Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Korona 2.0 Kwani Rais ana Ubia na Maisha Yenu?
Na. M. M. Mwanakijiji
Naandika kama shabiki wa Magufuli; naandika kama mtu ambaye nimeelewa malengo yake na mitazamo yake, na ninaandika kama mtu ambaye sijaegesha akili yangu mahali mwenyewe nikaondoka. Nimesoma na kufuatilia mijadala ya kile kinachodaiwa kuwa ni wimbi la pili (2.0) la maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) ambayo yanasemekana yanaendelea nchini mwetu. Wapo wengi ambao wanamuangalia Rais awape mwongozo wa nini cha kufanya na kwa kiasi kikubwa wanafanya hivyo kwa sababu Rais ndio kiongozi mkuu wa serikali na nchi.
Neno la Rais lina uzito wake, hofu za Rais zina uzito wake na ikumbukwe kuwa wengi wanachukulia kuwa kwa vile Rais ana watu wengi wanaomzunguka basi ana taarifa za mambo mengi ambayo labda watu nje ya serikali hawana. Aliposema watu wajifukize, mamilioni walijifukiza, aliposema watu wafunge na kuomba, watu walifunga na kuomba, aliposema watu waiage korona watu walifanya na send off! Na alipotangaza kuwa korona hakuna Tanzania na kuwa imekwisha watu waliamini hivyo.
Sasa hili wimbi la pili ni kweli? Kama ni kweli je Watanzania wafanye nini? Je, watu wanaokufa ni kweli wote wanakufa kwa korona au magonjwa mengine? Na kama wimbi hili kweli lipo kama nchi tufanye nini na kama mtu mmoja mmoja tufanye nini? Ni wazi msimamo wa serikali umetolewa na Rais jana huko Chato na kuwa hakuna mtendaji wa serikali atakayepingana na Rais kwenye hili isipokuwa kama yuko tayari kujiuzulu akipinga (resigning in protest). Kwa vile msimamo wa serikali unajulikana na kuwa serikali haitaleta lock down, na kuwa hata chanjo watu wafikirie mara mbilimbili basi sehemu ya nini kila mtu afanye ndio swali linalohitaji kujibiwa.
Ndugu zangu naandika kama shabiki; Watanzania msijitoe ufahamu na mkajifanya nyie fyatu! Rais si mbia wa maisha yenu, ya mababa na mama zenu, na wala si mbia wa maisha ya watoto wenu! Mnapougua, kuuguza na kuuguliwa yote hayo ni yenu; mauti yakiwafikia vilio ni kwenye nyumba zenu, jamaa, ndugu na marafiki zenu. Sasa kama hili ni kweli, kwanini watu wengine wafikiri wanaweza kuifanyia ibada imani ya mtu mwingine? Hivi, mnajua kwanini mitume wengine hawakuungana na Petro kujaribu kutembea juu ya maji japo wote walimuona Yesu akitembea juu ya maji na walimsikia Yesu akimwambia Petro atembee? (Mathayo 14:22-33).
Rais Magufuli anaweza kuwa na imani kubwa kabisa hata ya kutembea juu ya maji na akatembea; lakini wangapi wanaamini kama yeye? Kama imani yako haijafikia ile ya Magufuli sasa unakanyaga maji ya nini?
Ndugu zangu kuna njia tatu/nne kubwa na za haraka za kupunguza maambukizi ya corona:
1. Vaa barakoa iliyotengenezwa na kitambaa cha pamba (siyo hariri). Kuvaa barakoa kuna kulinda wewe na kinamlinda mwingine. Ukivaa barakoa funika pua na mdomo (korona inaingia zaidi kupitia puani!)
2. Osha mikono kwa sabuni mara kwa mara; epuka kusalimiana na watu kwa kushikana mikono. Ikitokea hivyo hakikisha huingiza vidole midomoni au puani (jitahidi kuosha kabla ya kufanya hivyo na baada).
3. Jiweke umbali wa karibu mita moja kutoka kwa mtu mwingine ambaye si wa nyumbani mwako. Na hii inaendana na kuepuka misongamano isiyo ya lazima hasa mahali ambapo watu hawavai barakoa. Na wale wenye ndugu (wazazi, mababu wazee) waambieni wasiende makanisani au misikitini kwa wakati huu au makanisa na misikiti iweke taratibu za kuhakikisha watu wanakaa mbalimbali na wanavaa barakoa!
4. Jifukize nyungu; sijui ni kwa namna gani hii ilisaidie kuzuia wimbi la kwanza lakini kama watu watafanya tena na kwa wingi wao mnaweza kujikuta mnazuia tena wimbi hili la pili maana kama ni chanjo msijipe matumaini saini.
Njia hizo tatu ndio njia zitakazokinga maisha yako na maisha ya wale uwapendeo. Lakini kama unafikiria Rais ana ubia na maisha yako haya we. Kwa sababu lile swali la bahati nasibu ya Magufuli kama italipa bado linasimama.