na wenzake wangeulizwa swali la namna hiyo wangejibuje?

Je Rais wa nchi ni sahihi kweli kumuita mtu Ikulu Tena haraka baada ya kutoka jera, na kumuuliza swali la namna hiyo swali ambalo halikuwa na masilai kwa wanachadema wote Bali masilai kwa Mbowe pekee?

Najiuliza swali kama ilo wangeulizwa wakina Mashinji, peter lijualikali,Halima mdeee Esteher Matiko na wenzake Nini kingejili kwa masilai ya Taifa?

Najiuliza swali Ili wangeulizwa wakina nani wale sijui wangejibuje?

Swali Ili ni swali fikirishi sanaaa najiuliza leo hii akiitwa Zitto zuberi kabwe angejibuje?

Najiuliza ningeulizwa Mimi leo sifi leo unashinda gani pale pale ningejibu Mimi nigeuze KIBARAKA wako,niwe kama MSIBA na mwendazake,ila unipe ruzuku. Na stori zingeishia pale kesho yake ningefungua kijarida kama kile kinaitwa sijui mwanahabari,sijui machinga na kusema wewe ndiye Mkombozi wetu na ningeweka PC Yako na picha mme yaani baba ambae ni mme wa Raisi nikasema wewe ni Jembe letu.

Mpaka Sasa najiuliza swali Ili angeulizwa Dr Slaa, walah sijui angejibuje jaman jaman nisaideni nyinyi mngejibu?

subiri matusi kutoka chaggadema
 
Back
Top Bottom