SWALI GUMU: Kwani Nape alishachukua maamuzi gani baada ya maoni ya kamati yake?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kuna watu hua tunaishia kulalamika bila hata kua na sababu za msingi na kwa mihemko ya ajabu ajabu, nauliza swali hili kwa makusudi mazima kabisa tuone jinsi ambavyo Mh Nape alionewa bila sababu za msingi.

Nape Nnauye aliunda kamati teule,ikaanza kazi ndani ya masaa 24 na baada ya kumaliza kazi hiyo ilimkabidhi maoni yake juu ya uchunguzi iliyoufanya.Kama waziri liipokea ripoti ya uchunguzi na hakufanya maamuzi yeyote zaidi alisema kuwa yeye ataikabidhi kwa walio juu yake.Je, Waliokua juu yake waliipokea ripoti ya kamati?

Mamlaka zilizo juu ya iliyokua wizara ya Mh Nape zingeipokea ripoti ile, zikaifanyia kazi na kama zisingeridhika nayo basi wangemkatalia na sio kumwadhibu kwa kumtoa ndani ya wizara.Hlikua jambo jema hata kidogo maana lilijaa hasira na Makosa lukuki ya kiutendaji. Odherwise iwe ni kweli Mh Nape aliandika barua ya kujiuzulu yeye mwenyewe kabla.Je, pamoja na hayo yote hiyo ilikua sababu ya kufikia maamuzi ya kumwadhibu?

Kwa mantiki hiyo haikua uamuzi sahihi kumwachisha Nape kazi kama waziri maana hata taarifa za kamati yake hazikufanyiwa kazi.Kwa lugha sahihi ni kwamba alionewa waziwazi.
 
Kulingana na kilichotokea, alie juu alitambua kabisa Nape angeweza kujiuzulu kama hatua zozote zisingechukuliwa dhidi ya kijana yule! akaona ni bora amtumbue haraka kabla ya yeye kujiuzulu na kumpa credit alikuwa mwanahabari huyo.
 
Back
Top Bottom